Madhara ya ujamaa bado yanalitafuna Taifa

ze farmer

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
922
Reaction score
1,821
Pamoja na mengi mazuri yalifanywa na serikali ya awamu ya kwanza lazima tukubali ujamaa ilikuwa ni KOSA LA KIUFUNDI KABISA. Naaandika haya kwa kuzingatia kuwa ukiisema serikali ya awamu ya kwanza kwa mabaya yake basi wewe si mzalendo (Niko tayari kwa hilo).
Mosi. Wakati wa kampeni liliibuka suala la mtu ukiwa tajiri huwezi kuwa raisi wa Tanzania ukiuliza sababu utaendelea kuambiwa atauza nchi au amepata utajiri kwa rushwa. Hili litaendelea kuliangamiza taifa milele
Mbili: Leo hii ukiwa mfanyabiashara mkubwa au ni innovative mkubwa sana basi utapigwa vita hadi na mwenyekiti wako wa mtaa. Chukulia suala rahisi tu Waziri anapopiga domo na kushangilia shirika la ndege kufa hii sio shirika linapigwa mkuki bali ni mtu binafsi na ubinafsi wake ya kuwa hawezi kuendesha shirika la ndege (What if tungempa masharti ya kuimarisha huduma)
Tatu: Matajiri wataishi kama mashetani. Hii ni kauli fupi ila ni nzito sana hasa katika karne hii 21 ya ushindani wa kiuchumi na technologia.
Nne: Hatuthamini kabisa katika uwezo wetu wa kufikiri ni hii ni sifa ya ujamaa uliotukuka (mediocriticy thinking). Yaani ukizalisha bidhaa Tanzania mathalani Toilet paper hamna mtu ataamini kama ni bora hii ni kuanzia mchambaji mpaka taasisi zinazoshughulikia ubora (shame on us)
Tano: Mimi ni mtetezi wa masikini. OK sawa ni Taifa la masikini na tutaendelea kuwatetea
Sita: Ujamaa hauamini katika Innovation kabisa mathalani mtanzania akagundua gari la kutumia maji badala ya mafuta utapigwa mawe mpaka usahau njia ya kutokea. Ila wenye mifumo tofauti huchukua wanampa wabobezi kusaidia ugundua na kuitumia technologia hiyo. NB. Wakati nakua kulikuwa na kijana mmoja mtaani alikuwa fundi sana wa kutengeneza magobole ya uwindaji na alifika level ya kuweka lisasi mpaka saba at once. Ila alifungwa miaka 30 jela nadhan sasa yuko nusu ya kifungo chake (Hii ndio Tanzania).
Saba na Mwisho. Tunaimani ya kuwa kila kitu kitajiweka sawa bila jitihada. Yaani hapa ndio tatizo kubwa sana lilipo. Utasikia tunataka kufikia middle income country ukiuuliza kwa sela zipi utaishiwa kukenuliwa meno na wazungumzaji.

NB. Sera ya Ujamaa ambayo bado inakumbatiwa na baadhi ya vyama vya siasa ni mwiba mkubwa wa maendeleo Tanzania. #Attitudemustchage#
 
Huu uzi umejaa madini sana, ni jambo gumu sana dunia ya leo ukataka uendeshe nchi yako kijamaa wakati unategemea mikopo na hisani za mabepari. Ajabu ni kwamba kila mtu anayeonekana kuja na wazo mbadala anachukuliwa kuwa ni muahini..

Najua tutafika tunapotaka ila itachukua muda sana. Vizazi kwa vizazi.
 
Pamoja na mengi mazuri yalifanywa na serikali ya awamu ya kwanza lazima tukubali ujamaa ilikuwa ni KOSA LA KIUFUNDI KABISA. Naaandika haya kwa kuzingatia kuwa ukiisema serikali ya awamu ya kwanza kwa mabaya yake basi wewe si mzalendo (Niko tayari kwa hilo).
Mosi. Wakati wa kampeni liliibuka suala la mtu ukiwa tajiri huwezi kuwa raisi wa Tanzania ukiuliza sababu utaendelea kuambiwa atauza nchi au amepata utajiri kwa rushwa. Hili litaendelea kuliangamiza taifa milele
Mbili: Leo hii ukiwa mfanyabiashara mkubwa au ni innovative mkubwa sana basi utapigwa vita hadi na mwenyekiti wako wa mtaa. Chukulia suala rahisi tu Waziri anapopiga domo na kushangilia shirika la ndege kufa hii sio shirika linapigwa mkuki bali ni mtu binafsi na ubinafsi wake ya kuwa hawezi kuendesha shirika la ndege (What if tungempa masharti ya kuimarisha huduma)
Tatu: Matajiri wataishi kama mashetani. Hii ni kauli fupi ila ni nzito sana hasa katika karne hii 21 ya ushindani wa kiuchumi na technologia.
Nne: Hatuthamini kabisa katika uwezo wetu wa kufikiri ni hii ni sifa ya ujamaa uliotukuka (mediocriticy thinking). Yaani ukizalisha bidhaa Tanzania mathalani Toilet paper hamna mtu ataamini kama ni bora hii ni kuanzia mchambaji mpaka taasisi zinazoshughulikia ubora (shame on us)
Tano: Mimi ni mtetezi wa masikini. OK sawa ni Taifa la masikini na tutaendelea kuwatetea
Sita: Ujamaa hauamini katika Innovation kabisa mathalani mtanzania akagundua gari la kutumia maji badala ya mafuta utapigwa mawe mpaka usahau njia ya kutokea. Ila wenye mifumo tofauti huchukua wanampa wabobezi kusaidia ugundua na kuitumia technologia hiyo. NB. Wakati nakua kulikuwa na kijana mmoja mtaani alikuwa fundi sana wa kutengeneza magobole ya uwindaji na alifika level ya kuweka lisasi mpaka saba at once. Ila alifungwa miaka 30 jela nadhan sasa yuko nusu ya kifungo chake (Hii ndio Tanzania).
Saba na Mwisho. Tunaimani ya kuwa kila kitu kitajiweka sawa bila jitihada. Yaani hapa ndio tatizo kubwa sana lilipo. Utasikia tunataka kufikia middle income country ukiuuliza kwa sela zipi utaishiwa kukenuliwa meno na wazungumzaji.

NB. Sera ya Ujamaa ambayo bado inakumbatiwa na baadhi ya vyama vya siasa ni mwiba mkubwa wa maendeleo Tanzania. #Attitudemustchage#
Njoo JULAWATA/Jukwaa la Wajamaa Tanzania kila jumamosi survey Dsm kwenye darasa la itikadi!.
 
Asante mkuu lakini kama ni jukwaa tu la midahalo bila kuwa na impact kwenye uchumi na taifa sidhani kama linamanufaa na halitanifaa.
 
Back
Top Bottom