madirisha ya aluminium

Elijah

JF-Expert Member
May 28, 2012
1,663
416
wakuu salama??Nimefungua workshop yangu kwa ajili ya kutengeneza na kufitisha madirisha ya aluminium kwenye nyumba,ni mjasiriamali mdog,naomba sapoti yenu,tuko tayari kuja eneo lako la ujenzi na kuchukua vipimo na kutoa quotation,msijali bei ni nafuu,just pm tutawasiliana na kukufikia
 
Weka namba ya simu na ikiwezekana jina la kampuni na mahali, pia kama una picha za kazi yako itasaidia.
 
Uko mkoa gani?
 

Mkuu biashara matangazo, huhitaji mpaka watu waku-PM tuambie hapa hapa bei ikoje kwa square meter kwa dirisha la unene wa sm 8 na sm 10. Pia kama wadau walivyosema hapo juu sema uko mkoa gani na tupe sampuli ya kazi zako. Binafsi niko kwenye mchakato wa kutafuta mtu wa kazi hii kwahiyo fanya fasta kabla sijampa kazi mtu mwingine.
 
Funguka bwana tupo wengi wenye kazi hiyo.Weka namba za simu hapa.
 
Sisi wafanyabiashara wa kibongo mawasiliano ni tatizo kubwa, unatangazo halafu haupatikani na unataka kuungwa mkono!
 
Kimyaaaaaaaaaaaaaaaa kuna umuhimu wa kuanzisha shule ya kutoa matangazo humu JF
 
Sawa,
Kuna fremu ipo hapa KIA, njia panda ya Airport, katikati ya Moshi na Arusha, nahitaji kuweka hiyo kitu, ni dirisha la urefu mita 2 na upana mita 2 pia.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…