Madudu ya Morogoro Paralegal yasiachwe yaendelee

Madudu ya Morogoro Paralegal yasiachwe yaendelee

Status
Not open for further replies.
LETA huo ushahidi maana hili shirika nalijua njia za huyu mama nazitambua kaliharibu shirika zuri lilokuwa lilete manufaa kwa wanawake na wananchi kinachoniuma zaidi ni kwamba yeye na huyo mhasibu Da Regina wanavyoiba hela kujinufaisha hadi huyo dada kanunua Harrier.
Pia kufoji report zinazoenda kwa wafadhili afu hela wanazitia kibindoni na kufanyia miradi kebekebe :disapointed:
 
hizo ni chuki binafc tu, matunda ya Morogoro paralegal yanajulikana mkoa wa Morogoro na ina mchango mkubwa kwa paralegals mkoani Morogoro. huyu mama amekuwa akiweka juhudi zake binafc ktk maendeleo ya hiyo NGO na co wizi km unavyodai coz maisha yake na familia yake ni ya kawaida mno kiac kwmb unaweza ucjue km ni mkurugenzi ukilinganisha na wakurugenzi wng wny majumba, magari na vitega uchumi kibao kwa ajili ya familia zao kwa kutumia fedha za wafadhili.

kwa hy hayo madai yake hayana ukweli wwt ni unafiki tu. nahic utakuwa umetoswa kwny mradi ww c bure. mama fanya kazi yako achana na maneno ht kwny kanga yapo!
 
hahahahaaha umeishiwa wewe anzisha ya kwako km unaona ni dili utaisoma namba... muache mama wa watu afanye kazi zake kwa manufaa ya jamii kwa sababu ht manufaa mengne huwezi kuyaona kwa macho km vile elimu itolewayo kwa wanajamii kuhusu mambo mbalimbali huwezi kusema hawafanyi kitu huo ni unafiki na wivu uco na maana. ww una yako, mama Masoy songa mbele mama kazi zako tunazitambua na ht wafadhili wanalijua hilo kwani mchango wako kwa Paralegal wa Morogoro na jamii kwa ujumla tunauona.
 
Naitwa Amani Mwaipaja-Mwanasheria Mshauri, Mtafiti na Mtetezi wa Haki za Binadamu. Nimekuwa Mwanasheria wa Morogoro Paralegal tangu mwaka 2007 hadi leo hii.
Baada ya kupitia maelezo ya Inkognito kuhusu Morogoro Paralegal, napenda kutoa taarifa za awali kuwa habari zilizoandikwa na Iknognito ni za Kizushi na uposhaji mkubwa wenye wenye lengo la kuharibu taswira, picha na hata kuleta uchonganishi kati ya watendaji wa Morogoro Paralegal, wafadhili na wapenda maendeleo wengine.

Kwa kifupi, nimeshiriki kwa ukaribu sana katika kuiandika katiba ya Morogoro Paralegal, naifahamu vizuri katiba ya Morogoo Paralegal, nafahamu utendaji wa Bi. Flora Masoy na hata wadau wanaoendelea kuunga mkono kazi nzuri za Morogoro Paralegal.

Hapo baadae, nitaweka UZI wangu binafsi kuhusu Morogoro Paralegal na nitaomba wasimamizi wa mtandao huu wasiouhamishe uzi (post)huo ili usichanganywe madudu ya Inkognito.

Kwa kifupi ni Kwamba, tuhuma zote alizozitoa Inkognito ni za Uzushi, hajazifanyia utafiti na inawezakana hata ni mkusanyiko wa maneno ya kuokoteza yenye lengo la kumchafua Mkurugenzi wa Kituo hicho Bi. Flora Masoy. Nitatuma post hiyo yenye Title UKWELI KUHUSU MOROGORO PARALEGAL muda si mrefu. Naomba Kuwasilisha.

