Kumekuwa na malalamiko kadha wa kadha kuhusu kununuliwa kwa madiwani wa CHADEMA huko Arumeru, binafsi sipingani na malalamiko hayo. Lakini kuna mambo yanayonifikirisha zaidi katika kauli zinazotolewa na walalamikaji.
Mwaka 2015 kulikuwepo na malalamiko ya namna hii, yaliyokihusu CHADEMA kununuliwa na Mh Edward Lowassa kwa mamilioni ya shilingi, lakini malalamiko haya yalibezwa na wanachama wa CHADEMA na kusemwa ni uzushi uliolenga kukichafua chama.
Leo ninyi ni mashahidi wanachama wa CHADEMA nchi nzima wanalalamika madiwani wao kununuliwa na hasimu wao mkuu CCM. Je? Tuwaamini? Na kama tutaamini! Kwanini tusiamini kuwa CHADEMA inanunulika pia, kiasi cha Edward Lowassa kumudu kununua 2015? Wapo watakaodai kuwa hapakuwepo na ushahidi uliothibitisha madai hayo! Je leo tuaminije madai ya kununuliwa kwa madiwani wakati pia hakuna ushahidi wa kuthibitisha hayo madai?
Nadhani ni mda muafaka kama chama kujitafakari na kuchukua hatua namna ya kukabiliana na madhaifu ndani ya chama badala ya kubaki na propaganda zisizo na mashiko. Ni ushauri tu.
Asanteni sana.