Madhara ya Sukari kwa binadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madhara ya Sukari kwa binadamu

Discussion in 'JF Doctor' started by Chocolate, Mar 18, 2009.

 1. Chocolate

  Chocolate Senior Member

  #1
  Mar 18, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33


  Japo nafahamu kwamba zote zina madhara katika mwili wa mwanadamu, Je kuna ufafanuzi wa kidaktari/kitaalamu kati ya kutumia sukari nyeupe na sukari ya brown? Ni ipi ina madhara zaidi?
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  U  Wote tunakubaliana kwamba sukari ni tamu na ni miongoni mwa bidhaa zinazotumika kwa wingi kila siku. Pamoja na umuhimu wake, lakini ni hatari kwa ustawi wa afya pale inapotumiwa kwa wingi kupita kiasi.

  Kwa kawaida kiwango cha sukari tunachotakiwa kutumika katika vinywaji vyetu, iwe chai, juisi, na vinginevyo, ni kiasi kidogo sana. Kwa upande mwingine, unapoweka sukari kiasi kidogo, ladha ya kinywaji au chakula hicho huonekana kama haijakamilika.

  Katika kutafuta ladha ya sukari iliyokolea, baadhi ya watu hupenda kuweka kiasi kingi cha sukari kwenye vinywaji na vyakula vyao na matokeo yake hujikuta katika matatizo mengine makubwa ya kiafya bila wao kujua kuwa chanzo ni sukari.

  Madhara yatokanayo na kupenda sana kula kiasi kikubwa cha sukari ni mengi, baadhi yake ni pamoja na kudhoofika kwa mfumo wa kinga ya mwili (Immunity System), kudhoofika kwa viungo vya mwili, kudhoofika kwa ngozi, kusababisha unene wa kupindukia, n.k.

  KIASI KINGI NI KIPI?
  Bila shaka unaweza kujiuliza kiasi kingi cha sukari ni kipi? Mazoea yanaonesha kuwa watu wengi huweka sukari kwenye kikombe kimoja cha chai wastani wa vijiko vitatu hadi vinne kama kiwango chao cha kawaida, kiwango ambacho ni kingi mara nne ya kile kinachokubalika.

  Wastani unaotakiwa kuwekwa kwenye kikombe kimoja cha chai ni kijiko kidogo kisichozidi kimoja na hata ikiwezekana pungufu ya hapo. Vilevile inashauriwa kujiepusha sana na unywaji wa vinywaji, kama juisi na soda ambavyo huongezewa sukari ya ziada.

  Tunaelezwa kwamba chupa moja ya soda huwa na wastani wa vijiko sita vya sukari, kiasi ambacho ni kikubwa kuliko kawaida. Hivyo ni vyema kujiepusha na unywaji wa soda wa kupindukia ukidhani unakunywa kinywaji salama kwa kuwa hakina kilevi.


  TUNAWEZA KWELI KUIEPUKA KABISA SUKARI?
  Ni dhahiri kwamba hatuwezi kuepuka kabisa matumizi ya sukari na kuiondoa katika milo yetu ya kila siku, lakini uelewa wa madhara yake na dhamira ya kuiepuka inaweza kumsaidia mtu kupunguza kiwango anachotumia kwa siku. Zifuatazo ni baadhi ya dondoo zinazoweza kukusaidia kupunguza matumizi ya sukari:

  Anza kuweka mazoea ya kusoma kiasi cha sukari kilichomo kwenye chakula au kinywaji unachokunywa. Mara nyingi kiasi cha sukari kinachowekwa kwenye kinywaji huoneshwa kwa gramu, ambapo kijiko kimoja kidogo cha sukari ni sawa na gramu 4. Hivyo ina maana kwamba iwapo kinywaji au chakula unachokula kina gramu 16 za sukari, hiyo ni sawa na vijiko vidogo vinne.

  Kuwa makini na chunguza kwa karibu, kwani vinywaji vingine havioneshi jina la sukari moja kwa moja, badala yake huita kwa majina kama vile ‘high fructose’, ‘molasses’, ‘dextrose’, n.k, hiyo yote ni sukari.

