Madini ya Sh15.8 bilioni yakamatwa yakitoroshwa

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,603
Reaction score
22,717
Chalinze. Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA), umekamata madini yenye thamani ya Sh15.8 bilioni yaliyokuwa yakitoroshwa kwenda nje ya nchi bila ya kibali na kukwepa kulipa kodi ya mapato.

Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Uzalishaji na Biashara ya Madini wa TMAA, Conrad Mtui alisema kuwa kiasi hicho cha madini aina mbalimbali kilikamatwa kati ya Julai, 2012 hadi Agosti, mwaka huu.

Mtui aliwaambia waandishi wa habari juzi katika ziara ya kutembelea migodi ya madini ya ujenzi ya Lugoba na Msolwa wilayani Bagamoyo, kuwa wakala ulikamata madini hayo katika matukio 53 ambayo yaliwahusisha mawakala wa madini.

"Baada ya kuanzisha madawati ya ukaguzi kwenye viwanja vya Kimataifa vya Ndege vya Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro na Mwanza, tuliwakamata wote waliokuwa wakijaribu kusafirisha madini hayo kinyume cha sheria, matukio haya yanaweza pia kuongezeka muda wowote.

"Wahusika wamefikishwa mahakamani na baadhi yao wamehukumiwa na madini yao kutaifishwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010," alisema Mtui.

Alipoulizwa kama kuna wachimbaji wakubwa waliokamatwa wakifanya hujuma hiyo, Mtui alisema waliokamatwa wengi walikuwa wafanyabiashara wadogo na madalali na hakukuwa na kampuni kubwa kwa kuwa kuna utaratibu maalumu wa ukaguzi na usafirishaji.

Hata hivyo, Mtui alisema baada ya kukaza uzi wa ukaguzi walifanikiwa kuongeza mrabaha kutoka kwenye migodi mikubwa ya dhahabu kiasi cha Dola za Marekani 427.98 kuanzia mwaka 2005 hadi mwishoni mwa Agosti mwaka huu.

"Wakala ulifanya ukaguzi na uhakiki wa madini yaliyozalishwa na kuuzwa na migodi mikubwa nchini. Ukaguzi huo ulisaidia kujua kiasi na thamani halisi ya madini yaliyozalishwa na kuuzwa kutoka migodi mbalimbali, ikiwamo saba ya dhahabu ya Geita, Golden Pride, Bulyanhulu, Tulawaka, North Mara, Buzwagi na New Luika," alisema.

Pamoja na kujinadi kwa mafanikio hayo, Mtui alisema bado kuna ujanja wa utoroshaji kupitia njia za panya na upungufu wa rasilimali watu unawazuia kufanya ukaguzi katika migodi midogo, hivyo kuchangia upotevu wa mapato.

"Tuna wakaguzi wetu katika baadhi ya migodi midogo yenye uzalishaji mkubwa...lakini kwa mingine ni hasara kwa sababu unaweza kukuta malipo ya wakaguzi ni makubwa kuliko mrabaha unaopatikana," alisema.

Chanzo:
Mwananchi
 
....Inakuwaje watu hao wanakuwa na idea hiyo?udhaifu serikalini
 
....inakuwaje watu hao wanakuwa na idea hiyo?udhaifu serikalini

shehe nchi hii haina mwenyewe, ukipata 'loop hole' piga hela mkuu,ukiwa mwaminifu hakuna atakaye kuthamini.
 
alaf uwaambie maisha magumu, watakushangaa!! bilioni!!
 
"Wakala ulifanya ukaguzi na uhakiki wa madini yaliyozalishwa na kuuzwa na migodi mikubwa nchini. Ukaguzi huo ulisaidia kujua kiasi na thamani halisi ya madini yaliyozalishwa na kuuzwa kutoka migodi mbalimbali, ikiwamo saba ya dhahabu ya Geita, Golden Pride, Bulyanhulu, Tulawaka, North Mara, Buzwagi na New Luika," alisema.

Pamoja na kujinadi kwa mafanikio hayo, Mtui alisema bado kuna ujanja wa utoroshaji kupitia njia za panya na upungufu wa rasilimali watu unawazuia kufanya ukaguzi katika migodi midogo, hivyo kuchangia upotevu wa mapato.

"Tuna wakaguzi wetu katika baadhi ya migodi midogo yenye uzalishaji mkubwa...lakini kwa mingine ni hasara kwa sababu unaweza kukuta malipo ya wakaguzi ni makubwa kuliko mrabaha unaopatikana," alisema.

Chanzo:
Mwananchi

Hizi taarifa zao za ukaguzi na uhakiki wa madini yaliyozalishwa na kuuzwa na migodi mikubwa zina usahihi kiasi gani?

Na hao wakaguzi wa TMAA wanadhibitiwa vipi?!
 
Chalinze. Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA), umekamata madini yenye thamani ya Sh15.8 bilioni yaliyokuwa yakitoroshwa kwenda nje ya nchi bila ya kibali na kukwepa kulipa kodi ya mapato.

Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Uzalishaji na Biashara ya Madini wa TMAA, Conrad Mtui alisema kuwa kiasi hicho cha madini aina mbalimbali kilikamatwa kati ya Julai, 2012 hadi Agosti, mwaka huu.

Mtui aliwaambia waandishi wa habari juzi katika ziara ya kutembelea migodi ya madini ya ujenzi ya Lugoba na Msolwa wilayani Bagamoyo, kuwa wakala ulikamata madini hayo katika matukio 53 ambayo yaliwahusisha mawakala wa madini.

