Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,618
Mwalimu wa miaka mingi na mzoefu, Richard Mabala, viongozi wengi wamepita mikononi mwake, mwandishi wa vitabu maarufu ya masomo kikiwemo Mabala the Farmer na Hawa the Bus Driver ambavyo wengi tumevitumia shuleni.
Mwalimu huyu bingwa anaelewa madhara ya viboko kwa watoto.
Tunaamini adhabu haina mbadala. Nidhamu hufunzwa haiadhibiwi. Watoto wakipendwa huiga upendo na kufanya makubwa wakichukiwa huiga chuki, wakifanyiwa ukatili na wao wana uwezekano wa kutumia mbinu za kikatili ukubwani.
Mawasiliano kati ya mtoto na mtu mzima yakiwa bora mtoto hufanya lolote lile mtu yule analomuelekeza. Mtoto ni binadamu kamili mwenye kusikia machungu na kuweka kumbu kumbu.
Tunaamini binadamu wote wanaofanya ukatili leo hii walijifunza ukatili au waliushuhudia wakauiga.
Tujenge Dunia yenye kuamini mbinu za amani katika maendeleo ya Kisiasa na Kiuchumi kwa kuandaa kizazi cha watoto wenye maadili, nidhamu, utii, heshima na uzalendo wa kweli bila kutumia mbinu za kikatili.
Tunaomba kusisitiza nidhamu na maasili inajengwa na watoto wanapaswa kukua wakiiga kutoka kwako mtu mzima na waielewe kama msingi mkuu katika maisha. Epuka kutumia ukatili kumjengea nodhamu na maadili, ishi ukiwa mfano kwake na hakikisha anaelewa umuhimu wa kutunza muda, mahusiano bora, uaminifu, ubora wa kazi ikiwemo uzingatiaji wa elimu, kujitunza mwenyewe na kutunza utu wa wengine.
Kwakuwa sisi wengi Watanzania tumelelewa kwa viboko, bado hatuna ushahidi vilianza lini hasa, tunaelewa kasumba hii imeota mizizi na wengi hatuelewi mbinu mbadala ya malezi kwa mtoto bila viboko. Inaeleweka kwa sababu hata mila potofu zenye madhara zilianza kama mazoea na leo hii zimeota mizizi tunapambana nazo baada ya kugundua tukiziacha tutanufaika zaidi kuliko kuendelea nazo.
Mabadiliko yanaanza na mimi na wewe.
Nini kifanyike kukomesha viboko? Alafu mtu anatueleza kuwa shuleni ni sehemu salama!