Madiwani wa chadema wamshutumu nyororo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani wa chadema wamshutumu nyororo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kichomiz, Jul 2, 2011.

 1. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,026
  Likes Received: 2,675
  Trophy Points: 280
  Madiwani wa CDM katika halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Shinyanga
  imemshutumu vikali Mwenyekiti wa halimashauri hiyo,bw Mathias Nyororo kutozingatia kanuni za kuongoza baraza la madiwani

  Bw. Yusuph Fungameza ambaye ni Mwanasheria wa CDM wilani humo alitoa shutuma hizo Jun 8 katika mkutano hadhara uliofanyika katika kata ya Igulwa mjini Ushirombo ambao ulilenga kuwaeleza wananchi sababu zilizowafanya madiwani wa CDM kususia kikao cha baraza Mei20.

  Bw. Fungameza ambaye ni diwani wa kata ya Uyovu "alisema madiwani wa CCM wamezoea kuburuzwa,lakini sisi tutazingatia kiapo chetu kwa kufuata kanuni na sheria zinazoongoza ya wilaya na Taifa la Tanzania.

  Mei kumi mwaka huu Bw. Nyororo alivunja kanuni kwa kufungua kikao saa 9:30 alasiri badala ya saa 3:00 asubuhi kama kanuni ya saba inavyosema na pia madiwani walikabidhiwa makabrasha ya kikao muda mfupi kabla ya kikao,badala ya kukabidhiwa makabrasha hayo siku 7 kabla ya kikao kwa mujibu wa kanuni".

  Pia madiwani wa CDM kwa kushirikiana na mbunge wa Bukombe Prf Kulikoyela Kahigi wamefanikiwa kuing'oa kampuni ya TANCAN kutoka Marekani iliyokuwa ikichimba dhahabu huku ikidai inafanya utafiti wa madini hayo
  baada ya kubaini kuwa kampuni hiyo ya kigeni imekuwa ikifanya shughuli zake wilayani humo,kwa muda wa miaka 8 bila kuwa na nyaraka zozote wala mkataba toka serikalini waliipa siku 45 kampuni hiyo iwe imeondoa mitambo yake na kurejea Rwamgasa wilayani Geita ilikotokea.

  Nae bw. Soud Ntanyangara Diwani wa kata ya Igulwa ambaye pia ni katibu wa madiwani wa CDM wilayani Bukombe alilaani kitendo cha wenye viti wa mitaa kuchangisha TSH 5000 kwa ajili ya vijana waliokuwa wanasajiliwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi na kusema kuwa suala hilo limezua utata katika jamii.
  CHANZO gazeti la MZAWA.
   
Loading...