Madiwani CHADEMA, CCM wala njama kumpindua Meya Moshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani CHADEMA, CCM wala njama kumpindua Meya Moshi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Mwandishi Wetu  [​IMG]


  Meya wa Moshi


  ULEVI wa madaraka umeanza kukisumbua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro Kutokana na mgogoro wa chini kwa chini unaofukuta miongoni mwa madiwani wa chama hicho wanaotaka kufanya mapinduzi ili kumwondoa madarakani Meya, Michael Jaffary.

  Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba mwaka 2010, CHADEMA kilishinda nafasi ya ubunge kwa kishindo katika Manispaa ya Moshi kwa Philemon Ndesamburo kuwabwaga washindani wake.

  Chama hicho pia kilishinda viti vya udiwani katika kata 17 kati ya 21 vya Chama cha Mapinduzi hivyo CHADEMA kupata fursa ya kuongoza halmshauri hiyo.


  Hata hivyo, pamoja na kupata mafaniko hayo katika kile kiinachoonekana kuwa ni kulewa madaraka baadhi ya madiwani wanadaiwa kuanza kusuka mipango ya kumwondoa Meya katika nafasi yake, wakimtuhumu kuwa hakidhi mahitaji ya kisiasa ya chama na wananchi wa Manispaa ya Moshi.


  Taarifa zilizolifikia Raia Mwema mjini Moshi na baadaye kuthibitishwa na vyanzo kadhaa zilieleza kuwa madiwani wanaoongoza harakati za kutaka kumwondoa Meya huyo wametoka katika kata tatu za manispaa hiyo na mwingine wa viti maalumu pamoja na wale wa Chama cha Mapinduzi.


  Habari zaidi zinaeleza kuwa madiwani hao wanajenga hoja kuwa Meya Michael Jaffary alihusika na operesheni ya kuvunja vituo vya kuoshea magari (car wash) iliyofanyika miezi mitatu iliyopita. Katika operesheni hiyo zaidi ya vituo 20 vilivyunjwa na askari wa manispaa hiyo.


  Vituo hivyo ni vile vilivyojengwa kinyume cha utaratibu na sheria zinazosimamia mipango miji kwa kujengwa katika makazi ya watu, hifadhi ya barabara na maeneo yenye majengo ya umma kama shule.


  Manispaa ya Moshi iliendesha operesheni ya kuvunja vituo hivyo vya kuoshea magari katika kata za Bondeni, Mawenzi, Kilimanjaro na Kiusa na operesheni hiyo ilitekelezwa usiku wa manane kwa kutumia askari wa manispaa hiyo

  Akizungumza na Raia Mwema moja wa madiwani wa CHADEMA katika Wilaya ya Moshi (jina linahifadhiwa) alisema wanazo taarifa za uhakika kuwa madiwani hao wamekuwa wakifanya vikao katika hoteli moja mjini hapa kupanga mipango ya kumwondoa meya madarakani.

  "Ni kweli kuna madiwani wenzetu wameungana na wale wa CCM kusuka mipango ya kumwondoa meya katika nafasi yake na tayari taarifa hizo tunazo na tumeshaanza kuzifanyia kazi," alisema diwani huyo.


  Kiongozi huyo alisema kuwa sababu nyingine inayotolewa na madiwani hao ni hatua ya Manispaa ya Moshi kuvunja pia baadhi ya majengo yaliyojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi katika maeneo ya miji.


  "Wao wanadai kuwa hatua ya kuvunjwa kwa vituo hivyo vya kuoshea magari na pia baadhi ya majengo kutaondoa umaaarufu wa chama hicho mkoani Kilimanjaro hivyo meya awajibishwe kwa kuruhusu kuvunjwa kwa vituo hivyo," alisema.


  Diwani huyo alisema baada ya kufanya vikao vya kusuka mpango huo madiwani hao wamekuwa wakiendelea kufanya ushawishi kwa madiwani wengine ili hoja ya kumwondoa meya itakapoletwa basi iungwe mkono na madiwani wengine.


  "Kinachowasukuma hao madiwani ni uroho wa madaraka tu kwani hoja zao hazina mashiko na masuala wanayoyatetea hayana msingi wala maslahi kwa wananchi wa mji wa Moshi," aliongeza diwani huyo katika mazungumzo yake na gazeti hili.

  Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA katika Manispaa hiyo, Jomba Koi, alikanusha kuwapo kwa mgogoro wowote na kumtaka mwandishi wa RaiaMwema kuachana na habari za aina hiyo.

  "Mimi ni mwenyekiti wa madiwani na hatuna mgogoro wowote ila nakushauri uachane na habari za aina hiyo haina maana yoyote zaidi ya kuleta hali ya vurugu ndani ya chama," alisema Koi.


  Akizungumzia madai hayo Meya wa Manispaa hiyo Michael Jaffary alishindwa kuthibitisha au kukanusha njama hizo za kutaka kumuondoa katika wadhifa huo.

  "Siwezi kuzungumzia hatua hiyo ila nataka nikueleze kuwa kutofautiana kimtazamo ni masuala ya kawaida katika uongozi wa umma na ninachoweza kusema tofauti zilizopo ni za kimtazamo tu ila suala la kutaka kuniondoa madarakani siwezi kulisemea," alisema meya huyo.

  Alisema uamuzi wa kuvunja vituo vinavyolalamikiwa ulifikiwa na vikao halali vya halmashauri na wala si uamuzi wake binafsi hivyo wanaoalalamika kama wapo walikuwa pia sehemu ya uamuzi huo wa pamoja katika halmashauri.


  "Mimi kama Meya siwezi kujiamulia majengo na mali nyingine za wananchi zivunjwe ila hayo ni maamuzi (uamuzi) halali yaliyofikiwa katika vikao vya halmashauri hivyo anayelalamika kuhusu mimi atakuwa hanitendei haki," alisema.


  Kuhusu kuvunjwa kwa baadhi ya majengo Meya huyo alisema kimsingi uamuzi huo pia ulifikiwa katika vikao vya Baraza la Madiwani na hatua hiyo inatokana na matayarisho ya maombi ya mji huo kutaka kuwa jiji.


  "Unajua tumejiwekea malengo ya kuugeuza mji wa Moshi kuwa jiji katika kipindi cha miaka miwili ijayo kuanzia sasa na moja ya sifa zinazotakiwa ni mji kuwa katika mpangilio unaokubalika hivyo Baraza la Madiwani limeazimia kukomesha ujenzi holela usiozingatia sheria za mipango miji," alisema.


  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo, hakuwa tayari kuzungumzia mgogoro huo akisema bado haujafikishwa rasmi ofisini kwake.


  "Sisi ngazi ya mkoa bado hatujapata rasmi taarifa hizo lakini naomba ungeacha kwanza kuandika suala hilo hadi hapo tutakapokutana kwa vikao rasmi na unajua migogoro hii inapokuwa kwenye media (vyombo vya habari) haileti picha nzuri na unavuruga chama," alisema Ndesamburo ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini.


  Naye Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema, alikuwa na maoni tofauti na Ndesamburo akieleza kuwa kutofautiana kwa madiwani hao ni hatua nzuri katika kukuza wigo demokrasia ndani ya chama chao.


  "Sisi kama mkoa bado hatujapata rasmi malalamiko dhidi ya meya au madiwani lakini kama madiwani wanaona kuna dosari miongoni mwao na wakazungumza si jambo baya bali ni katika kupanua wigo wa demokrasia ndani ya chama chetu," alisema Lema.


  Alisema hata hivyo malalamiko hayo yakiwasilishwa yatashughulikiwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kichama na muafaka wake utapatikana kwani CHADEMA ni chama kilichokomaa na kimeshakumbana na matatizo ya aina hiyo.
   
 2. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama raia wanajenga bila mpangilio ni hatua nzuri kubomoa mapema kabla hali haijawa mbaya. Huwezi kuweka garage kila mahali tu bila mpangilio. Ila cha msingi hapa ni kwamba hao wenye garage ni wafanyabiashara na kuna waajiriwa wa kazi hizo wanaotegemea kipato kutoka hapo kwa ajili ya kutunza familia zao. Hivyo wanavyowabomolea wawatafutie maeneo mengine wawape kwa ajili ya kufanya biashara zao. Vinginevyo watakuwa wanawaweka watu katika hali ngumu kimaisha.
  Hao wanaotaka kumwondoa meya kwa sababu hii sidhani kama wanafanya vizuri. Wanachotakiwa ni kumshauri jinsi ambavyo wataweza kupata maeneo mengine ya kuwapa hao waliobomolewa wafanye biashara zao kwa amani.
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Hilo dogo,kamati kuu ya CDM huwa haiogopi kufanya maamuzi magumu
   
 4. M

  MR NDEE Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  vyanzo vyako vina uhakika kiasi gani?uliwahoji kwa njia gani?baraza lipi lilipitisha azimio?je meya na mkurugenzi walipitisha? au kisa ni kwakuwa Kiusa imebomolewa?au unafikiri CDM, iruhusu ujenzi holela? usiwe unatafuta kuchafua Moshim yetu kaa ujue huu ndo mji wa wagumu HATUSHAWISHIKI NA HATUDANGANYIKI
   
 5. milioni

  milioni Member

  #5
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa mapapa wa ccm wanataka kutuharibia mji wetu.
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  hii nayo ni habari? ndo maana jamaa alimuambia muandishi aachane nayo. no meaning.
   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kwako kipi chenye maana?
   
 8. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wawaulize madiwani wa Arusha kilichowasibu endapo wanatamani usaliti!!!!
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hz car wash zote zilizobomolewa zilikua zinamilikiwa na vigogo wa ccm na ndugu zao na zilikua zimejengwa kinyume cha sheria kwenye viwanja vya wazi (open space) na zilikuwa hazilipiwi kodi.
   
 10. mpiganiahaki

  mpiganiahaki Senior Member

  #10
  Nov 26, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Raia mwema niwale wale magamba tu, hayana jipya
  Kwa taarifa yako Moshi ndio ngome kuu ya chadema na hata muandike nini, hamuwezi kutubadilisha watu wa Moshi,
  Na katika uongozi madhubuti wa mzee wetu ndesa pesa na meya wetu Jafari tutahakikisha Moshi inakuwa jiji
  Sisi wana Moshi tunajua ni namna gani magamba inavyo wauma kwa kushindwa kulipata jimbo la Moshi(M) toka tuingie kwenye vyama vingi na kwa hili wanamoshi tunaithamini historia hii na tutailinda hadi tutakapo ifukia ccm kaburini
  Na wewe mwandish katafute kingine tena
   
 11. M

  MR NDEE Member

  #11
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  HAwawezi kutuvuruga KATU,wamwache meya wetu na Bomambuzi yetu,Moshi ni yetu hawana nafasi kabisa,PASUA,BOMAMBUZI,BONDENI,NA KOOOOOTE NI JAFARRY TU, MAPINDUZI KILA SIKU MOSHI IWE JUUU
   
 12. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mapenzi mabaya sana utaki kuamini sababu ya mahaba
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Again! RAIA MWEMA! No comment
   
 14. w

  wikolo JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa nini mwandishi anaanza kwa kusema ulevi wa madaraka umeanza kukisumbua chadema? Ndani ya habari yenyewe anaongelea madiwani watatu tu na wengine wa CCM!! Nadhani lengo lake ni kuichafua chadema tu hakuna lingine hapo. Nimeishitukia hii habari!!
   
Loading...