Madiwani 41 Moshi wamkataa Mkurugenzi wa Halmashauri

Kumbuka CCM hawajawahi kuongoza Halmashauri ya Moshi,hao ni madiwani wa CHADEMA walionunuliwa na mwendazake kugombea CCM,lakini mioyo yao ni Chadema.
Hiyo mioyo yao uliipima hadi ukajua kuwa ni Chadema??.
 
Madiwani 41 wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameandika barua ya kumkataa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kastory Msigala wakimtuhumu kufanya maamuzi binafsi kupitisha baadhi ya miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

Madiwani hao walioandamana hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha barua yao, wanalalamikia ukusanyaji wa mapato hafifu kutokana na utendaji usio shirikishi wa mkurugenzi huyo pamoja na utolewaji wa maamuzi ya utekelezaji wa miradi bila kushirikisha kamati ya fedha na baraza la madiwani.

Hatua hiyo imefikiwa ikiwa zimepita siku chache tangu madiwani wa Manispaa ya Moshi mkoani hapa, kupiga kura za kumkataa Meya wa Manispaa hiyo, Juma Raibu.

Akizungumza jana baada ya kikao cha madiwani kilichokaa ofisi za CCM wilayani Moshi, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Moris Makoi alisema tatizo hilo ni la muda mrefu na wamekuwa wakimlalamikia lakini hakuna mabadiliko, ndiyo maana wameamua kuandika barua hiyo. “Fedha za halmashauri zinapoletwa kutoka Serikali kuu kwa ajili ya maendeleo, mkurugenzi anatakiwa kutoa tangazo likieleza matumizi ya fedha hizo na kamati ya fedha ndiyo yenye mamlaka ya kuidhinisha manunuzi yote ya halmashauri kikanuni,” alisema.

Ujenzi Hospitali ya Wilaya

Katika hatua nyingine, Makoi alizungumzia changamoto ya Hospitali ya Wilaya, akisema Moshi kumekuwa na changamoto ya eneo na walitarajia wangekaa na mkurugenzi kukubaliana wajenge majengo ya ghorofa lakini imeonekana mkurugenzi alitaka lipatikane eneo la hekari 30 kwa ajili ya Hospitali hiyo.

“Jambo hilo lilisababisha Kamati ya Mipango na Fedha iitishe vigezo kutoka Wizara ya Afya, kujua ili eneo lijengwe hospitali ni nini ambacho kinahitajika, lakini tulipoletewa moja ya kigezo ilikiwa ni eneo husika kufikika na kata zote za halmashauri husika. Halmashauri hii ina majimbo mawili na kata 32.

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa, awali mkurugenzi aliwaandikia madiwani wote barua kuwataka kutafuta eneo la kujenga hospitali hiyo na baadhi walileta lakini hakuyafuatilia na badala yake amekuwa akiwagawa na kutoa maamuzi binafsi.

Kwa upande wake Diwani wa Uru kusini, Wilhad Kitali alisema wamechaguliwa kutetea maslahi ya wananchi na inapofika mahali wanaona kasi ya ukusanyaji wa mapato inashuka ni lazima wapige kelele yaongezeke na fedha ipatikane kuwaletea maendeleo wananchi.

“Tumekutana madiwani katika ofisi za chama ili kujadili mwenendo mbovu wa halmashauri yetu, tumechaguliwa kuhakikisha tunapigania maslahi ya wananchi, leo tumefika hapa kuyazungumzia na tunaamini kwa kuwa CCM ni chama sikivu, malalamiko yetu yatafanyiwa kazi,” alisema.

Mkurugenzi, RAS wazungumza

Akijibu malalamiko hayo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Kastory Msigala alisema Mwenyekiti wa Halmashauri ndiye msemaji mkuu na kama ana jambo atamwita mkurugenzi, likimshinda atalipeleka kwa mkuu wa wilaya au mkoa.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu madiwani hao kupeleka barua kwa mkuu wa mkoa, alisema anasubiri maelekezo ya mkoa.

Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Willy Machumu alithibitisha ofisi ya mkoa kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi Vijijini, aliyomuandikia Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, wakimtuhumu mkurugenzi wa halmashauri hiyo kukiuka taratibu na miongozo ya Serikali.