“Baada ya kuanzisha madawati ya ukaguzi kwenye viwanja vya Kimataifa vya Ndege vya Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro na Mwanza, tuliwakamata wote waliokuwa wakijaribu kusafirisha madini hayo kinyume cha sheria, matukio haya yanaweza pia kuongezeka muda wowote.

“Wahusika wamefikishwa mahakamani na baadhi yao wamehukumiwa na madini yao kutaifishwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010,” alisema Mtui.

Alipoulizwa kama kuna wachimbaji wakubwa waliokamatwa wakifanya hujuma hiyo, Mtui alisema waliokamatwa wengi walikuwa wafanyabiashara wadogo na madalali na hakukuwa na kampuni kubwa kwa kuwa kuna utaratibu maalumu wa ukaguzi na usafirishaji.

Hata hivyo, Mtui alisema baada ya kukaza uzi wa ukaguzi walifanikiwa kuongeza mrabaha kutoka kwenye migodi mikubwa ya dhahabu kiasi cha Dola za Marekani 427.98 kuanzia mwaka 2005 hadi mwishoni mwa Agosti mwaka huu.

“Wakala ulifanya ukaguzi na uhakiki wa madini yaliyozalishwa na kuuzwa na migodi mikubwa nchini. Ukaguzi huo ulisaidia kujua kiasi na thamani halisi ya madini yaliyozalishwa na kuuzwa kutoka migodi mbalimbali, ikiwamo saba ya dhahabu ya Geita, Golden Pride, Bulyanhulu, Tulawaka, North Mara, Buzwagi na New Luika,” alisema.

Pamoja na kujinadi kwa mafanikio hayo, Mtui alisema bado kuna ujanja wa utoroshaji kupitia njia za panya na upungufu wa rasilimali watu unawazuia kufanya ukaguzi katika migodi midogo, hivyo kuchangia upotevu wa mapato.

“Tuna wakaguzi wetu katika baadhi ya migodi midogo yenye uzalishaji mkubwa...lakini kwa mingine ni hasara kwa sababu unaweza kukuta malipo ya wakaguzi ni makubwa kuliko mrabaha unaopatikana,” alisema.

Chanzo:
Mwananchi

Kwahiyo ukaguzi ulianza toka August 2012 na ripoti inatolewa September 2014. My country Tanzania.
 
Hii inaonyesha udhaifu mkubwa uliopo kwenye serikali ya ccm
 
Chalinze. ................... kwenye migodi mikubwa ya dhahabu kiasi cha Dola za Marekani 427.98 kuanzia mwaka 2005 hadi mwishoni mwa Agosti mwaka huu.

"Wakala ulifanya ukaguzi na uhakiki wa madini yaliyozalishwa na kuuzwa na migodi mikubwa nchini. Ukaguzi huo ulisaidia kujua kiasi na thamani halisi ya madini yaliyozalishwa na kuuzwa kutoka migodi mbalimbali, ikiwamo saba ya dhahabu ya Geita, Golden Pride, Bulyanhulu, Tulawaka, North Mara, Buzwagi na New Luika," alisema.

.......................kupitia njia za panya na upungufu wa rasilimali watu unawazuia kufanya ukaguzi katika migodi midogo, hivyo kuchangia upotevu wa mapato.

"Tuna wakaguzi wetu katika baadhi ya migodi midogo yenye uzalishaji mkubwa...lakini kwa mingine ni hasara kwa sababu unaweza kukuta malipo ya wakaguzi ni makubwa kuliko mrabaha unaopatikana," alisema.

Chanzo:
Mwananchi

Nchi ya wagagagigikoko hii.

Wazungu walishajua ujinga,udhaifu na ufisadi unaotamalaki kwa watawala wa nji hii. Nawahakikishia katika muda wa miaka 10-20 ijayo nchi hii itakuwa imebakia mashimo na milima ya udongo utakaokuwa umeachwa na wazungu baada ya kuvuna madini yote!!!

Sijaelewa hii figure ni mamilioni,mabilioni au dola tu 427.98?kiasi cha Dola za Marekani 427.98 kuanzia mwaka 2005 hadi mwishoni mwa Agosti mwaka huu. Lakini hawa jamaa wa TMAA wanajikosa tu kwa Watz lakini hakuna wanachofanya. Mbona hawajaainisha ni madini ya aina gani,uzito gani na bei yake sokoni? Mbona hawajasema kuhusu DHAHANU inayotoroshwa kwa Helikopta kila siku zinazoruka moja kwa moja toka kweny machimbi hayo huku zikiwa zimesheheni tani na tani za madini na hao jamaa hawalipi hata sentano, hakuna cha mrahaba wala mraba! Angalia TANZANITE inavyoibwa kule Mererani mpaka inafikia kuwa nchi zinazotorosha ndizo zinaonekana kwenye soko zinazo zalisha madini hayo kwa wingi.

Halafu unakuwa na Rais dhaifu kazi yake ni kukenua meno na kuchekacheka tu na hana mamuuzi hao. Kwenye Katiba yao pendekezwa swala la Raslimali za Taifa limezungumzwa kwa juujuu tu maana wana uhakika sheria ya Maadili ya Viongozi na Ufisadi yametupwa nje na hivo Watawala wa CCM wamejihakikishia Ulaji wa uhakika kwa miaka mingi mingine ijayoi!

Hivi ile ndege ndogo ya mizigo toka Kenya iliyoanguka katika mbuga ya Serengeti mwanzoni mwa mwezi wa 9 baada ya kuruka toka Mwanza ilikuwa imebeba nini?
 
Back
Top Bottom