  Aidha, ili kupunguza makali ya sukari, kunywa kiasi kingi cha maji kila siku, epuka unywaji wa pombe wa kupindukia na pata muda wa kupumzika au kulala usingizi wa kutosha.

  KINGA YA MWILI
  Kama tujuavyo, kinga ya mwili ni silaha ya asili ya mwili ya kupambana na maambukizi yoyote yanayosababishwa na bakteria, virusi na parasaiti wengine. Ili kuwa na kinga ya mwili ya uhakika, ni muhimu sana kuimarisha kinga hiyo kwa kula vyakula vyenye virutubisho na kujiepusha na ulaji wa vyakula kama sukari ambayo inaathiri mfumo mzima wa kinga ya mwili.

  Kuna ushahidi wa kutosha wa kisayansi kuwa matumizi ya sukari huathiri mfumo wa kinga ya mwili. Seli nyeupe za damu (white blood cells) ndizo seli zinazoimarisha mfumo wa kinga ya mwili, lakini kiasi kikubwa cha sukari kinapoingia kwenye mishipa ya damu, hudhoofisha uwezo wa seli hizo kupambana na bakteria na virusi wanaoweza kuvamia mwili.

  Kwa kuzingatia kuwa kinga ya mwili ndiyo msingi wa afya ya binadamu, ni vizuri kujiepusha na matumizi ya vyakula vinavyohatarisha kinga zetu. Lazima ujiulize kama matumizi yako ya sukari ni ya kiwango cha kawaida ama ni ya kuhatarisha afya yako, kama yanahatarisha afya yako, chukua hatua ya kupunguza matumizi yake haraka kabla hujachelewa.
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Thanks Dr MziziMkavu (Naturopathic Physician)
   
 4. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  asante sana na ubarikiwe mkuu
   
 5. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  asante MziziMkavu kwa elimu unayotoa hapa jamvini
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  @ Blaki Womani Asante na wewe Ubarikiwe mbinguni..........
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  @CUTE na wewe pia Ubarikiwe mbinguni.....
   
 8. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu, itatusaidia wengi
   
 9. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  asali ni mbadala mzuri wa sukari kusema kweli.
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,852
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu ni kweli kabisa kuwa sukari inaleta magonjwa mengi ingawa inahitajika mwilini pia. pia kuna ishu ambayo huwa naiona iko siielewi vizur juu ya hii sukari, nijuavyo ikiingia mwilini huwa simple sugar and not complex as we are taking it. sugar environment is a conducive environment for bacteria growth an fungi. For that matter huwa najiulizaga if blood sample contais a lot of sugar whow does antigen survive? na je ni kwasababu tu mwili uko starile kwa kias kikubwa lakin pia over occurance ya bacteriological and fungal diseases huwa nazi associate na hili je niko sahihi au la. Mimi siyo dr but ni mwalim tu so ukiniambia hili utanisaidia sana katika ufundishaji wangu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Asante mkuu kwa elimu hyo.
   
 12. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante kaka.
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  U

  WENGI wetu tumeshasikia ushauri wa kula sukari kidogo – ushauri ambao ni mzuri kiafya. Lakini licha ya tahadhari mbalimbali zinazotolewa na wataalamu wa afya kuhusu madhara yatokanayo na ulaji mwingi wa sukari, bado idadi kubwa ya watu hupenda kutumia sukari kwa wingi kwa njia mbalimbali.

  Utumiaji wa sukari siyo lazima ile sukari nyeupe (white) au kahawia (brown) pekee, bali pia hata sukari asilia inayopatikana kwenye matunda, maziwa, asali, vinywaji baridi, pombe, baadhi ya nafaka, n.k. Hizo zote ni aina za sukari ambazo zinatofautiana faida na madhara.

