Madiwani Rombo walilia posho

don-oba

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
1,387
677
Katika hali ya kustaajabisha, madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo wamesusia vikao mbalimbali wakilalamika kwamba posho ya mahudhurio ya vikao (Sitting allowance) imepunguzwa.

Madiwani hao wasema hawatahudhuria vikao mpaka hapo posho itakapopandishwa.

Ikumbukwe kwamba stahili hizo za posho wanalipwa kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali za serikali. Mkurugenzi Mtendaji wa H/W Rombo amesema hawezi kuwaongezea posho madiwani kinyume na taratibu, kwani wao wapo kuwatumikia wananchi na si kulilia posho.

H/W Rombo baraza lake linaongozwa na CHADEMA kwakuwa na idadi kubwa ya madiwani.


=======================
MADIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, wamesusa posho za vikao vya kamati vinavyoendelea kwa madai kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Magreth John amezipunguza bila ridhaa yao.

Madiwani hao kutoka kamati za Elimu, Afya, Maji na Uchumi, Ujenzi na Mazingira wamegoma kupokea posho ya Sh 40,000 kwa kila kikao wakitaka kulipwa posho ya awali ya Sh 82,000.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, John amekiri kususiwa posho hizo na kuongeza kuwa hatua hiyo inafuatia kufuatwa kwa waraka wa serikali wa mwaka 2007 na 2012 unaoelekeza viwango stahili vya posho kwa madiwani.

Mkurugenzi amesema waraka huo wenye Kumb Na CHB/443/01 wa Novemba 26, 2007 umetaja viwango vya malipo ya madiwani kwa mwezi, posho ya madaraka kwa wenyeviti wa kamati, wenyeviti wa halmashauri za wilaya, manispaa na majiji nchini na kwamba yeye ni msimamizi na hafanyi kwa matakwa yake.

Amesema, kutumika kwa waraka huo kutaisaidia halmashauri kuokoa zaidi ya Sh milioni 60 ambazo zitatumika katika miradi ya maendeleo kama afya, elimu na maji.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Evarist Silayo amesisitiza msimamo wake kwamba posho ya kikao ni Sh 82,000 kama ilivyo kwa halmashauri nyingine mkoani Kilimanjaro ambazo zipo juu ikilinganishwa na Rombo.

“Posho hii tumeikuta ilipitishwa na madiwani wa awamu zilizotangulia lakini pamoja na hilo tulipoingia sisi tulijaribu kuondoa vyakula wakati wa vikao vya kamati... hakuna diwani wa Rombo analipwa posho ya usafiri, madaraka isipokuwa wenyeviti wa kamati na mwenyekiti wa halmashauri,” amesema.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Rombo linaundwa na madiwani 38, wakiwamo 28 wa kata, huku kati yao 37 ni kutoka Chadema na mmoja kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM
).

Chanzo: Habari Leo
 
kwani wanalipwa shilingi ngapi na wanadai kulipwa ngapi?
CCM wana figisu za Kipuuzi sana, mnapunguza posho za madiwani kwa sababu ni wa upinzani kisha wakizidai mnadi ni walafi..kama nyie sio walafi kwa nini hampunguzi za wabunge ili tupate fedha za maendeleo? na kwa nini mnang'ang'ania kupunguza kwenye halmashauri zinazoongozwa na wapinzani za CCM mmekaa kimya? wapuui sana
 
Ndio maana sisi wenye akili tunasema anayeshabikia na kuamini chadema itamletea maisha bora akapimwe akili
Ni kweli ukapimwe akili ikiwa mbunge analipwa posho na analipwa mshahara sembuse diwani wasiokuwa na mshahara. Kwenye vikao vya ccm vya kujadili ujinga mnalipana posho.
 
Wangesaidia serikali ipate pesa nyinga ili wao na wananchi wawe na pesa nyingi. Swali lingine tafadhali.
 
Chadema ni wasanii na waganga njaa tu.chama kinachotetea wanyonge hakiwezi kulilia posho,wajiuzulu tu,uitishwe uchaguzi mdogo
 
MADIWANI WANGELIPWA 1/4 YA MISHAHARA NA MARUPURUPU YOTE YA MBUNGE KWA MWEZI. PODHO YAO IWE ROBO YA ILE YA MBUNGE KWA SIKU. WOTE NI WAWAKILISHI WA WANANZENGO
 
Wapeni.mnawaonea tu mbona wabunge wanalipwa posho zaidi ya milioni 9 kwa mwezi na mshahara juu hawa 820000 inakuwa nongwa?
 
Mwenyekiti wa Halmashauri huyo bwana Evarist Silayo nimesoma naye udsm huyu jamaa kwenye harakati ni moto mwingine kabisa. Hawa watu wa Rombo wamempata mtu ambaye level zake sio za hapa.
 
Tuache siasa kwenye mambo ya msingi. Ni haki kwa kila mtu kupata stahiki yake ili imwezeshe kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na kwa wakati. Kama kiwango hicho kilifanyiwa evaluation na kikapitishwa ni halali yao, kazi za hawa watu ni kubwa, kata nyingine jografia yake ni ngumu. Tuwape stahiki yao waweze kufanya majukumu yao ipasavyo, tusiwanyanyase watu kwa kuwa tu ni chama fulani au dini au Kabila fulani.
 
Back
Top Bottom