Madiwani ‘wamtosa’ Lipumba

Madiwani ‘wamtosa’ Lipumba

Lipumba atafute wafadhili apate hela awalipe ccm hela walizomuhonga, kazi ya kuiua CUF hataiweza tena haswa kule zenji!!!! anajisumbua tu, alipe hela za watu awe huru arudi Rwanda kutafuta kazi.
huko ndiko nyumbani kwao??unamaanisha!!
 
Lipumba anatafuta mtu wa kufa nae, mke wake Sakaya anataka matumizi kwa lazima.
 
Hakuna Mkutano mkuu uliokaa kuridhia kujiuzulu kwa Prof Lipumba. Acheni kutunywesha chai isiyo na sukari
1. Kwahiyo Lipumba alikaa ofisini kusubiri huo mkutano? 2. Ule mkutano aliouvuruga akishirikiana na wahuni pale Blue Pearl ulikuwa kwa ajili gani?
 
1. Kwahiyo Lipumba alikaa ofisini kusubiri huo mkutano? 2. Ule mkutano aliouvuruga akishirikiana na wahuni pale Blue Pearl ulikuwa kwa ajili gani?
Wakati wa mkutano Ubungo Plaza, walijadili nini wakati tayari Pro Pesa ashatengua barua yake ya kujiuzulu few months ago
 
Wakati wa mkutano Ubungo Plaza, walijadili nini wakati tayari Pro Pesa ashatengua barua yake ya kujiuzulu few months ago
Mkuu Granta, bahati mbaya umejibu swali moja, nashukuru kwa majibu mazuri yanayotegemewa kutumiwa na Mutungi, Lipumba. Haiwezekani kuwa CUF hawakuwa wakibanwa kuitisha mkutano wa kuridhia au kutoridhia kwa kuwa Pro pesa alikuwa ameishajiuzulu na kuondoka kabisa ofisini? Rafiki yangu hivi haiwezekani kwamba CUF wangebanwa na unachokiandika iwapo Pro Pesa angekuwa ameandika akiomba kujiuzulu na kusubiri uamuzi wa mkutano mkuu kuridhia au kutoridhia wakati akiwa anaendelea kuwa ofisini? Kumbe CUF wangeridhia au wasingeridhia kitu gani wakati Pro Pesa akiwa Peacock aliitangazia dunia kuwa anabwaga manyanga na anaondoka nchini kwenda Rwanda na kweli akafanya hivyo?
 
yah ,na kama hesabu zao ziko Sawa.wakiichukua kigamboni na temeke kisha wakaja kuiteka kinondoni wamechukua tena jiji lao!!!!!
kuna mambo yanakera chini ya jua

Na ndiyo sababu wamewakataa Madiwani wa viti maalum wa CDM na CUF.
 
Aliandika barua ya nini
Tena akaja live live bila chenga kwenye maluninga huku akidai dhamira yake inamsuta mwe kisa lowasa sasa huwa najiuliza kwa sauti kilichomtoa bado kipo kinachomrudisha ni nini tena aliwaacha wana ukawa katika kipindi kigumu kama ni mgonjwa aliyezidiwa unaweza sema alitoa oxygen iliyokuwa inamsaidia kupumilia sijui alikuwa akidhamiria kitu gani hiyo ni siri yake yaani kwa sisi wakristo Biblia Takatifu imeandikwa mtu mmoja anapowakwaza ni bora akavikwa jiwe kubwa shingoni na kutupwa baharini .
 
Kuna mtu alimfananisha Magufuli na shetani hasw pale aliposema wananchi ni mashetani akasema yeye ndio shetani anavuruga nchi kwa kutaka kuendekeza wizi wa CCM
 
Uamuzi uliotolewa na UKAWA wa kutoshirikiana na Profesa Ibrahim Lipumba hautaathiri umoja huo wa vyama vya upinzani katika uchaguzi wa umeya wa manispaa za Dar es Salaam, baada ya madiwani wa CUF kumsusa.

Profesa Lipumba anatambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwamba ndiye mwenyekiti halali wa CUF, hata pale mkutano mkuu uliporidhia kujiuzulu kwake na kufuatiwa na uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi kumfukuza uanachama.

Mgogoro huo wa CUF uliokigawa chama hicho makundi mawili, uliwasukuma viongozi wa UKAWA wakiongozwa na Freeman Mbowe kutoa tamko la kumtenga Profesa Lipumba kwa madai kwamba analazimisha uenyekiti wa chama.

Licha ya Profesa Lipumba kudai anaungwa mkono na wanachama wengi wa CUF, madiwani wote wa chama hicho katika manispaa za Dar es Salaam wametangaza kuiunga mkono UKAWA kwenye uchaguzi wa meya katika manispaa zote.

Uchaguzi wa Meya unafanyika baada ya kuanzishwa kwa wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni. Ubungo imemegwa kutoka Wilaya ya Kinondoni na Kigamboni imemegwa kutoka Wilaya ya Temeke.