“Kwa utaratibu suala hili analishughulikia Mkuu wa Wilaya kwa kuwa ndiye mwenye wilaya husika. Sisi Mkoa tunasubiri vikao halali kati ya Mkuu wa Wilaya, mkurugenzi wa Halmashauri na mwenyekiti,” alisema Machumu.
Hawa Wachaga hawataki kila kitu? Tuliwapelekea pale mradi wa viberenge katika jitihadi za kuiboost Kilimanjaro ifikie hadhi ya kuwa jiji, wakaukataa!
Niliwashangaa sana eti wanalilia ajira ya kubeba mabegi itakufa. Nikawauliza swali moja, stendi ya mabasi ya mikoani ya Magufuli haina mlima, lakini ukiwauliza vijana wa boda boda pale wanabeba mabegi zaidi ya laki moja kwa siku; asubuhi na jioni. Nikawauliza hawa Wachaga, je pale Mbezi kuna mlima? Kama hakuna, kwanini biashara ya kubeba mabegi kwa kina boda boda imeshamiri, wao wanahofia nini?
Kifupi, nawashauri hawa wakwe zangu (ndugu zangu wawili wameoa huko) waache kuwa rigid. Otherwise watajikuta wanabaki nyuma...
 
Ukifika kwenye halmashauri halafu ukasikiliza argument za madiwani utagundua kwamba kazi Bado ni ndefu sana. Madiwani wengi ni hopeless.
Mwisho wa siku, hao Madiwani ni reflection ya Jamii husika kwasababu huchaguliwa na Jamii husika kupitia sanduku la kura.

In short, When it comes to democracy kubaliana na yote, na ndio maana hata Lema, Sugu na Msigwa walikuwa Wabunge.
 
kwa akili Za madiwani hapo utakuta Mkurugenzi alikua anawanyima posho
 
Kumbuka CCM hawajawahi kuongoza Halmashauri ya Moshi,hao ni madiwani wa CHADEMA walionunuliwa na mwendazake kugombea CCM,lakini mioyo yao ni Chadema.
Hii ni kweli 100% hawa madiwani ni chadema waliovalia koti la ccm. Hata wale wa Moshi waliomtimua Meya ni chadema 100%
 
Madiwani 41 wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameandika barua ya kumkataa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kastory Msigala wakimtuhumu kufanya maamuzi binafsi kupitisha baadhi ya miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

Madiwani hao walioandamana hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha barua yao, wanalalamikia ukusanyaji wa mapato hafifu kutokana na utendaji usio shirikishi wa mkurugenzi huyo pamoja na utolewaji wa maamuzi ya utekelezaji wa miradi bila kushirikisha kamati ya fedha na baraza la madiwani.

Hatua hiyo imefikiwa ikiwa zimepita siku chache tangu madiwani wa Manispaa ya Moshi mkoani hapa, kupiga kura za kumkataa Meya wa Manispaa hiyo, Juma Raibu.

Akizungumza jana baada ya kikao cha madiwani kilichokaa ofisi za CCM wilayani Moshi, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Moris Makoi alisema tatizo hilo ni la muda mrefu na wamekuwa wakimlalamikia lakini hakuna mabadiliko, ndiyo maana wameamua kuandika barua hiyo. “Fedha za halmashauri zinapoletwa kutoka Serikali kuu kwa ajili ya maendeleo, mkurugenzi anatakiwa kutoa tangazo likieleza matumizi ya fedha hizo na kamati ya fedha ndiyo yenye mamlaka ya kuidhinisha manunuzi yote ya halmashauri kikanuni,” alisema.

Ujenzi Hospitali ya Wilaya

Katika hatua nyingine, Makoi alizungumzia changamoto ya Hospitali ya Wilaya, akisema Moshi kumekuwa na changamoto ya eneo na walitarajia wangekaa na mkurugenzi kukubaliana wajenge majengo ya ghorofa lakini imeonekana mkurugenzi alitaka lipatikane eneo la hekari 30 kwa ajili ya Hospitali hiyo.

“Jambo hilo lilisababisha Kamati ya Mipango na Fedha iitishe vigezo kutoka Wizara ya Afya, kujua ili eneo lijengwe hospitali ni nini ambacho kinahitajika, lakini tulipoletewa moja ya kigezo ilikiwa ni eneo husika kufikika na kata zote za halmashauri husika. Halmashauri hii ina majimbo mawili na kata 32.

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa, awali mkurugenzi aliwaandikia madiwani wote barua kuwataka kutafuta eneo la kujenga hospitali hiyo na baadhi walileta lakini hakuyafuatilia na badala yake amekuwa akiwagawa na kutoa maamuzi binafsi.

Kwa upande wake Diwani wa Uru kusini, Wilhad Kitali alisema wamechaguliwa kutetea maslahi ya wananchi na inapofika mahali wanaona kasi ya ukusanyaji wa mapato inashuka ni lazima wapige kelele yaongezeke na fedha ipatikane kuwaletea maendeleo wananchi.

“Tumekutana madiwani katika ofisi za chama ili kujadili mwenendo mbovu wa halmashauri yetu, tumechaguliwa kuhakikisha tunapigania maslahi ya wananchi, leo tumefika hapa kuyazungumzia na tunaamini kwa kuwa CCM ni chama sikivu, malalamiko yetu yatafanyiwa kazi,” alisema.

Mkurugenzi, RAS wazungumza

Akijibu malalamiko hayo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Kastory Msigala alisema Mwenyekiti wa Halmashauri ndiye msemaji mkuu na kama ana jambo atamwita mkurugenzi, likimshinda atalipeleka kwa mkuu wa wilaya au mkoa.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu madiwani hao kupeleka barua kwa mkuu wa mkoa, alisema anasubiri maelekezo ya mkoa.

Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Willy Machumu alithibitisha ofisi ya mkoa kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi Vijijini, aliyomuandikia Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, wakimtuhumu mkurugenzi wa halmashauri hiyo kukiuka taratibu na miongozo ya Serikali.

“Kwa utaratibu suala hili analishughulikia Mkuu wa Wilaya kwa kuwa ndiye mwenye wilaya husika. Sisi Mkoa tunasubiri vikao halali kati ya Mkuu wa Wilaya, mkurugenzi wa Halmashauri na mwenyekiti,” alisema Machumu.
Atakuwa kawanyea nyie wachaga.

Huyo bwana namfahamu nimrfanya nae Kazi ni mtu hapendi unabaishaji,majungu na shortcut
 
Huyo Moris Makoi achunguzwe kwanza. Anatumia udiwani wake na uenyekiti wa halmashauri kunyanyasa wananchi. Mkoani Arusha anajulikana Kwa unyanyasaji wake. Serkali imchunguze kwanza kuhusu vibanda zaidi ya 30 anavyovimiliki eneo la stand ndogo, kuhusu uhalali wake, na unyang'anyi mkubwa ambao amewafanyia wananchi ambao huwapangishia hivyo vibanda Kwa Hila. Makoi anasema vibanda hivyo alipewa na mheshimiwa waziri mkuu, amekua anaikwamiah serkali kufanya mbotesho eneo lile, na yeye huikosesha serkali mapato, nae hikisanya fedha nyingi kuliko Jiji katika eneo Hilo. Kibabe yeye amejipa tend ya ulinzi kwenye vile vibanda kila mwisho wa mwez kampuni yake inakusanya usshuru wa ulinzi, na Kwa vile anajua yeye ndo mwenye kampuni ya ulinzi inayolinda eneo la stendi ndogo, saizi amezua taharuki na kutishia vibanda vitachomwa moto ikiwa wale wafanyabiashara wanaofanya biashara zao pale watasikiliza serkali. Yan mtu mmoja awe na vibanda vyote hivyo, ulinzi, choo, inatafakarisha. Pia Hilo vuguvugu la kumkataa mkurugenzi wa Jiji hata huku Arusha yupo nyuma ya hayo magenge, na huwakataa wakurugenzi pindi wanapogusa maslahi yake. Mwenyekiti makoy achunguzwe kwanza
 
Walianza na Meya, sasa Mkurugenzi, kituo kinachofuata itakuwa ni...?
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ndiyo walimkataa Meya.

Hawa ni madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi wanamkataa Mkurugenzi wao.

Wilaya ya Moshi ina Halmashauri mbili kama nilivyozitaja japo juu.
 
Back
Top Bottom