Madhara ya Sukari kwa binadamu


Asante sana Dr. MziziMkavu,
Kwa hakika matumizi ya asali nayakubali na huwa ninatumia japo si kila wakati (si unajua tena sisi ambao tumefikia saa 10 jioni). Je kwa wanawake haisaidi katika kuongeza nguvu ya yale mambo ya wakubwa? maana na wao si unajua tena wakifikia 40s wanaanza ile law of diminishing return!!! Au kuna njia nyingine natural kwa wanawake? Angalao kwa mamen inakuwa ni kama nuts, asali, etc.
 
Hakuna utafiti uliobainisha kwamba Sukari inasababisha diabetes. Ila mtu mwenye diabetes ndiye anashauriwa apunguze au asitumie kabisa sukari kwa sababu mwili wake hauna uwezo wa kuitumia. kwa hakika ,Sukari ina manufaa mengi kwa mwili wa binadamu ikitumiwa in moderation.
 
Mkuu.@Zogwle Kuamsha tamaa ya kiume au kike

Juisi ya tangawizi nusu kijiko pamoja na yai nusu iliochemshwa na asali. Tumia kila siku kwa muda wa mwezi mmoja.​
 
Achane kuwatisha watu! maisha ni mafupi just enjoy life!

Mimi napiga Kilimanjaro larger 5 kila weekends... ila pia napiga tizi la kufa mtu..pia nakunywa sana maji mengi. sina tumbo ni misuli tu!

Just enjoy life!
 
As Usual respect to U.....
Tunaomba na madhara ya chumvi nayo utuletee mkuu. Siku njema....
 
Kweli mkuu, kwakweli nakula sukari nyingi, pia vyakula kama ugali wali ukichanganya na ngano kimiminika, duuu manake sasa nina kilo nyingi, na juzi nilipiga jalamba kidogo nahema kama tractor yenye miss, hata nanilii ...... mi nilidhani labda umri manake nimepita wastani wa MTz kuishi! Hiyo itakuwa mishuga tu, waganga wangu wa kienyeji hawajawi nipa somo hili, naenda fukuza wote! Thanks mkuu kwa shule hii, ngoja nipunguza ili walau nanii... nirudishe heshma..
 
As Usual respect to U.....
Tunaomba na madhara ya chumvi nayo utuletee mkuu. Siku njema....

Chumvi huleta high blood pressure.Kidney huondoa unwanted fluid kwa kufilta damu na hili tendo hufanyika by delicate balance of sodium na other mineral salt-osmosis.ukila chumv nying kidney itashindwa kuondoa extra fluid na kuwa mkojo instead fluid itabuild up resulting into high blood pressure.ii pressure italeta matatizo kwenye kidney,arteries,heart and brain.kwa iyo magonjwa kama kidney failure,narrowness of artery,dementia e.t.c.Huo ndo uelewa wangu mheshimiwa
 
Sukari ni mojawapo ya kirutubisho ambacho hutumiwa na watu wengi sana. Kama neno lenyewe lilivyo SUKARI likimaanisha UTAMU... ni kiungo kinacholeta ladha ya Utamu pale kinapotumiwa katika baadhi ya vyakula.

Lakini katika utamu ule ule tunaoupata tunapoitumia sukari matokeo yake yanaweza kuwa kinyume cha huo utamu na ukawa MCHUNGU sana.

Kama wataalamu wa afya wanavyosema Sukari inaweza kusababisha ugonjwa wa Kisukari pale inapozidi sana mwilini. Ugonjwa wa Kisukari ni ugonjwa hatari kama yalivyo magonjwa mengine yanayoofanya mwili kudhoofu sana na hivyo mtu aweza kupoteza maisha kabla ya muda wake.

Watu wengi wanafikiri kuwa labda sukari ya kawaida haiwezi kusababisha ugonjwa wa kisukari lakini nikuhakikisheni pale utakapotumia sukari nyingi na kongosho yako ikashindwa kuitoa sukari hii katika damu na kuihifadhi katika mwili katika mfumo tofauti lazima ugonjwa huu uupate tu.

Ni vyema kama kupunguza kabisa au kuacha kabisa kutumia sukari na vitu vyenye asili ya sukari nyingi ili kuujenga mwili kuwa katika hali ya afya njema zaidi.

Kwa hiyo watanzania wenzangu tusitishike sana na mafisadi kwamba wanaficha sukari ili kutunyonya. Hii ni katika mpango wa Mungu tu kutuweka katika afya njema zaidi.

Tuziweke afya zetu kuwa imara kwa kupunguza kutumia sukari. Niwahakikishie tukiacha kutumia sukari hiyo mizigo waliyojaza kwenye magodown itawaozea maana demand itakuwa ni ndogo sana. Watatafuta hata wa kuwagawia bure hawatapata.

Tuzipende afya zetu na tuwape heko mafisadi wanaofikiri kwa kubana sukari kwenye magondown wanamkomoa Mtanzania kumbe ndo wengine tutaimarisha afya zetu.

Siyo lazima kutumia sukari, ujumbe uwafikie.
 
Vema kabisa mkuu,sukari sio kitu cha lazima kwetu. Mi nashangaa hii kuwa ajenda wakati wengi huko vjijini wanatumia chumvi kama mbadala wa sukari,kama vile kwenye uji.
 
Vema kabisa mkuu,sukari sio kitu cha lazima kwetu. Mi nashangaa hii kuwa ajenda wakati wengi huko vjijini wanatumia chumvi kama mbadala wa sukari,kama vile kwenye uji.
Ni kijiji gani unachokiongelea mkuu,isije ikawa unaongelea mabwe pande?
 
Vema kabisa mkuu,sukari sio kitu cha lazima kwetu. Mi nashangaa hii kuwa ajenda wakati wengi huko vjijini wanatumia chumvi kama mbadala wa sukari,kama vile kwenye uji.

Wanasiasa na mafisadi wanataka kutuaminisha kuwa ni kitu muhimu sana kwamba ukiikosa utakufa. Sukari mbona ipo hata ukila ugali tu sukari inayohitajika na mwili mtu ataipata tu.

Kuishi na kuwa na afya njema siyo lazima kutumia cane sugar. Tusitishwe yapo muhimu ya kujadili siyo sukari.
 
Ni kijiji gani unachokiongelea mkuu,isije ikawa unaongelea mabwe pande?

Kwani mkuu wee unaamini kwamba bila sukari ya miwa huweza kuishi? Hiyo tu ndo inakufanya upumue? Ukinywa uji bila hata kuweka chumvi au hiyo sukari miwa mwili haupati sukari yake kama kawaida?
 
Kwani mkuu wee unaamini kwamba bila sukari ya miwa huweza kuishi? Hiyo tu ndo inakufanya upumue? Ukinywa uji bila hata kuweka chumvi au hiyo sukari miwa mwili haupati sukari yake kama kawaida?
Hizo ni sababu mufilisi kabisa tafuta utetezi mwingine huu bado haukidhi
 
mkuu kwavile nyie mna uwezo wa kunywa juice asubui mkazani wote wako hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…