Tayari manispaa za Ubungo na Kinondoni zimegawana kata na kila moja itakuwa na meya na uchaguzi unatarajiwa kufanyika wiki ijayo. Manispaa za Temeke na Kigamboni bado hazijafikia mchakato wa kugawana kata na madiwani.

Madiwani kadhaa wa CUF waliozungumza na mwandishi wa habari hizi, kwa nyakati tofauti walisema hawamuungi mkono Profesa Lipumba anayepinga Ukawa.

Maulid Mtulia ambaye ni Mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF, ameonyesha wasiwasi kwamba kuna njama ya kumpunguza Salima Mwasa ambaye ni Mbunge Viti Maalumu wa CUF katika orodha ya wapigakura wa halmashauri hiyo.

Amesema endapo Mwasa ataondolewa halmashauri ya Kinondoni, idadi ya kura za Ukawa itabaki 17 dhidi ya CCM 17.

Tayari Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilishagawanya rasmi madiwani wake kwenda Manispaa mpya ya Ubungo na wengine kubakia Kinondoni kulingana na jiografia ilivyo. Kinondoni itabaki na kata 20 wakati Ubungo itakuwa na kata 14.

Kwa upande wa CCM, katika Manispaa ya Kinondoni ina madiwani tisa, viti maalumu vitatu na wabunge watano wa kuteuliwa na Rais, wenye sifa ya kupiga kura, ambao ni Profesa Makame Mbarawa, Angela Kairuki, Dk Tulia Ackson, Profesa Joyce Ndalichako na Balozi Augustine Mahiga. Hatua hii inafanya idadi ya kura za CCM kuwa 17 dhidi ya 18 za UKAWA.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM, Kinondoni, Salum Madenge alikataa kutaja idadi ya kura halisi za CCM katika halmashauri hiyo ya Ubungo huku akisema chama hicho kitashinda kwa hesabu na jinsi kilivyojiandaa. Madenge alisema suala la uchaguzi ni hesabu na CCM imejipanga kupata ushindi katika uchaguzi huo.

“Kama wao wana kura hizo 14, basi sisi ni zaidi yao, subiri utaziona siku ya kupiga kura. Unajua uchaguzi ni hesabu kwa hivyo tumeshajipanga wala usijali…, ” alisema Madenge huku akitoa kicheko.

Halmashauri ya Ubungo

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey Polepole alinukuliwa Julai mwaka huu akizitambua Kata 14 za halmashauri hiyo za Makurumla, Mburahati, Manzese, Mabibo, Sinza, Ubungo, Makuburi, Kimara, Mbezi, Msigani, Saranga, Goba, Kibamba na Kwembe.

Hesabu ya kata hizo inaonyesha kuwa CUF ina kura (2), CHADEMA (10) na CCM (2). Kwa tofauti ya idadi hiyo ya madiwani, inaifanya CCM kukosa nafasi yoyote ya ushindi hata bila kutegemea mgogoro wa Lipumba ndani ya CUF.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo alisema uchaguzi huo utafanyika siku yoyote kuanzia wiki hii.

Kuhusu mchanganuo wa idadi ya kura za vyama, Kayombo alitaka kusubiri waraka kutoka mamlaka husika.

“Kata ziko 14 na CCM ina Kata(2), CUF (2) lakini naomba tusubiri waraka utakaokuwa na taarifa zote za uchaguzi, wala usijali tutaweka mbele ya vyombo vya habari, nadhani itakuwa wiki hii,” alisema Kayombo.

Temeke na Kigamboni

Kwa Halmashauri mbili za Temeke na Kigamboni, CCM itakuwa na nafasi ya kuchukua ushindi kwa hesabu ya kura zozote zitakazogawanywa katika pande hizo mbili kutokana na kuwa na idadi kubwa ya madiwani ikilinganishwa na UKAWA.
ni muhimu kufahamu kuwa prof. lipumba m/kiti wa cuf, hagombani na madiwani wa cuf wala mtu yeyote yule ndani ya chama chake (cuf) bali anapambana na mkono haramu ulioingia kwenye chama chake ukitokea cdm!
 
Ha, ha, ha, hata madiwani wa Mtwara wamemsusia akabaki akiwahutubia akina mama pekee.
acha dharau ndugu yetu wewe kwani wakina mama sio watu? au sio wanachama wa cuf? je wewe ulitaka awahutubie akina nani sasa! cuf ya prof.lipumba haitaji mamluki wa cdm ok?
 
acha dharau ndugu yetu wewe kwani wakina mama sio watu? au sio wanachama wa cuf? je wewe ulitaka awahutubie akina nani sasa! cuf ya prof.lipumba haitaji mamluki wa cdm ok?
Ok,
Bali inahitaji Mamluki wa CCM,
Sawa Nimekuelewa
 
Hii movie itaisha lini??..

Kiufupi hakuna mtu timamu anayeweza kumuunga mkono professor uchwara kwa fyoko fyoko anazozifanya.
hv wew ukiambiwa uletu angalau ndugu zako 5 wanao fananafanana tu na prof. uchwara utaweza, acha kuaminishwa na kukaririshwa na masilahi ya watu, wanao endekeza siasa chakavu zafaida zao!
 
Back
Top Bottom