Maduka ya Kariakoo kufunguliwa hadi usiku

Maduka ya Kariakoo kufunguliwa hadi usiku

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,100
Reaction score
34,915
Kova1%2817%29.jpg

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulemani Kova

Polisi kwa kushirikiana na wafanyabiashara jijini Dar es Salaam, wameanzisha mchakato wenye lengo la kuyafanya maduka yaliyopo Kariakoo yafanye kazi hadi saa sita usiku.
Kwa mujibu wa utaratibu uliopo sasa, maduka hayo yanafungwa ifikapo saa 12:00 jioni.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulemani Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa, jeshi hilo linawasiliana na wafanya biashara wa eneo hilo, ili kuanza majadiliano.

Alisema hatua ya maduka hayo kufunguliwa hadi saa sita usiku itasaidia kuongeza kipato cha wafanyabiashara, kukuza uchumi na kupunguza msongamano wa watu.
Kwa mujibu wa Kova, masuala ya msingi yatakayopewa kipaumbe katika mchakato huo ni yanayohusu ulinzi na usalama.
Kova alisema majadiliano hayo yamelenga kuimarisha ulinzi wa kutosha katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu ya kuweka taa kubwa na kufunga kamera za kuwabaini wahalifu.

Pia alisema mchakato huo utajumuisha kuanzishwa njia za simu ambazo zitatumika kwa haraka katika kutoa taarifa za uhalifu.
"Hatua hii itawasaidia hata watu wanaotoka kazini jioni, kwenda madukani kununua bidhaa pasipo uharaka wala msongamano,” alisema.
Alisema jambo la muhimu kwa wafanyabiashara hao ni kuzingatia masharti yanayohusu ulinzi.

Wakati huo huo jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watu 11 wanaosadikiwa kuwa majambazi sugu, wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali jijini hapa.
Miongoni mwa makosa hayo ni ujambazi wa kutumia silaha, wizi wa televisheni, pikipiki za miguu mitatu bhangi na gongo.
Kova alisema kuwa bado wanaendelea na operesheni ya kuwasaka majambazi sugu kwa lengo la kuondoa uhalifu jijini humo.

CHANZO: NIPASHE
 
Utafikiri polisi, wafanyabiashara na wezi wanashirikiana. mji hauna taa barabarani ni giza totolo then unataka wananchi wabebe mali usiku wakitegemea kulindwa na kamanda Kova khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

Hadithi njoo utamu kolea. .... ...
 
hapo zamani za kale palitokea kariakoo watu walikuwa wanafanya shopping mpaka saa sita za usiku.....he he he he heeeee
 
kama anamaanisha anachoongea basi kova wa ukweli lakini mimi nashindwa kuelewa kwa nn wanashindwa kuweka camera?? Kamera inaleta discipline ya hali ya juu ila sijui manake wezi wanaiba mchana pee na hawakamatwi sembuse usiku?? Hili ni dili Kova keshapewa mchongo na mafia watampa cha juu sasa ole wake atakayeenda saa sita usiku kufanya shoping.
 
Mchana inawashinda, usiku si itakuwa balaa!
 
kama anamaanisha anachoongea basi kova wa ukweli lakini mimi nashindwa kuelewa kwa nn wanashindwa kuweka camera?? Kamera inaleta discipline ya hali ya juu ila sijui manake wezi wanaiba mchana pee na hawakamatwi sembuse usiku?? Hili ni dili Kova keshapewa mchongo na mafia watampa cha juu sasa ole wake atakayeenda saa sita usiku kufanya shoping.

hali ilivyo sasa: mfanyabiashara anatoka kkoo saa 12 anafika kimara saa 2 usiku anakuta majambazi wanamsubiri mlangoni, wanachukua chao na roho yake, polisi wanapigiwa simu wanakuja saa6 ucku. Chondechonde mr kova, tumechoka kusoma misa ya wafu kwa marehemu aliyeuwawa kwa binduki.
 
mjomba nakubaliana na wewe.Basi Kova kama hajatumwa na wala sio kampeni basi aimarishe ulinzi na jiji liwe safe hayo mambo mengine automatically yatafuata. Weka taa kila sehemu na CCtv czmera . Wala sio bei kubwa kusema kwamba serikali inashindwa.
 
Hili la Kamanda Kova ni wazo Zuri!, tusiwe too negative!
Kova ndiye anataka watu wafanye shopping usiku au ni wananchi wenyewe? Hajasema hilo wazo limetoka wapi. Huo usafiri wa kuwabeba watu na shopping zao usiku utatoka wapi? Kova anapenda sana kuongea na vyombo vya habari. Ameona uchaguzi umemfunika akaona aje na hekaya hii.
 
hiyo biashara itafanyikaje, maaana Taa zitakuwa kwenye maduka tu lakini miguu michache ukitoka kariakoo unakabwa na kuchukuliwa kila kitu, kama mchana wanashindwa kudhibiti, wataweza usiku?
 
Back
Top Bottom