Asante Moderator

Amani Mwaipaja
Mwanasheria Mshauri
Mobile: 0787-070707
 
Jaman kweli dunia Sio mbaya ila walimwengu ndio wabaya. Mama huyu kama angekua anakula pesa za miradi angalau hata angetengeneza ka nyumba kake. Inkognito wewe una chuki binafsi tu. Moroparalegal msikate tamaa na kazi yenu kubwa mnayoifanya kutetea haki za binadamu. Mungu anaiona
 
LETA huo ushahidi maana hili shirika nalijua njia za huyu mama nazitambua kaliharibu shirika zuri lilokuwa lilete manufaa kwa wanawake na wananchi kinachoniuma zaidi ni kwamba yeye na huyo mhasibu Da Regina wanavyoiba hela kujinufaisha hadi huyo dada kanunua Harrier.
Pia kufoji report zinazoenda kwa wafadhili afu hela wanazitia kibindoni na kufanyia miradi kebekebe :disapointed:

Kama wangekua wanaiba auditors si wangeshagundua? Au hua hakuna ukaguzi kwenye mahesabu jaman? Kwa elimu yangu ninachojua hela za miradi hua zinatolewa report ya mapato na matumizi.
 
Naitwa Amani Mwaipaja-Mwanasheria Mshauri, Mtafiti na Mtetezi wa Haki za Binadamu. Nimekuwa Mwanasheria wa Morogoro Paralegal tangu mwaka 2007 hadi leo hii.

Baada ya kupitia maelezo ya Inkognito kuhusu Morogoro Paralegal, napenda kutoa taarifa za awali kuwa habari zilizoandikwa na Iknognito ni za Kizushi na uposhaji mkubwa wenye wenye lengo la kuharibu taswira, picha na hata kuleta uchonganishi kati ya watendaji wa Morogoro Paralegal, wafadhili na wapenda maendeleo wengine.

Hapo baadae, nitaweka UZI wangu binafsi kuhusu Morogoro Paralegal na nitaomba wasimamizi wa mtandao huu wasiouhamishe uzi (post)huo ili usichanganywe madudu ya Inkognito.

Ukishaweka huo uzi naomba unitag.
 
Acha ukenge wewe kwani lengo la kuanzisha hyo NGO ni kula fedha? Au wahisani wanatoa fedha kwa ajili ya huyo mama ili azile yeye na familia yake? Jipange nyie ndio mnaorodisha taifa nyuma kwani ndio mnaonufaika na ufisadi serikalini na kwenye hayo ma NGO.

Kama kungekua na wizi NGO ingeshakufa siku nyingi kwasababu miradi isingefanikiwa inkognito ungeuliza wenzako wenye ujuzi wakuambie jinsi mahesabu yanavyoenda Sio kukurupuka na mada za kuokoteza
 
Bwana Inkognito epuka majungu na Fitina, wasioelewa watafurahia ushabiki wa taarifa hii. Huyu bwana Inkognito anahitaji maada. Angalia vizuri majibu yake katika post ya mwisho. Bila shaka alikuwa anafanya kazi katika mradi mmojawapo akaondolwa kazini ghafla!

Pia nina mashaka na uzoefu wake katika ajira.

Umri pia ambao bila shaka uko chono ya miaka 25 ambao kwa kawaida umejaaa shauku bila udadisi wa kina ukizingatia hisia kuliko uhalisia.

mashirika yanayoanzishwa na watu kama hawa yana misukosuko mingi sana, kimfumo, masharti ya wafadhili nk ambayo mwisho wa siku maamuzi mengine huwa hayahitaji kumfurahisha kila mtu, bali kutimiza lengo la huduma husika.

natamani nipate mlengwa aliyepata huduma hapo ili atupe upande wa pili wa shilingi.

Uzoefu unaonyesha mtu kama huyu hajui hata proposal inaandikwaje na ndio mtu wa kwanza kudai ongezeko la mshahara bila kujali kiongozi wa shirika husika amapata shida kiasi gani hata kupata huo mshahara wake.

Kituo hiki kuwepo tangu 1993 mpaka leo 2013 miaka ishirini ya utoaji huduma? Ninavyojua uongozi wa mashirika haya ulivyo mgumu, ninampongeza sana mama Flora Masoy.

Natamani siku moja uanzishe shirika lako au uwe kiongozi wa taasisi fulani uonje ugumu wa kuwa kiongozi. Nina uhakika utarudi kumuomba radhi huyu mama na kutambua kile unachofanya. Hoja yako imepitiliza kuweza kupimwa kama hoja yenye mashiko, imekaa sana kibinafsi kuliko kiutendaji ndugu
Inkognito.
 
Umedhulumiwa ndomaana umekuja kusema.tuanze namleta Uzi wewe umekula ngapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom