Madudu mji mpya Kigamboni

Madudu mji mpya Kigamboni

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
668
Reaction score
426
na Josephat Isango

UJENZI wa mji mpya wa Kigamboni huenda ukakwama baada ya wananchi kudai kuwa serikali imekuwa ikikiuka sheria na mambo ya msingi, ikiwemo ushirikishwaji katika zoezi hilo. Kamati ya wadau wa mji huo mpya, ambayo inatambuliwa na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi kwa mujibu wa barua yake ya Juni 28, 2010, imelalamika kuwa zoezi lote lina upungufu mkubwa.

Barua hiyo imeeleza kuwa hali hiyo imeongeza shaka kama mradi huo utatekelezwa kwa manufaa ya wananchi au ni ulaji wa watu wachache tu. Kamati hiyo imeshangazwa na tofauti za kauli zilizotolewa na viongozi wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi kuhusu mradi huo, wakinukuu kauli ya Waziri Prof. Anna Tibaijuka, aliyotoa bungeni akisema:

"Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2011/2012 wizara yangu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, itakamilisha maandalizi ya mpango kamambe baada ya kujadili katika mikutano ya hadhara itakayofanyika kwenye eneo la mpango huo."

Lakini uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, hakuna mikutano iliyofanyika, zaidi ya mkutano mmoja tu uliofanyika eneo la Kibada (Uvumba), na wananchi kusema kuwa hawajaeleweshwa wajue nini hatma yao kama mradi huo utatekelezwa. Kwa mujibu wa habari hizo, wananchi wa Kigamboni wamesema wamewasilisha barua za malalamiko na ufafanuzi 69 serikalini, ikiwemo kwa rais, lakini hawajawahi kujibiwa kwa maandishi zaidi ya kupewa ahadi za kisiasa ambazo hazitaji moja kwa moja athari na mustakabali wa ardhi yao.

Hoja kubwa wanayotumia ni kuwa zoezi hili limetawaliwa na usiri mkubwa, na kuwa wananchi wa eneo husika hawakushirikishwa, jambo ambalo ni kinyume kabisa na sehemu ya 4 ya sheria namba 8 ya mipango miji ya mwaka 2007, kifungu E. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, katika kikao alichokaa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na wabunge wa Dar es Salaam, ilibainika kuwa zoezi la ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni limegubikwa na ushirikishwaji hafifu wa wananchi, viongozi wa serikali na wawakilishi wa wananchi walikuwa hawapati ushirikishwaji sawa sawa, badala yake waziri na watendaji wa wizara wamekuwa hawafuati sheria.

Wamedai kuwa badala yake viongozi hao wanatumia ubabe, nguvu na zoezi kuwa la siri na wananchi hawapewi taarifa za utekelezaji.
Hata hivyo, kauli ya Waziri Tibaijuka, kwamba "wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha itaendelea na juhudi za kutafuta fedha kwa ajili ya kulipa fidia stahiki kwa wananchi" imeongeza hofu, na kwamba inapingana na kauli aliyotoa Rais Kikwete wakati wa uzinduzi wa kivuko kipya cha Mv. Magogoni.

Katika hotuba yake siku hiyo, wananchi wa Kigamboni walisema rais aliuthibitishia umma wa wakazi hao kuwa hakuna mwananchi atakayehamishwa kutoka eneo la mradi kwenda eneo jingine, isipokuwa watapangwa upya na eneo kuboreshwa. Aidha, wananchi wa Kigamboni wamesema hadi sasa hawaelewi huu mradi ni wa serikali au wa wawekezaji kutokana na kauli zinazopingana zilizotolewa na waziri na naibu wake bungeni.

Waziri wa Ardhi aliliambia Bunge Novemba 2011 kuwa; "Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha itaendelea na juhudi za kutafuta fedha kwa ajili ya kulipa fidia stahiki kwa wananchi", lakini kumbukumbu halisi za Bunge (hansard) zinamnukuu naibu wake akisema: "Kwa hiyo natoa wito kwa wananchi wa Kigamboni kwamba wale wote wanaomiliki maeneo katika eneo hilo wajitokeze wakitaka wao wenyewe waalike wawekezaji popote, wanaopatikana waje washirikiane wajenge kile ambacho kimesanifiwa katika eneo la mpango wa mji mpya na serikali itaidhinisha."

Wananchi wa Kigamboni wameitaka serikali kuachana na utekelezaji wa mradi huo kwani wanajua haina pesa za kuwahamisha.
Baadhi ya wananchi hao walihoji kwamba kama serikali inaweza kuwahamisha na kuwaboreshea makazi, kwanini haikuboresha maslahi ya walimu hali iliyosababisha taifa kuyumba kielimu kwa kiasi cha kuleta aibu?

"Hela za Kigamboni zipo, ila za elimu na madaktari hakuna, unasikia mwandishi? Hela za Kigamboni zipo za kujenga mji kwa ajili ya Wazungu, ila za kuboresha daftari la wapiga kura hakuna. "Unajua hapa tutapigwa changa la macho kwenye mradi huu hadi tutajuta. Nasikitika kusikia kuwa viongozi wa CCM wameanza kuwahadaa watu kuwachagulia watu kwenye kamati.

"Natoa tahadhari, zoezi hili sio la kukurupuka, linahitaji elimu, hivyo waheshimu kamati yetu," alisema mzee mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini. Waziri Tibaijuka, akiongea kwa simu toka Ngorongoro alikosema alikuwa anasuluhisha mgogoro wa ardhi alisema: "Hatutaanza upya, mradi wa mji mpya wa Kigamboni unaendelea na mchakato hapo tulipofikia, na nikija Dar es Salaam nitatolea ufafanuzi zaidi wa suala hili."
 
Mradi kama huu unawezekana tu katika nchi ya malimbukeni ambayo raia wake no second class citizens na wageni ndio bora. Nadhani imefika wakati sasa wananchi kupambana na jaws wakoloni weusi kwa njia zote.
 
Nimepata habari kuwa kamati zinaundwa na nyaraka za kikao cha wabunge wa mkoa wa DSM na
waziri mkuu zinasambazwa kwa wananchi,hata mimi nimeziona zikiongelea mpango mzima wa mradi
wa Kigamboni na pia nimesikia kuwa makubaliano tayari kuwa fidia italipwa 35,000 kwa Square meter?
au ni propaganda za kisiasa?
 
Tuombe na tushukuru maana matatizo yanaongezeka kwa kasi na kama wahanga tutakuwa wengi!
Angalieni maana nchi hii inagawanwa na wenye pesa na mnyonge hana chake katika nchi hii
Mkiona wenzenu wa sehemu nyingine anaamuka/wanaamuka kudai haki msiwadharau bali nanyi muamke huko mliko kudai haki yenu pia maana yapo mliyedhulimiwa
Waanaodai haki wakiwa wengi basi mdaiwaji atakuwa makini na hatacheza na haki za watu kawe ila mkiendelea kudharau kuwa kule ni wao ila yetu yataisha kitalaam nawe utaliwa mali yako kitalaam vilevile!
Umoja ni nguvu
 
Nafikiri wangetumia cubic meters, maana wangine wameinvest kwenda juu na chini.
 
Tuombe na tushukuru maana matatizo yanaongezeka kwa kasi na kama wahanga tutakuwa wengi!
Angalieni maana nchi hii inagawanwa na wenye pesa na mnyonge hana chake katika nchi hii
Mkiona wenzenu wa sehemu nyingine anaamuka/wanaamuka kudai haki msiwadharau bali nanyi muamke huko mliko kudai haki yenu pia maana yapo mliyedhulimiwa
Waanaodai haki wakiwa wengi basi mdaiwaji atakuwa makini na hatacheza na haki za watu kawe ila mkiendelea kudharau kuwa kule ni wao ila yetu yataisha kitalaam nawe utaliwa mali yako kitalaam vilevile!
Umoja ni nguvu

Mkuu uko sahihi kabisa watanzania ni wakati wa kuamka na kukataa kufanywa watumwa nchini mwetu,
tuige mfano wa wakazi wa Kinyerezi pamoja na manispaa ya Ilala kuuzia watu form kibao,wananchi
wamekomaa na kuishtaki manispaa mahakamani na manispaa wakapigwa marufuku kutia mguu Kinyerezi"
 
Naibu waziri wa ardhi aliliambia bunge kila mkazi wa kigamboni atakuwa na uhuru wa kuuza au kutafuta mwekezaji wake , waziri mkuu kasema mradi batili umejaa usiri na uongo mwingi uanze upya wananchi wasilikishwe , lkn waziri wa ardhi kakataa kuanza upya ss sijui anafanya kazi kwa maslahi ya nani ? Anabishana na bosi wake
 
kuna eneo wametangaza kulinunua as soon as possible, nafikiri ndipo wanapojenga zile nyumba 80,000 ambazo wahanga ndiyo watahamishiwa hapo.

Bado kuna mtata na usiri mkubwa wa mradi huu.
 
“Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2011/2012 wizara yangu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, itakamilisha maandalizi ya mpango kamambe baada ya kujadili katika mikutano ya hadhara itakayofanyika kwenye eneo la mpango huo.”
Mie ninalo swali dogo kwa Mheshimiwa Waziri: Nakala ya audio-visual CD inayoeleza mpango wa kuiendeleza Kigamboni inasema kutajengwa mashule "for whites only." Je, Mh. Waziri yuko tayari kuwekabayana jambo hili lenye sura ya ukaburu wazi wakati wa "mikutano ya hadhara itakayofanyika kwenye eneo la mpango huo”?
 
Mie ninalo swali dogo kwa Mheshimiwa Waziri: Nakala ya audio-visual CD inayoeleza mpango wa kuiendeleza Kigamboni inasema kutajengwa mashule "for whites only." Je, Mh. Waziri yuko tayari kuwekabayana jambo hili lenye sura ya ukaburu wazi wakati wa "mikutano ya hadhara itakayofanyika kwenye eneo la mpango huo"?

Mh naanaza kunusa harufu ya nchi kuuzwa,kuna shule za "whites only"? kwa nini wasiweke wazi kuwa washamuuzia mmarekani eneo la Kigamboni? wanaleta blabla nyiiiingi,hivi kweli serikali ya Tanzania ina uwezo wa kujenga mji wa
kisasa!!kwa pesa gani waliyonayo ya kulipa watu fidia? Nafikiri kuna mchezo unaendelea sijui kama Ndungulile anajua
au ndo alivyotishwa kuitwa kwenye vikao vya chama akaogopa"?
 
Bado kdg tu uchaguz uje,zile "Fly-over" ziko wapi? Hlo limeshndikana, elimu ndo hiyo imeenda kinyume na malengo yao (ingawa wanajitahd kwa kuwapasisha watoto wa primary wasojua kuandika majina yao na kusoma sentensi rahisi ili wapate jina kwenye tathmini za MDGs),madaktari wakidai maslah wanafukuzwa na kufutiwa ujuzi na waTanzania manakufa,walimu pia...hili la mji mpya litafanyika kwa uhalali?
Kuna msemo m1 nanukuu, "umeshindwa mchana kwenye jua la Mungu, utaweza usiku kwenye taa ya mzungu?"
 
Nimepata habari kuwa kamati zinaundwa na nyaraka za kikao cha wabunge wa mkoa wa DSM na
waziri mkuu zinasambazwa kwa wananchi,hata mimi nimeziona zikiongelea mpango mzima wa mradi
wa Kigamboni na pia nimesikia kuwa makubaliano tayari kuwa fidia italipwa 35,000 kwa Square meter?
au ni propaganda za kisiasa?

35,000 kwa square meter bado ni ndogo ukilinganisha thamani ya ardhi inavyopanda na jinsi kigamboni ilivyoolala kwenye strategic location na pia jinsi ilivyo karibu na mjini. Angalau wangeuza kwa 150,000 kwa kila square meter pale ambapo hapajaendelezwa na 400,000 kwa square meter sehemu yenye jengo au mali nyingine ya aina hiyo. Ikishindikana hiyo basi wananchi wapewe a reasonable amount pamoja na kuwa included kwenye mradi...mfano zikijengwa apartments za ghorofa nane au kumi kwenda juu mwananchi apewe angalau floor mbili ahangaike nazo. Mbona nasikia kuna sehemu hapa dar tena temeke hii hii raia walifidiwa 100,000 kwa square meter? It can be done they should play their part!!
 
Huyu M.k.w.e.r.e ana double standard nyingi sana katika utendaji wake and he always like to take sides lakini hana msimamo,ule ukaribu wake na George W. Bush ndio ulileta kizaazaa hiki.
 
Mimi sielewi hivi Dr F. Ndugulile na wewe unadhani hatuhitaji mradi huu kutoka moyoni kwako kabisa?
 
Last edited by a moderator:
Nimepata habari kuwa kamati zinaundwa na nyaraka za kikao cha wabunge wa mkoa wa DSM na
waziri mkuu zinasambazwa kwa wananchi,hata mimi nimeziona zikiongelea mpango mzima wa mradi
wa Kigamboni na pia nimesikia kuwa makubaliano tayari kuwa fidia italipwa 35,000 kwa Square meter?
au ni propaganda za kisiasa?

Hapa kuna kitu wanaficha, kuna siri kubwa hapa, ninachojiuliza na naomba pia tukumbushane, mwaka jana ktk bunge, Waziri Prf Tibaijuka aliomba nusu ya bajeti yake ya Wizara iende Kigamboni, nakumbuka ilikuwa zaidi ya 60bl, mbona sasa mwaka wa fedha unaelekea ukingoni na hakuna cha maana tunachokiona? Hivi kweli huo mji utajengwa kwa staili hii? Hivi hii serikali inajua kuna watu walikuwa wanategemea nyumba zao kukopa hela kwenye mabenki na taasisi nyingine za fedha leo hawakopesheki na huu ni mwaka wa tano sasa.
Mbunge naona unagonga 'like' tuu hapa, tupe mikakakti yako jinsi ya kupata majibu ya kweli, pata uzoefu wa kwa Mhe Mnyika, anaitisha mkutano anagawa no za simu za Waziri na Naibu wake ili wananchi waulize na wao.
 
Huyu M.k.w.e.r.e ana double standard nyingi sana katika utendaji wake and he always like to take sides lakini hana msimamo,ule ukaribu wake na George W. Bush ndio ulileta kizaazaa hiki.

Halafu watu walishndwa kuona?hata mie kilaza nligundua kuwa pale lazima anasain mkataba wa kuchukua mali mingi sana tena hadharani ,hata wanaIntelijensia hamkustuka?dah!
 
Nimepata habari kuwa kamati zinaundwa na nyaraka za kikao cha wabunge wa mkoa wa DSM na
waziri mkuu zinasambazwa kwa wananchi,hata mimi nimeziona zikiongelea mpango mzima wa mradi
wa Kigamboni na pia nimesikia kuwa makubaliano tayari kuwa fidia italipwa 35,000 kwa Square meter?
au ni propaganda za kisiasa?

35,000 shilingi au dolari, usitake kutuua kwa bp
 
Back
Top Bottom