Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Chama Cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania, TCCIA Kimefanya Uchaguzi Mkuu na Kumchagua Kwa kushindo Mwenyekiti aliyemaliza muda wake , Wolter Maeda ambaye alitetea nafasi yake kwa kupita bila kupingwa.
Uchaguzi huo ambao hufanyika kila baada ya miaka minne ,uliambatana na Mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho,ambapo mfanyabiashara Maeda alishinda kwa kushindo kwa kupigiwa kura zote za ndio baada ya kutojitokeza kwa mpinzani wa kushindana naye kuwania nafasi hiyo.
Wengine waliochaguliwa katika Mkutano huo ni pamoja na Alphonce Lema ,Makamu mwenyekiti kitengo Cha Biashara, Olais Monaban,Makamu mwenyekiti kitengo Cha Viwanda na Suleiman Nkya Makamu mwenyekiti kitengo cha Kilimo.
Akiongea mara baada ya Mkutano huo mkuu kumalizika ,mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi , Privanus Katinila alisema kuwa Mkutano huo umezingatia jenda na kuwachagua viongozi watakaowasaidia wafanyabiashara kuondoa changamoto mbalimbali katika kukuza uchumi wa Taifa.
Katinila ambaye ni afisa biashara jiji la Arusha,aliwataka viongozi waliochaguliwa kuwa na jukumu la kuimarisha chama hicho kwa kuwaunganisha Wafanyabiashara ili kukuza sekta ya kilimo na biashara katika kukuza uchumi wa mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake mwenyekiti mpya wa TCCIA Mkoa wa Arusha, Wolter Maeda pamoja na kuwashukuru wajumbe kwa kuonyesha imani kubwa kwake alisema jukumu lake kubwa lililopo mbele yake ni kuwaunganisha Wafanyabiashara ili chama hicho kiwe msaada mkubwa kwa Wafanyabiashara katika kukuza uchumi .
"Nawashukuru Sana wajumbe kwa kunichagua na kupata menejimenti mpya nataka chember yetu ijulikane kote duniani ,katika janga la Corona tulipotezana Ila kwa Sasa lazima tuungane na kushirikiana, tuishi na janga hili la Corona na tufanye biashara zetu vizuri na tukuze uchumi wa nchi yetu"alisema
Alisema janga la Corona lisiwe sehemu ya kurudisha nyuma uchumi wa Taifa letu Ila liwakomaze Wafanyabiashara waweze kuimarisha biashara zao.
Awali afisa mtendaji wa TCCIA,Sia Matunda alieleza mafanikio ya Chember katika kipindi Cha miaka minne ni pamoja na kuwawakilisha vyema Wafanyabiashara katika Baraza la Wafanyabiashara Ikulu Dar es Salaam na kueleza changamoto mbalimbali za Wafanyabiashara.
Pia wamefanikiwa kuwasilisha mapendekezo ya Kodi kwenye kamati za bunge,kuimarisha mabaraza ya Wafanyabiashara wilayani na Mkoa,kujenga Chember imara kwenye wilaya ,kuongeza wanachama hadi kufikia asilimia 70.
Alisema pamoja na mafanikio hayo changamoto kubwa bado ni janga la Corona hata hivyo aliwashauri Wafanyabiashara kuendelea kuishi na ugonjwa huo na kubuni masoko ya ndani zaidi kuliko kutegemea masoko ya nje ambayo yamepigwa na janga la Corona.
"Tunalenga kujiimarisha kifedha ili kuweza kuwafikia Wafanyabiashara na kujenga Chember ngazi ya wilaya zitakazosaidia kutatua kero za wafanyabiashara ."alisema Matunda.
End....