Madiwani: Tunataka mikopo kama wabunge

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
22,124
49,384
Madiwani: Tunataka mikopo kama wabunge

  • Wasema wao ndio walio karibu zaidi na wananchi
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni juzi walifanya kikao kilichojadili hatua ya serikali kuwasimamia wabunge kupata mikopo ya sh milioni 200 huku wao wakishindwa kukopeshwa hata baiskeli.

Kikao hicho kiliongozwa na Katibu wa Madiwani Mkoa wa Dar es Salaam, Julian Bujugo, ambapo madiwani hao walitoa malalamiko yao, ikiwa ni pamoja na mishahara yao ambayo ni sh laki moja na ishirini kwa mwezi.

Chanzo kikuu kiliiambia Tanzania Daima kuwa wameshangazwa na hatua ya wao kudharaulika huku wakiwa ndio watendaji wakuu kwa wananchi katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.

Madiwani walimtaka Bujugo kuhakikisha anafuatilia suala la masilahi yao kwa kuhakikisha anakutana na viongozi wa serikali ili kupata muafaka juu ya malipo wanayopewa.

Walisema wanasikitika na jinsi hali ngumu inavyowakabili wananchi mbalimbali huku wabunge wakikopeshwa sh milioni 200 na benki moja (jina linahifadhiwa).
Ilielezwa kuwa fedha ya kulipia mikopo ya wabunge hao itatokana na kupangiana semina pamoja na safari za nje ya nchi, bila kutolewa fedha zozote kutoka katika mishahara yao.

"Huwezi kuamini, leo baadhi yetu tunalalamikia kupanda kwa sukari na gharama za maisha lakini ukweli ulio wazi wabunge wanaishi kama wafalme katika nchi hii...inabidi na sisi tusimame imara tuhakikishe tunaongezewa posho na kupewa mikopo," kilieleza chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, madiwani hao walihitaji kuona mabadiliko yanayokaribiana na wabunge, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha serikali inasimamia haki na kuwatafutia mikopo madiwani wote.

Kiliongeza kuwa katika miaka yao ya uongozi madiwani hawajawahi kukopeshwa mkopo hata wa sh milioni 20 wala milioni 10, wakati wabunge wamekabidhiwa hundi za magari za sh milioni 90 hivi karibuni.

"Hapana, ni kudanganyana, ni nani kati yetu anayesimamia masilahi ya wananchi kati yetu na wabunge ...tena hawa bila nguvu yetu hakuna rais wala mbunge anayeweza kupatikana," ilidaiwa.

Kikao kama hicho kinatarajiwa pia kufanyika katika wilaya za Temeke na Ilala na kukutanisha madiwani ili kujadili masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na masilahi yao.

Hivi karibuni wabunge walipewa mkopo wa hundi za sh milioni 90 kwa ajili ya kununua magari pamoja na kukopeshwa sh milioni 200 kama mkopo wa kawaida.

SOURCE: Tanzania Daima, 18th March 2011 - Madiwani: Tunataka mikopo kama wabunge
 
Hii habari inaonesha jinsi nchi ilivyo katika hali mbaya. Kila mwenye/wenye nafasi wanajiangalia wao kwanza. Sikutegemea wawakilishi wa wananchi kujadili mambo kwa ubinafsi/umimi wa hali ya juu kama huu. Hebu angalia hii argument yao:

"Huwezi kuamini, leo baadhi yetu tunalalamikia kupanda kwa sukari na gharama za maisha lakini ukweli ulio wazi wabunge wanaishi kama wafalme katika nchi hii...inabidi na sisi tusimame imara tuhakikishe tunaongezewa posho na kupewa mikopo"

Kumbe kinachowaumiza hapa ni WABUNGE kuishi kama wafalme ilhali WAO (MADIWANI) wakiwa hawana kitu na sio wananchi wa hali ya chini. Hii inamaanisha wakipatiwa hicho wanachokihitaji, kelele zote zimekwisha; wananchi mtajua wenyewe. Kuna haja ya KATIBA MPYA ku-address hivi vitu. Suala la mishahara na viwango vyake kwa watumishi mbalimbali, hususan wa wanolipwa kwa kodi za wananchi, ni lazime liwe la kikatiba na sio suala la kuunda tume au kundi fulani kama wabunge kujilipa kifisadi wanavyotaka wao.

Ni lazima Katiba iseme wazi, kwa mfano, kima cha chini cha msahara na posho nyingine haziruhisiwi kutofautiana kwa (zaidi ya) kiwango fulani na kima cha juu kabisa. Na pia kama ilivyo kwa viongozi/rais wastaafu ambao nadhani wanalipwa 80% ya mshahara wa rais aliyeko madarakani wakati huo, kanuni hii, au kadiri Katiba Mpya itakavyoagiza, pia i-apply kwa watumishi wengine na sio kwa wachache kana kwamba wao ni miungu.
 
Dah! Mi nikajua wanalalama wabunge kulipwa vizuri ilhali nchi ni maskini, kumbe na wao wanataka waonje mafanikio? Kwisha habari yetu!
 
Hawa jamaa badala ya kujadili namna ya kutatua matatizo yanayotukabili wao wanajijadili wao!!
 
Inauma sana kuona Diwani ambaye muda wote yupo pamoja na wananchi ananyanyaswa namna hii.

Serikali lazima itupie macho hapo.
 
Back
Top Bottom