Madhara ya kung'oa jino gego la juu

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,658
2,804
hodi,wataalamu,naomba kujuzwa kama kuna madhara yeyote ya kung'oa jino gego la juu,maana nimekuwa nikisikia dhana mbalimbali juu ya watu kupoteza maisha na maradhi mengine ya kichwa ,wanaosema hivyo wanadai kuwa meno ya juu yameshikamana na mishipa mingi ya fahamu.

Hivyo wadau naomba kujuzwa kama kuna madhara yeyote yale ,na kama hamna basi naomba kujuzwa hospitali yenye wabobezi wazuri wa tiba ya meno na kinywa ili nikang'oe hili jino.

asante.
 
Kama unaishi dar, mwenge africasana kuna hospitali inaitwa holistic ni wataalam wa tiba ya meno, niling'oa jino la juu na sikupata madhara yoyote
 
hodi,wataalamu,naomba kujuzwa kama kuna madhara yeyote ya kung'oa jino gego la juu,maana nimekuwa nikisikia dhana mbalimbali juu ya watu kupoteza maisha na maradhi mengine ya kichwa ,wanaosema hivyo wanadai kuwa meno ya juu yameshikamana na mishipa mingi ya fahamu.

Hivyo wadau naomba kujuzwa kama kuna madhara yeyote yale ,na kama hamna basi naomba kujuzwa hospitali yenye wabobezi wazuri wa tiba ya meno na kinywa ili nikang'oe hili jino.

asante.
Mkuu niliponea chupu chupu kufa usifanye mchezo na gego la juu ,nikumbuka mwaka 2007 sitashau kamwe,Kuna mishipa mingi ya jino kwenda kichwani ,nenda Hospital makini ,usaha ulikua unatoka kwenye gego na pua ya kushoto itoboka ,na nilipotolewa jino niilipewa antibiotics na sikuwahi kuacha kumeza lakini kilichotokea Basi tu sitakisahau kamwe!
 
duh,mbona wanitisha ndugu?
 
na gego la chini halina tatizo kama uking'oa?? Na vipi kuhusu jino kukua kumwelekea mwenzake na sio kuelekea juu ambayo inapelekea kusukumwa kwa jino linaloelekewa (impaction)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom