ndiyomkuusana
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 668
- 426
na Josephat Isango
UJENZI wa mji mpya wa Kigamboni huenda ukakwama baada ya wananchi kudai kuwa serikali imekuwa ikikiuka sheria na mambo ya msingi, ikiwemo ushirikishwaji katika zoezi hilo. Kamati ya wadau wa mji huo mpya, ambayo inatambuliwa na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi kwa mujibu wa barua yake ya Juni 28, 2010, imelalamika kuwa zoezi lote lina upungufu mkubwa.
Barua hiyo imeeleza kuwa hali hiyo imeongeza shaka kama mradi huo utatekelezwa kwa manufaa ya wananchi au ni ulaji wa watu wachache tu. Kamati hiyo imeshangazwa na tofauti za kauli zilizotolewa na viongozi wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi kuhusu mradi huo, wakinukuu kauli ya Waziri Prof. Anna Tibaijuka, aliyotoa bungeni akisema:
"Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2011/2012 wizara yangu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, itakamilisha maandalizi ya mpango kamambe baada ya kujadili katika mikutano ya hadhara itakayofanyika kwenye eneo la mpango huo."
Lakini uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, hakuna mikutano iliyofanyika, zaidi ya mkutano mmoja tu uliofanyika eneo la Kibada (Uvumba), na wananchi kusema kuwa hawajaeleweshwa wajue nini hatma yao kama mradi huo utatekelezwa. Kwa mujibu wa habari hizo, wananchi wa Kigamboni wamesema wamewasilisha barua za malalamiko na ufafanuzi 69 serikalini, ikiwemo kwa rais, lakini hawajawahi kujibiwa kwa maandishi zaidi ya kupewa ahadi za kisiasa ambazo hazitaji moja kwa moja athari na mustakabali wa ardhi yao.
Hoja kubwa wanayotumia ni kuwa zoezi hili limetawaliwa na usiri mkubwa, na kuwa wananchi wa eneo husika hawakushirikishwa, jambo ambalo ni kinyume kabisa na sehemu ya 4 ya sheria namba 8 ya mipango miji ya mwaka 2007, kifungu E. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, katika kikao alichokaa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na wabunge wa Dar es Salaam, ilibainika kuwa zoezi la ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni limegubikwa na ushirikishwaji hafifu wa wananchi, viongozi wa serikali na wawakilishi wa wananchi walikuwa hawapati ushirikishwaji sawa sawa, badala yake waziri na watendaji wa wizara wamekuwa hawafuati sheria.
Wamedai kuwa badala yake viongozi hao wanatumia ubabe, nguvu na zoezi kuwa la siri na wananchi hawapewi taarifa za utekelezaji.
Hata hivyo, kauli ya Waziri Tibaijuka, kwamba "wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha itaendelea na juhudi za kutafuta fedha kwa ajili ya kulipa fidia stahiki kwa wananchi" imeongeza hofu, na kwamba inapingana na kauli aliyotoa Rais Kikwete wakati wa uzinduzi wa kivuko kipya cha Mv. Magogoni.
Katika hotuba yake siku hiyo, wananchi wa Kigamboni walisema rais aliuthibitishia umma wa wakazi hao kuwa hakuna mwananchi atakayehamishwa kutoka eneo la mradi kwenda eneo jingine, isipokuwa watapangwa upya na eneo kuboreshwa. Aidha, wananchi wa Kigamboni wamesema hadi sasa hawaelewi huu mradi ni wa serikali au wa wawekezaji kutokana na kauli zinazopingana zilizotolewa na waziri na naibu wake bungeni.
Waziri wa Ardhi aliliambia Bunge Novemba 2011 kuwa; "Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha itaendelea na juhudi za kutafuta fedha kwa ajili ya kulipa fidia stahiki kwa wananchi", lakini kumbukumbu halisi za Bunge (hansard) zinamnukuu naibu wake akisema: "Kwa hiyo natoa wito kwa wananchi wa Kigamboni kwamba wale wote wanaomiliki maeneo katika eneo hilo wajitokeze wakitaka wao wenyewe waalike wawekezaji popote, wanaopatikana waje washirikiane wajenge kile ambacho kimesanifiwa katika eneo la mpango wa mji mpya na serikali itaidhinisha."
Wananchi wa Kigamboni wameitaka serikali kuachana na utekelezaji wa mradi huo kwani wanajua haina pesa za kuwahamisha.
Baadhi ya wananchi hao walihoji kwamba kama serikali inaweza kuwahamisha na kuwaboreshea makazi, kwanini haikuboresha maslahi ya walimu hali iliyosababisha taifa kuyumba kielimu kwa kiasi cha kuleta aibu?
"Hela za Kigamboni zipo, ila za elimu na madaktari hakuna, unasikia mwandishi? Hela za Kigamboni zipo za kujenga mji kwa ajili ya Wazungu, ila za kuboresha daftari la wapiga kura hakuna. "Unajua hapa tutapigwa changa la macho kwenye mradi huu hadi tutajuta. Nasikitika kusikia kuwa viongozi wa CCM wameanza kuwahadaa watu kuwachagulia watu kwenye kamati.
"Natoa tahadhari, zoezi hili sio la kukurupuka, linahitaji elimu, hivyo waheshimu kamati yetu," alisema mzee mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini. Waziri Tibaijuka, akiongea kwa simu toka Ngorongoro alikosema alikuwa anasuluhisha mgogoro wa ardhi alisema: "Hatutaanza upya, mradi wa mji mpya wa Kigamboni unaendelea na mchakato hapo tulipofikia, na nikija Dar es Salaam nitatolea ufafanuzi zaidi wa suala hili."