Madiwani CUF walaani agizo la kumweka ndani Halima Mdee

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
pic+madiwani.jpg

Diwani wa kiwalani Mussa Kafana (Katikati) akizngumza na wanahabari katika ofisi za wabunge wa CUF zilizopo Magomeni Jijini Dar es salaam

Kwa ufupi
Madiwani hao wamedai kwamba alichofanyiwa Halima Mdee si kitendo cha haki kwa sababu kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake.

By Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz
Madiwani 19 wa Chama cha CUF Mkoa wa Dar es Salaam, wamelaani hatua ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ya kuagiza polisi kumkamata na kumweka ndani kwa saa 48 mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa madai ya kutoa kauli za kashfa kwa Rais na uchochezi kwa Taifa.

Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) alikamatwa jana (Julai 4) na polisi na kuwekwa ndani kwa amri hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake leo (Julai 5), diwani wa Kiwalani, Mussa Kafana amewaambia waandishi wa habari kuwa kwa niaba ya chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam wamesikitishwa na hatua hiyo.

"Tumeamua kulisema kwa uchache kwa sababu tumepata fursa. Tunalisema kwa sababu linatugusa, Mdee (Halima) ni sehemu ya madiwani na mjumbe wa Baraza la Jiji la Dar es Salaam," amesema.

Kafana ambaye pia ni naibu meya wa Jiji la Dar es Salaam, amesema alichofanyiwa Mdee ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwa sababu kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake.

"Sasa hivi imekuwa tofauti ukisema jambo linaloenda kinyume cha mtu fulani unakamatwa unawekwa ndani. Taifa linakoenda siko, ndiyo maana tunalaani na hatukubaliani na kitendo hiki," amesema Kafana.

======

TAMKO LA MADIWANI WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) WA MKOA WA DAR ES SALAAM JUU YA KUUNGA MKONO HOTUBA NA MSIMAMO WA CHAMA ULIOTOLEWA NA KATIBU MKUU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD TAREHE 28 JUNE 2017 KATIKA HOTEL YA PEACOCK:

Tarehe 5 JULAI, 2017

NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
WAHESHIMIWA VIONGOZI WA CUF,
WAHESHIMIWA WANACHAMA WA CUF,
WAHESHIMIWA WANANCHI, MABIBI NA MABWANA,

NAOMBA NIANZE KWA KUWASALIMU KWA SALAMU ZA CHAMA CHETU HAKI SAWA KWA WOTE,

1. Awali ya yote, tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima na kutuwezesha kukutana hapa asubuhi hii, kwa lengo la kutoa Tamko na msimamo wetu Rasmi juu ya sintofahamu inayoendelea ndani ya Chama chetu, na kuunga mkono Hotuba na msimamo wa Chama uliotolewa na Katibu Mkuu wetu, Maalim Seif Sharif Hamad. Tukiwa ni Madiwani wa CUF, kutoka Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam na kupitia kwenu ujumbe wetu uweze kuwafikia wana-CUF wenzetu, Wapenda Mabadiliko wote nchini, na Watanzania kwa Ujumla.
2. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru nyinyi Waandishi wa Habari kwa kuhudhuria kwenu na mara zote kutukimbilia kila tunapokualikeni mbali na Changamoto mnazokabiliana nazo juu ya uhuru wa Habari na aina ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano jinsi unavyoikandamiza demokrasia nchini na kutopenda kukosolewa.

3. Tarehe 28 June, 2017 Katibu Mkuu wetu alifanya mkutano na Wahariri na Waandishi wa Habari pale Peacock Hotel na kuelezea kwa kina kadhia ya muendelezo wa hujuma zinazofanywa na Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi, Afisa Mtendaji Mkuu, Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA- Emmy K Hudson na Profesa Ibrahim Lipumba dhidi ya CUF na viongozi wake.

4. Mtakumbuka vyema kuwa Chama chetu kimeshiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Bila ya kuwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wetu Profesa Ibrahim H. Lipumba kwa utashi wake mwenyewe mbali na kumnasihi sana kusitisha mpango wake huo, kila mmoja wetu kwa wakati wake alishiriki kwa namna moja au nyingine kuhakikisha Profesa Lipumba hajiuzulu nafasi ya uenyekiti wa Chama Taifa. Sote tuliamini kuwa kujiuzulu kwake kungeweza kuleta athari kwa sisi wagombea watarajiwa wa wakati huo na kuathiri ushirikiano wa vyama vyetu katika UKAWA. Profesa Lipumba alipuuza kilio chetu sote wana-CUF na kushikilia msimamo wake na mara baada ya kutoa Taarifa hiyo rasmi ya Kung’atuka/Kujiuzulu pale Peacock Hotel Tarehe 6 Agosti, 2016 alielekea Kigali, nchini Rwanda kwa shughuli aliyoiita ya utafiti wa kiuchumi wenye lengo la kuja kuisaidia Serikali ijayo ya awamu ya Tano.

5. Sisi Madiwani 19 tuliopo mbele yenu hapa leo, Pia Tumepambana katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka 2015 bila ya kuwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Mheshimiwa Juma Duni Haji ambaye kwa mujibu wa makubaliano ya UKAWA alilazimika kujiunga CHADEMA ili apate nafasi ya kuwa Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumeshiriki uchaguzi tukiwa kama Mayatima na Wakiwa. Tumeweza kushinda nafasi tulizozipata za kuwakilisha wananchi katika kata zetu katika mazingira magumu bila ya uwepo na ushiriki wa Profesa Lipumba ambaye mbali na kudai kuwa atabaki kuwa mwanachama wa kawaida na kuahidi kushiriki kampeni za majimbo hakuweza kufanya hivyo hata katika Jimbo au Kata moja na si pekee kwa Dar es Salaam bali hakushiriki kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015 katika maeneo yote nchini. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu ametusimamia na kuvuka salama na CUF kupata mafaniki makubwa pande zote mbili za Muungano kama tunavyofahamu. Mgombea wetu wa Urais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameshinda nafasi hiyo. Tumefanikiwa kupata Wabunge wengi wa majimbo, Madiwani na kupata kura za kutosha kwa Mgombea wetu wa Urais tuliyemuunga mkono kupitia UKAWA Mheshimiwa Edward Lowassa.

6. Sote tunafahamu kuwa unaoitwa Mgogoro wa uongozi ndani ya Taasisi yetu ya CUF umepandikizwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi tarehe 23 Septemba, 2016 baada ya kumuandikia barua Katibu Mkuu wa CUF ya kumtambua na kututaka wana-CUF tumrejeshe Profesa Lipumba katika nafasi ya Uenyekiti wa Chama chetu kwa madai kuwa Profesa Lipumba alitengua barua yake ya Kujiuzulu na kwamba Haikupaswa kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Taifa kuijaza nafasi hiyo kwa Baraza Kuu la uongozi Taifa kuitisha Mkutano huo Tarehe 21 Agosti, 2016. Si Jaji Mutungi wala profesa Lipumba aliyeweza mpaka leo hii kuwaeleza wana-CUF na Watanzania kwa ujumla ni Ibara ipi ya Katiba ya CUF inayoruhusu KIONGOZI AKIJIUZULU ANAYO HAKI YA KUTENGUA KUJIUZULU KWAKE KWA KUMUANDIKIA BARUA KATIBU WA MAMLAKA ILIYOMCHAGUA? Sisi madiwani tunatambua na Watanzania wanajua kuwa Kujiuzulu kwa Profesa Lipumba kulikamilika kwa Wajumbe 700 wa Mkutano Mkuu Taifa kupokea na kujadiliana juu ya ajenda hiyo ya kujiuzulu kwake na Wajumbe 476 Walipiga kura za kukubali Profesa Lipumba kuachia nafasi hiyo.

7. Tangu wakati huo Madiwani wa Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wastahiki Manaibu Meya Mheshimiwa Musa Kafana (Mstahiki Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam), Mheshimiwa Ramadhani Kwangaya (Mstahiki Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo) na Mheshimiwa Omary Kumbilamoto (Mstahiki Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala) tukiwa ni viongozi wa Chama kiserikali, tumekuwa kitu kimoja na msimamo wa kuyaangalia maslahi mapana ya ustawi wa Taasisi yetu ya CUF dhidi ya maadui wa ndani na nje ya Chama chetu. Utafiti tulioufanya na matukio tuliyoyashuhudia ya vitendo na mwenendo wa Profesa Lipumba ambaye ni kiongozi wetu tuliyekuwa tunampenda na kumuheshimu sana, imejidhihirisha pasina shaka kuwa CUF chini ya Profesa Lipumba haipo katika mikono salama na uhuru wake kamili wa kupambana na kusimamia mabadiliko makubwa ya kidemokrasia, kisiasa na Kiuchumi nchini. CUF chini ya Profesa Lipumba imekuwa ni sehemu na au tawi la mshindani wetu mkuu wa kisiasa Chama Cha Mapinduzi-CCM dhidi ya upinzani wa kweli wa kisiasa, suala hili haliitaji tochi. Hata wale Wabunge wawili wanaomuunga mkono Profesa Lipumba wamekuwa bega kwa bega na Wabunge wa CCM bungeni dhidi ya Wabunge wa Upinzani.

8. Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad katika Mkutano wake na Wahariri na Waandishi wa Habari pale Peacock Hotel, uliofanyika Tarehe 28 June, 2017 alielezea kwa kina njama na hujuma zilizofanywa na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini kughushi nyaraka na kuziwasilisha RITA ili kumsaidia Mshirika wake Profesa Lipumba apewe usajili wa wajumbe FEKI wa Bodi ya Wadhamini wa CUF ambao ndio moyo wa Chama, kwa lengo la kutaka kujinusuru na kesi ya wizi wa fedha za ruzuku ya Chama kiasi cha Shilingi Milioni 369, lakini pia lengo ni kujihalalishia kufanyika kwa dhuluma nyingine ya uchotaji na kugawana fedha za ruzuku ya Chama kiasi cha shilingi milioni 900 zilizozuiliwa kutolewa na Mahakama Kuu kufuatia kesi iliyofunguliwa na CUF ikiwa hesabu hizo mpaka kufikia June 30, 2017.

MAAZIMIO NA MSIMAMO WA MADIWANI WA MANISPAA ZA MKOA WA DAR ES SALAAM:

9. Sisi Madiwani wote 19 wa CUF katika Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam tunaunga mkono hotuba na Msimamo wa Chama uliotolewa na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad, Tarehe 28 June, 2017 Peacock Hotel, Dar es Salaam kwa asilimia mia moja.

10. Tunaungana na viongozi wa Chama chetu kuipinga RITA na maamuzi yake mbele ya Mahakama Kuu kwa kufungua kesi dhidi yake kwa mujibu wa kifungu cha 26 kwa kukiuka taratibu za Sheria ya Wadhamini (The Trustees' Incorporation Act Cap. 318) kwa kutojiridhisha juu ya uhalali wa majina ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CUF yaliyofikishwa kwake na iwapo yamefanywa na kikao halali cha Chama chenye mamlaka hayo kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

11. Tunaungana na pendekezo la Chama la kuwasilisha maombi mbele ya Mahakama Kuu kuitaka isimamishe kesi nyengine zote zilizofunguliwa na Chama kuhusiana na kadhia hii hadi hapo shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya RITA litakapoamuliwa.

12. Tunapinga kwa nguvu zote njama na mipango ya Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi kwa kushindwa kuheshimu hadhi na nafasi yake mbele ya jamii na kujiingiza katika vitendo vya hovyo vyenye muelekeo wa kutaka kuiharibia mustakbali mwema Taasisi yetu ya CUF na kuwaathiri wadau mbalimbali walioshiriki kuiasisi na kuijenga kwa takribani miongo miwili na nusu sasa, sisi kama Madiwani tukiwa ni sehemu ya waathirika wa maamuzi hayo.

13. Tunapinga juhudi zinazofanywa na Profesa Lipumba na wafuasi wake wote ambao wamekuwa na vitendo na mwenendo usiofaa wa kuharibu mali za Chama, kuiba fedha za ruzuku, kusababisha uvunjifu wa amani, kuharibu taswira ya Chama mbele ya Jamii, na kufanya majaribio ya utekaji na kushambulia wanachama na viongozi wa Chama. Aidha tunapinga njama na hila za kuundwa Baraza Kuu FEKI na vyombo vingine vya maamuzi kinyume na Katiba ya CUF na nje ya mamlaka waliyonayo Kikatiba. Madiwani tunatambua uwepo wa Kamati ya Utendaji ya Taifa moja inayoongozwa na Katibu Mkuu, na Baraza Kuu la Uongozi Moja ambalo wajumbe wake wamepatikana kupitia Mkutano Mkuu wa Taifa wa Uchaguzi uliofanyika June, 2014 Blue Pearl Hotel, Dar es Salaam. Madiwani wote tunaunga mkono na kuheshimu hatua zilizochukuliwa na Baraza Kuu hili Halali la CUF kuwasimamisha na Kuwavua uanachama Wanachama wote ambao wameshiriki kukiuka Kanuni na Maadili ya Chama chetu kwa Mujibu wa Katiba.