  Wakati viwanda vya uzalishaji sukari duniani vinaongezeka, tatizo la unene kupita kiasi kwa binadamu nalo linaendelea kuongezeka. Sukari inahusika kwa kiasi kikubwa na tatizo la kuongezeka kwa unene wa kupindukia (obesity). Kwa watu wanene, ulaji wa sukari hata kijiko kimoja tu

  kwa siku, huchangia kwenye tatizo. Sukari ni ya kuepukwa, siyo tu kwa watu wanene, bali hata kwa watu wengine wenye kujali afya zao.
  Katika kitabu chake kiitwacho LICK THE SUGAR HABIT, mwanalishe Nancy Appleton (PhD), ameelezea sababu 146 za kwa nini sukari hudhoofisha afya zetu, zifuatazo ni baadhi ya sababu hizo:

  - Sukari huweza kuathiri ukuaji wa homoni mwilini (kitu ambacho ni muhimu kwa kumfanya mtu kuishi na afya njema wakati wote).
  - Sukari ndiyo chakula cha saratani mwilini
  Sukari huongeza lehemu mwilini (cholesterol)
  - Sukari huweza kusababisha kizunguzungu na kudhoofisha mwili kwa watoto
  - Sukari huweza kudhoofisha nguvu ya macho
  - Sukari huweza kuzuia utembeaji wa protini mwilini
  - Sukari huweza kusababisha mzio wa chakula (food allergies)
  - Sukari huchangia ugonjwa wa kisukari
  - Sukari huweza kusababisha ugonjwa wa moyo
  - Sukari huweza kuharibu umbo la vinasaba vya mwili (DNA)
  - Sukari huweza kusababisha utukutu, utundu na kukosa umakini kwa watoto
  - Sukari huweza kuchangia kupunguza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yatokanayo na wadudu aina ya bakteria (infectious diseases).

  Hizo ni baadhi tu ya hizo sababu 146. Je, kwa kujua sababu zote zilizothibitishwa kuhusu madhara yatokanayo na sukari, kuna sababu gani ya kuendelea kupenda kutumia sukari? Kitu kizuri pekee kuhusu sukari ni kwamba kina ladha tamu na tunapokula, tunajisikia raha. Hapa ndipo pahali panahitaji kuangaliwa kwa makini.

  Kiasilia, mwanadamu ana ladha sita tofauti, zikiwemo za uchungu, utamu, ukali, ukakasi. Hivyo kuacha kabisa ulaji wa ladha tamu kunaweza kusababisha madhara mengine ya kibaiolojia na ndiyo maana watu wengi hushindwa kujizuia kutumia sukari, hasa kwa watoto ambao kwao huonekana ni jambo lisilowezekana kabisa kuacha kulamba sukari.

  Hata hivyo, kuna habari njema kuwa unaweza kutumia mbadala wa sukari na kupata ladha ya utamu katika vinywaji au vyakula vyako bila kuwa na madhara. Moja ya mbadala wa sukari anayeaminika na wengi tangu enzi na enzi, ni asali, ambayo unaweza kuitumia kwenye vinywaji mbalimbali bila kuwa na madhara.

  Hata hivyo, baadahi ya wataalamu wanasema kuwa kwa kuwa asali nayo ina ‘fructose’, huenda ikawa na mdhara pia, ingawa kwenye vitabu vya dini na baadhi ya wanasayansi wameielezea asali kama kitu kisicho na madhara mwilini licha yakuwa nayo ni tamu kama sukari.

  Baadahi ya wanasayansi wamependekeza zaidi mbadala wa sukari kuwa ni ‘Stevia’ na ‘Xylitol’, ambavyo vinatokana na mimea na majani lakini vina ladha ya utamu kuliko hata sukari. ‘Stevia’ na ‘Xylitol’ hutumika zaidi katika nchi za Ulaya,

  Japan na Amerika ya Kusini, kwetu Afrika hazijulikani sana na sidhani kama zipo.
  Jambo la msingi ni kujua kwamba sukari tunaipenda, lakini siyo chakula kizuri kama tunavyoweza kudhani, hivyo tujitahidi kuiepuka kadri tunavyoweza kwa kutumia mbadala kama asali, pale tunaposhindwa kabisa kuiepuka, basi tutumie kwa uchache sana.
   
 14. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2013
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ahsante Mkuu niklikuwa napenda sana sasa nimestuka na naacha rasmi,WABHEJASANA NYANDA!
   
 15. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2013
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,523
  Trophy Points: 280
  Mzizi mkavu ubarikiwe
   
 16. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2013
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  nilikuwa nchi china, huwezi amini chai yao hawaweki sukari kabisa lakini ukienda mgeni wanakuwekea sukari pembeni ujinyonge mwenyewe, nilipo wauliza wakaniambia angalia miili ya watu wetu halafu uangalie na miili yenu baada ya kuangalia nikapata jibu kuwa sukari sumu na inachangia vifo vingi sana kwa upande wa unene na uzito kupindukia..tangu hapo nimepunguza utumiaji wa sukari kwa kiwango kikubwa saa kwanza unywaj wa da nimeig chini chai naweka kijiko moja tu..
   
 17. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #17
  Jan 23, 2013
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  I wish elimu hii ingewafikia watu wengi zaidi...
   
 18. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2013
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Picha nzuri hiyo ya kijiko cha sukari mpaka natamani kulamba
   
 19. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2013
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Daktari wangu MziziMkavu umetoa angalizo zuri sana kwa matumizi ya sukari na athari zetu mwilini. Ninapenda kama unaweza kutupa dondoo kwa madhara ya sukari kwa matumizi ya asali. Sote tunajua kuwa asali inakuja kwa kasi sana katika matumizi ya kubibu magonjwa mbalimbali na kirutubisho pia. Sasa sukari ya asali haina madhara kwa hayo uliyoorodhesha hapo juu? Japo kweli tunajua asali inatokana na natural pollen sugar, etc but whati can we say my Dr?
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Mkuu Zogwale Sukari ina madhara lakini

  Asali haina madhara sukari iliyoko ndani ya Asali ni Natural Pollen sugar haina Madhara kwa binadamu ni Dawa

  na ni Tiba kwa Afya ya Binadamu hata kama utakuw unakunywa kila siku Asali haita kudhuru sana itakuongezea nguvu za kiume katika mwili wako na kukutibu baadhi ya magonjwa yaliko mwilini mwako. Hizi hapa chini ni baadhi ya Faida ya kutumia asali.

  Asali ina manufaa mengi mojawapo ikiwa ni kusaidia kupunguza uzito. Mtumiaji huweka kijiko kikubwa kimoja ndani ya maji ya moto na kunywa kila siku asubuhi. Hii pia humsaidia kupunguza kitambi.


  Pili, asali husaidia kutibu vidonda vya tumbo. Mtumiaji anaweza kunywa kijiko kikubwa kimoja asubuhi, mchana na jioni. Kama hiyo haitoshi, asali pia - hasa ile ya nyuki wadogo - wakubwahusaidia kutibu kikohozi kwa watoto na.Wakubwa.

  Wakati mwingine baadhi ya watumiaji huchanganya na kiini cha yai na kutengeneza mkorogo unaonyeshwa watoto. Kumbuka kuwa ni vema mkorogo huo ukatumika siku hiyo hiyo.

  Pamoja na matumizi hayo, asali pia husaidia pale inapotokea mtu ameungua kwa moto. Basi ni vema ikapakwa mara moja wakati mgonjwa akielekea hospitali kwa matibabu zaidi. Waweza pia kupaka na yai bichi lililovunjwa kama unalo.

  Kwa ndugu zangu akina dada na akina mama, asali pia hutumika kwa ajili ya kufanyia steaming ya nywele. Ukienda nayo saloon wataalamu watakusaidia bila kusahau kuongeza mng’aro wa ngozi ya mtumiaji iwapo anatumia.

  Labda niseme kuwa katika nyakati za hivi karibuni kumekuwa na tatizo sana la kisukari linaloathiri nguvukazi ya taifa. Tatizo hili

  pia linaweza kuepukwa kwa kiwango fulani kwa mtumiaji wa chai na kahawa, kuweka asali badala ya sukari katika vinywaji hivyo.


  Vile vile badala ya kupaka jamu kwenye mkate, kwa wenzangu wenye shida ya uzito mkubwa waweza kuweka

  asali. Kumbuka si tu utaburudika bali pia unatibu shida za kiafya. Ikumbukwe kuwa matumizi makubwa ya sukari hayana tija sana kwa mwili, hivyo ni bora kukinga kuliko tiba kwa sababu ni ghali.

  Hivyo basi, ni vema wanafamilia mkajitahidi kuhakikisha kuwa mnakaa na asali nyumbani kama huduma ya kwanza. Asali inayopatikana katika maduka mbalimbali au katika vibanda maalumu vya uuzaji asali pia inafaa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...