Madini aina ya Graphite yamegundulika huko wilayani Handeni

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Madini aina ya Graphite yanayotumika kutengenezea vipuri vya magari na yanayozalisha nishati ambayo pia inatumika kuendeshea magari badala ya kutumia mafuta, yamegundulika huko wilayani Handeni mkoani Tanga.

Kufuatia kugundulika kwa madini hayo tayari wawekezaji wamefika kwenye kijiji kilichogundulika madini hayo cha Kwamsisi kilichopo wilayani Handeni kuanza uwekezaji wa kuchimba madini hayo ambayo ni adimu hapa duniani.

Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amewataka wawekezaji kufika wilayani hapo hasa kwenye sekta ya madini kwasababu handeni ni moja kati ya wilaya zenye hazina kubwa ya madini.

Kufuatia hatua Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Wiliam Makufwe amedai kuwa kupatikana kwa madini hayo kutaiongezea mapato halmashauri yake pamoja na taifa kwa ujumla.
 
Wananchi wa kwamsisi tumesema hatutaki yachukuliwe madini yetu tutatafuta wawekezaji wenyewe ila kama wabishi waache wachukue ZONGO litaongea tusije kulaumiana baadae 👹👹👹
 
Wanaanza kwa mbwembwe kwakusema wananchi watakombolewa kiuchumi. Mradi ukikolea hali ya wananchi inabaki vilevile.
 
Weka kuta RAISI MAGUFULI wangu maana ukitoa Nigeria kwa wizi wa hapa na pale, TZ inafuatia katika ubora huo huo Afrika nzima.
 
1. Wananchi watafaidika na ugunduzi huu
2. Serikali itapata mapato
3. Ajira
4. Fidia
5. Tupo kwenye upembuzi
6. Hatukupata kitu
7. Mgodi unauzwa

Walah hayo hapo juu ni maneno ya ubeti kwenye wimbo wa ugunduzi wa madini
Haha haaaaaaaa
Mwishi wa siku utasikia

Tulipata hasara sana tulinunua mgodi usio na kitu tunafunga mgodi.

Byeeeeeeee
 
Madini aina ya Graphite yanayotumika kutengenezea vipuri vya magari na yanayozalisha nishati ambayo pia inatumika kuendeshea magari badala ya kutumia mafuta, yamegundulika huko wilayani Handeni mkoani Tanga.

Kufuatia kugundulika kwa madini hayo tayari wawekezaji wamefika kwenye kijiji kilichogundulika madini hayo cha Kwamsisi kilichopo wilayani Handeni kuanza uwekezaji wa kuchimba madini hayo ambayo ni adimu hapa duniani.

Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amewataka wawekezaji kufika wilayani hapo hasa kwenye sekta ya madini kwasababu handeni ni moja kati ya wilaya zenye hazina kubwa ya madini.

Kufuatia hatua Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Wiliam Makufwe amedai kuwa kupatikana kwa madini hayo kutaiongezea mapato halmashauri yake pamoja na taifa kwa ujumla.
Let's hope ma beberu hawatayachukua nakutuachia mashimo bila kufukia
 
  • Thanks
Reactions: m99
Madini hayo kitambo sana watu tulishayagumia hko kusini

Ova
 
Back
Top Bottom