Madokta hii ni kansa au..........

Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,223
2,902
Nina binamu yangu msichana anasumbuliwa na tatizo la kupasuka ulimi,tangu limeanza mpaka sasa ni miaka mitatu,tatizo lilianza baada ya kutumia vidonge vya maleria vya SP wakati ule vinatumika vikamsababishia reaction ikiwepo kuvimba mpaka mdomo,akaenda hospitali akapata matibau na kupona baada ya mwezi akaona ulimi wake una kama michirizi,akaenda hospitali akapewa dawa ya kusukutua ikaisha, baada ya miezi mitatu ikatokea michirizi mikubwa (mipasuko)ambayo haiumi hata akila vitu vya chachu kama machungwa,ila akiwa kwenye period(hedhi) ndio mipasuko inakuwa mingi mpaka inauma akimaliza inapungua na haiumi, akaenda kituo cha afya wakamwandikia aende amana kule akapimwa akambiwa hana tatizo zaidi ya ukosefu wa vitamin b, wakampa vidonge vya vitamin b coplex 30 akatumia mpaka vikaisha hakuna nafuu, akaenda kwa daktari wa magonjwa ya vinywa pale magomen, akafanyiwa vipimo akaambiwa ana aleji ya vitu vingi tu,na hakutakiwa kula vitu hivyo mpaka baada ya miezi sita,akapewa na vidonge vya vitamin b coplex vingi nakutakiwa kutumia kwa muda wote wa miezi sita, sasa miezi sita imeisha na tatizo liko pale pale, sasa wadau na madaktari wenye ujuzi au kufahamu wa tatizo hili ni kansa au nini,naomba msaada wenu tumsaidie ndugu yangu,nawasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom