Madiwani 41 Moshi wamkataa Mkurugenzi wa Halmashauri

Madiwani 41 Moshi wamkataa Mkurugenzi wa Halmashauri

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
18,010
Reaction score
30,987
Madiwani 41 wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameandika barua ya kumkataa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kastory Msigala wakimtuhumu kufanya maamuzi binafsi kupitisha baadhi ya miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

Madiwani hao walioandamana hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha barua yao, wanalalamikia ukusanyaji wa mapato hafifu kutokana na utendaji usio shirikishi wa mkurugenzi huyo pamoja na utolewaji wa maamuzi ya utekelezaji wa miradi bila kushirikisha kamati ya fedha na baraza la madiwani.

Hatua hiyo imefikiwa ikiwa zimepita siku chache tangu madiwani wa Manispaa ya Moshi mkoani hapa, kupiga kura za kumkataa Meya wa Manispaa hiyo, Juma Raibu.

Akizungumza jana baada ya kikao cha madiwani kilichokaa ofisi za CCM wilayani Moshi, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Moris Makoi alisema tatizo hilo ni la muda mrefu na wamekuwa wakimlalamikia lakini hakuna mabadiliko, ndiyo maana wameamua kuandika barua hiyo. “Fedha za halmashauri zinapoletwa kutoka Serikali kuu kwa ajili ya maendeleo, mkurugenzi anatakiwa kutoa tangazo likieleza matumizi ya fedha hizo na kamati ya fedha ndiyo yenye mamlaka ya kuidhinisha manunuzi yote ya halmashauri kikanuni,” alisema.

Ujenzi Hospitali ya Wilaya

Katika hatua nyingine, Makoi alizungumzia changamoto ya Hospitali ya Wilaya, akisema Moshi kumekuwa na changamoto ya eneo na walitarajia wangekaa na mkurugenzi kukubaliana wajenge majengo ya ghorofa lakini imeonekana mkurugenzi alitaka lipatikane eneo la hekari 30 kwa ajili ya Hospitali hiyo.

“Jambo hilo lilisababisha Kamati ya Mipango na Fedha iitishe vigezo kutoka Wizara ya Afya, kujua ili eneo lijengwe hospitali ni nini ambacho kinahitajika, lakini tulipoletewa moja ya kigezo ilikiwa ni eneo husika kufikika na kata zote za halmashauri husika. Halmashauri hii ina majimbo mawili na kata 32.

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa, awali mkurugenzi aliwaandikia madiwani wote barua kuwataka kutafuta eneo la kujenga hospitali hiyo na baadhi walileta lakini hakuyafuatilia na badala yake amekuwa akiwagawa na kutoa maamuzi binafsi.

Kwa upande wake Diwani wa Uru kusini, Wilhad Kitali alisema wamechaguliwa kutetea maslahi ya wananchi na inapofika mahali wanaona kasi ya ukusanyaji wa mapato inashuka ni lazima wapige kelele yaongezeke na fedha ipatikane kuwaletea maendeleo wananchi.

“Tumekutana madiwani katika ofisi za chama ili kujadili mwenendo mbovu wa halmashauri yetu, tumechaguliwa kuhakikisha tunapigania maslahi ya wananchi, leo tumefika hapa kuyazungumzia na tunaamini kwa kuwa CCM ni chama sikivu, malalamiko yetu yatafanyiwa kazi,” alisema.

Mkurugenzi, RAS wazungumza

Akijibu malalamiko hayo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Kastory Msigala alisema Mwenyekiti wa Halmashauri ndiye msemaji mkuu na kama ana jambo atamwita mkurugenzi, likimshinda atalipeleka kwa mkuu wa wilaya au mkoa.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu madiwani hao kupeleka barua kwa mkuu wa mkoa, alisema anasubiri maelekezo ya mkoa.


Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Willy Machumu alithibitisha ofisi ya mkoa kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi Vijijini, aliyomuandikia Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, wakimtuhumu mkurugenzi wa halmashauri hiyo kukiuka taratibu na miongozo ya Serikali.

“Kwa utaratibu suala hili analishughulikia Mkuu wa Wilaya kwa kuwa ndiye mwenye wilaya husika. Sisi Mkoa tunasubiri vikao halali kati ya Mkuu wa Wilaya, mkurugenzi wa Halmashauri na mwenyekiti,” alisema Machumu.
 
Walianza na Meya, sasa Mkurugenzi, kituo kinachofuata itakuwa ni...?
 
Watajuana wenyewe. Sisi hayatuhusu.
Kwenye amani hawatushirikishi na sisi kwenye shida zao wasitushirikishe.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki yeyote atendaye mema katika utumishi na uongozi wake
 
Enzi za Mzee baba sijui kama haka kamchezo Ka kuwatoa wenzao wa chama Chao kangefanyika. wanamuonea mama ni mpole.
Ulikuwepo Tz kweli? Kipindi Cha Magufuli madiwani ndio walichachsmaa kuwakataa wakurugenzi sehemu nyingi Sana
Songwe, Serengeti, mwanga, shinyang, buchosa.
Hizo ni sehemu chache ambazo madiwani walimkataa mkurugenzi enzi ya jiwe
 
Kata 32 ziifikie hospital moja ya wilaya hilo haliwezekani.
Wilaya ya Moshi ni kuanzia kibosho mpaka ukatoboe Marangu huko kwa Mrema ni kipande kirefu.

Mimi nafikiri kwa kuwa wilaya hii imejaliwa hospital za dini nyingi kama Kibosho DDH nk vituo vya afya viko vingi pia, lakini pia wengi wana access ya mawenzi na KCMC, sio lazima hiyo hsptl ijengwe katikati.
Ijengwe kwenye upande ambao wanaona bado hakuna hsptl ya karibu hata kama ni huko mabogini, kahe nk
 
Back
Top Bottom