Madini ya bati yatishia kasi ya kilimo mkoani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madini ya bati yatishia kasi ya kilimo mkoani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Oct 16, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Imeandikwa na Deus Gabone, Karagwe;

  Tarehe: 15th October 2011  KUIBUKA ghafla kwa soko la madini ya bati yanayopatikana katika wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera, huenda kukaathiri jitihada za serikali za kufufua kilimo kupitia sera ya Kilimo Kwanza.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, kilo moja ya madini hayo huuzwa kwa kati ya Sh 17,000 na Sh 20,000, hali iliyochangia kuwavutia wengi, hasa wakulima ambao wameamua kutelekeza mashamba yao na kukimbilia katika biashara ya madini ya bati ambayo soko lake lipo nchi jirani ya Uganda.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wachimbaji hao wamedai kuwa, wameyachukuliwa madini kama mkombozi wao, baada ya kulima kwa muda mrefu, lakini mazao yao yakikosa soko la uhakika na hivyo kupata usumbufu katika kuchangia shughuli za maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za kata na zahanati.

  "Lakini sasa madini yanalipa, hatuwakimbii tena wanaochangisha fedha za miradi ya maendeleo," anasema mmoja wa wakazi wa kijiji cha Nyaruzumbula yalipo machimbo hayo.

  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kaitambuzi, Deodatus Kainamula amethibitisha wakazi wengi kuchangamkia madini ya bati na kuongeza kuwa, kwa takribani miaka miwili sasa, wananchi wana uwezo wa kuchangia shughuli za maendeleo bila ya usumbufu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sasa hivi utasikia wageni wamepewa eneo wanatupiga bao kwa kuhonga viongozi wetu milioni mia tat mia tatu
   
 3. k

  kituro Senior Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  gazeti gani mkuu!
   
Loading...