Madudu ya Trafic Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madudu ya Trafic Mbeya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nyandulu, Jan 21, 2011.

 1. n

  nyandulu Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KAMANDA MPINGA HILI NALO LIANGALIE KWA MACHO MAWILI.
  Jamani wana JF hivi ni lini Watanzania wataishi katika nchi yao bila kunyanyasika ebu sikieni yanayofanyika hapa Mbeya , Vituko vya wenzetu wa jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani vijana wa Mpinga.
  Kwanza kuna mtu anaitwa MGENI, @ Obama huyu ni RTO anacheo cha ASP (assistant Suplitendant of Police) Huyu bwana kweli kajitahidi sana kurekebisha usafiri wa daladala hapa mkoani, mambo ya wrong parking, kukatisha route, usafi wa madereva na kondakta, pia kuweka alama (numba) kubwa ubavuni mwa kila gari na nyuma maandishi yanayo onyesha route ya gari, hapo kila mtu anasifia.
  Haya waswahili hawakusema uongo pale wiliposema Mgema akisifiwa Tembo hulitia Maji, na kweli Obama sasa tembo kalichakachua.
  - Unyanyasaji wanaofanyiwa hawa madereva ni kinyume kabisa na haki za binadamu, kupigwa, matusi, kuwekwa rumande bila sababu mbaya zaidi mtu anakaa zaidi ya masaa 24 mahakamani hapelekwi na hakuna dhamana wala hakuna askari atakae mtoa isipo kuwa ASP Mgeni, akikutoa rumande hakuelezi kosa anakwambia potea, fikiria sasa umewekwa rumande kosa hujui mahakamani hukupelekwa usomewe kosa lako, je? Kama sio kuwanyanyasa raia wasio na hatia ni nini?
  - ASP Mgeni amekuwa n a utaratibu wa kufanya vikao na wamiliki wa vyombo vya usafiri na wahudumu katika sekta hiyo pamoja na watu wa Sumatra na wadau wengine. Ni jambo jema sasa kituko ni kwamba mikutano hii haina tija kwa maana yeye ndie mtoa hoja na mjibu hoja hizo, hakubali hoja wala maoni kutoka kwa wadau hao, akisema amesema, Kiongozi wa Sumatra mkoa Bw Amani hana sauti kwa ASP Mgeni @ Obama hata kwa hoja zile zinazo ihusu Sumatra yenyewe.
  - ASP Mgeni amekuwa ni kero sasa badala ya kuwa msaada kwa wananchi hata polisi wenzake wanamshangaa, kunasiku moja majira ya jioni katika maeneo ya SINDE alisimamisha magari kwa maana ya kufanya ukaguzi akiwa yeye na askari wawili katka zoezi hilo walisimamisha magari zaidi ya kumi na ukaguzi wa gari moja huchukua masaa kadhaa sasa kwa bahati mbaya sana kuna gari moja aina ya Toyota Mark II lilibeba mama mjamzito aliyekuwa akipelekwa katika hospitali ya rufaa, Dereva wa gari hilo alishuka na kuomba akaguliwe ili amuwahishe huyo mgonjwa hospitali, kauli aliyopata kutoka kwa Obama inasikitisha – (mgonjwa kwani hiyo ni amburance issue kama ni kuzaa hata hapo kwenye gari anaweza kujifungua)
  - Kali zaidi ni hii, yeye kama RTO ametoa maelekezo kwa Traffick wote kukusanya Tsh 1000 kwa kila daladala kila siku kwa mfano kutoka Uyole mpaka stend kuu utakuta vituo vitano vya Traffick kila kituo unaacha book hivyo daladala moja inaacha inatenga Tsh 5000, kila siku ukizidisha mra siku 30 = 150,000 zidisha mara daladala kama 200 zilizo kwenye route hiyo ni tsh approximaterly tsh 30,000,000 pato la hawa jamaa kwa mwezi. Hapo ni gari isiyo na makosa, kama umepatikana na kosa unatozwa kuanzia Tsh 5000 hadi 50,000 usipelekwe mahakamani,
  - Mbali na huyo Obama kuna msaidizi wake Henry na askari mwingine wanamwita mlugaluga hawa ni wanyanyasaji wakubwa . kuna mgomo wa daldala umeanza tarehe 20/01/2011, sababu ni watu kukataa kunyanyaswa . Jamani wana JF hii yaweza kuwa Richmond nyingine, hebu ijadilini.
  - Kamanda Mpinga kama kweli unania njema na hawa maskini wa Tanzania hebu take action Jambo afande

  -
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Poleni na maswaibu ya Police huo mbeya. Wasalimie wazee wa Ilemi!
   
Loading...