SAVERA
Senior Member
- Jun 25, 2013
- 114
- 42
Madiwani wa Kata zilizo ktk mpango wa ujenzi wa mji mpya yaani KDA wamekubali kupofushwa macho na Wizara na waziri Mama Tibaijuka kwa kukubali kusafirishwa na Wizara eti kwa lengo la kwenda kujifunza juu miji mingine inavyojengwa.
Mwaliko huo pia ulikuwa ni pamoja na Mbunge wa Kigamboni Dr.Ndungulile,lakini hongera kwa Mbunge huyu alikataa ofa hiyo.
Kwa nini tunasema ni usaliti,kwenye kikao cho Full Council Temeke kikiongozwa na Meya ilionekana kuwa ofa hiyo si halali kwani Council haina taarifa ila alitafutwa kila diwani na kupewa ofa hiyo kama yeye.Na makubaliano yakawa ni kwamba wasiende mpaka wizara,ilete taarifa kwenye council na kueleza faida na hasara za safari hiyo,na lengo lake.
Lakini cha kushangaza madiwani hao wakakubaliana wao pembeni na kuamua kukubali ofa hiyo na kusafiri zao kwenda China na kwingineko eti kujifunza miji inavyojengwa.
La kujiuliza ni je kweli wakirudi watakuwa na ujasiri wa kusimama pamoja na wananchi na kukataa matakwa ya wizara ambayo imewafanya wengi wao kupanda ndege na kwenda nchi ambako hawakutegemea kufika?Je Meya atakuwa na ujasiri huo? baada ya kuwasiliti hata wenzao kwenye Full council? Kazi kwenu Wana Kigamboni'