14. Tunawapongeza viongozi wetu wote wa Kitaifa wakiwemo Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Taifa, Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi, Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na Wabunge wetu wote ambao wamekuwa mstari wa mbele kukisimamia Chama katika kipindi hiki cha mpito wa Changamoto zinazotukabili. Pongezi za kipekee zimuendee Jemedari wetu wa mapambano haya Katibu Mkuu wa Chama chetu Maalim Seif Sharif Hamad na wasaidizi/Manaibu Katibu Mkuu wake Mheshimiwa Nassor Ahmad Mazrui na Mheshimiwa Joran Lwehabura Bashange kwa kazi nzuri ya kuongoza mapambano ya kudai haki sawa kwa wote dhidi ya hila na njama ovu za maadui wa Chama chetu waliopo ndani ya Chama na nje ya Chama.

15. Tunatoa wito kwa Wanachama wa CUF, viongozi wa CUF Tanzania Bara na Visiwani-Zanzibar na Watanzania nchini kote kuendelea kuwa na subra katika kipindi hiki ambacho viongozi wetu wa Kitaifa wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali za Kisheria na Kisiasa ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala hili lililopandikizwa na watu wasio na nia njema na CUF. Ni matumaini yetu ya hakika kuwa kwa Uwezo na msaada wa Mwenyezi Mungu tutazishinda hila na njama zote za maadui wetu na CUF itaendelea kuimarika zaidi na zaidi kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

16. Ni imani yetu kuwa CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI. CUF ina wanachama wapatao milioni 2.5, Wabunge 42, Madiwani 320 nchi nzima, wenyeviti/wajumbe wa vijiji na vitongoji zaidi ya 2250 nchini, wapenzi zaidi ya milioni 1.5 nchini kote, kutokana na hali hii na kwa madhumuni ya kulinda misingi ya Utawala bora na Utawala wa Sheria, kwamba Mahakama Kuu utayapa umuhimu wa kipekee kuyashughulikia Mashauri yote yaliyowasilishwa mbele yake na kwa uzito unaostahiki, kuzingatia Haki, ili kuiepusha nchi yetu na mgogoro usio na sababu zaidi ya malengo ya muda mfupi ya baadhi ya watu wanaodhani kwamba kwa kuihujumu CUF watafanikiwa kuzima matumaini na matarajio ya Watanzania wengi wapenda Mageuzi na Mabadiliko ya Kisiasa, Kiuchumi na Kidemokrasia nchini. Hakuna diwani mwenye akili timamu, anayejitambua, mpenda Haki na mwenye kukitakia mema Chama chetu cha CUF anayeweza kuunga mkono na kuwa upande wa DHULMA NA USALITI.
MADIWANI WA MANISPAA ZA DAR ES SALAAM KAMWE HATUTAKUBALI KUYUMBISHWA.

Tunawashukuru sana kwa kutusikiliza.

HAKI SAWA KWA WOTE

Tamko hili limetolewa leo Tarehe 5 Julai, 2017 na madiwani wa CUF Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi ya wa Wabunge wa CUF-Magomeni.

Mussa Kafana
Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
KWA NIABA YA MADIWANI WOTE
Mawasiliano:0713 068 592
 
Mimi nilifikiri watasema "kitendo cha DC kuamuru Halima awekwe ndani, ni kinyume cha Sheria Namba ...... ya Mwaka ......"
Kumbe ni zogo tu.
 
Hivi wapinzani mbona mnazidi kuwa laini...watawala washabadilika nyinyi bado mnaleta upinzani wa chips mayai. Badilisheni mbinu.
 
Nimesikiliza hii clip nimeshangaa kwa nn Halima kakamatwa...............
Hapa ndo nimeona mgufool ni rais mjinga sana kwani ilitakiwa amshukuru huyu mwana mama kwa kumfungua bichwa lake gumu
HUYU DADA ANAPASWA KUOMBEWA SANA KWANI KAONGEA MAMBO YA MSINGI AMBAYO HAKUNA MWANAccm HATA MMOJA ANAWEZA KUWATETEA WATZ
 
Mwaka huu wasukuma mtaaibika sana tu wadogo zangu, ni aibu kubwa kwa mwanaume wa kisukuma kupigana ama kurumbana na mwanamke hadharani. lakini sio kwa hao tu hata makabila mengine ya watz yaliyo mengi ni hali kadharika, heti leo wanaume wazima mnajitokeza hadharani kushabikia ugonvi wa WANAUME na MWANAMKE?
 
Mimi nilifikiri watasema "kitendo cha DC kuamuru Halima awekwe ndani, ni kinyume cha Sheria Namba ...... ya Mwaka ......"
Kumbe ni zogo tu.
Sasa na wewe twambie kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 18 inatoa Uhuru wa kutoa maoni yako, sasa ni kwanini huyo DC anaamua kuvunja Katiba ya nchi yetu na kuona maoni ya kumkosoa Rais wa nchi iwe kama uhaini?

Kwani yeye DC wa Kinondoni hajui kuwa cheo ni dhamana, na huyo Rais wetu anapaswa kupokea maoni yetu sisi wananchi tuliompigia kura na kumpa dhamana ya kuliongoza Taifa hili?
 
pic+madiwani.jpg

Diwani wa kiwalani Mussa Kafana (Katikati) akizngumza na wanahabari katika ofisi za wabunge wa CUF zilizopo Magomeni Jijini Dar es salaam

Kwa ufupi
Madiwani hao wamedai kwamba alichofanyiwa Halima Mdee si kitendo cha haki kwa sababu kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake.

By Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz
Madiwani 19 wa Chama cha CUF Mkoa wa Dar es Salaam, wamelaani hatua ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ya kuagiza polisi kumkamata na kumweka ndani kwa saa 48 mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa madai ya kutoa kauli za kashfa kwa Rais na uchochezi kwa Taifa.

Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) alikamatwa jana (Julai 4) na polisi na kuwekwa ndani kwa amri hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake leo (Julai 5), diwani wa Kiwalani, Mussa Kafana amewaambia waandishi wa habari kuwa kwa niaba ya chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam wamesikitishwa na hatua hiyo.

"Tumeamua kulisema kwa uchache kwa sababu tumepata fursa. Tunalisema kwa sababu linatugusa, Mdee (Halima) ni sehemu ya madiwani na mjumbe wa Baraza la Jiji la Dar es Salaam," amesema.

Kafana ambaye pia ni naibu meya wa Jiji la Dar es Salaam, amesema alichofanyiwa Mdee ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwa sababu kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake.

"Sasa hivi imekuwa tofauti ukisema jambo linaloenda kinyume cha mtu fulani unakamatwa unawekwa ndani. Taifa linakoenda siko, ndiyo maana tunalaani na hatukubaliani na kitendo hiki," amesema Kafana.

Chanzo: Mwananchi
Mungu ibariki cuf .
 
Usikute bwana mdogo Hapi aliagizwa na boss wake kufanya alichofanya ili kulinda tumbo lake. Haingii akilini kabisa. Nondo za Mdee zitakuwa zilimchoma sana. Mzee wa "mfumo dume" kuambiwa alipaswa kupewa semina elekezi kabla hajawa Rais ni dongo linalochoma mno japo Mdee hajavunja sheria yoyote ndo maana wamekimbilia kumkokomoa kwa kutumia sheria ya enzi za mkoloni. Na mzee wenu si mnajua hapendagi kupewa makavu live?!
 
Usikute bwana mdogo Hapi aliagizwa na boss wake kufanya alichofanya ili kulinda tumbo lake. Haingii akirini kabisa. Nondo za mtee zitakuwa zilimchoka sana. Mzee wa "mfumo dume" kuambiwa alipaswa kupewa semina elekezi kabla hajawa Rais ni dongo linalochoma mno japo Mdew hajavunja sheria yoyote ndo maana wamekimbilia kumkokomoa kwa kutumia sheria ya enzi za mkoloni. Na mzee wenu si mnajua hapendagi kupewa makavu live?!
Mzee wa kusifiwa.
 
Back
Top Bottom