Madereva wa Masafa marefu: Changamoto mbalimbali tunazokutana nazo barabarani Usiku

hosh kosh

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
748
572
Habar za weekend wakuu?

Haka ka uzi bana naongelea kuhusu safari za usiku kwa madereva wa magar aina zote, wanaopenda kusafiri usiku.

Binafsi wakuu, najihusisha na vishughuli vyangu hasa mkoani kwahiyo muda mwingi huwa na kuwa ktk pilika zangu mkoani, so huwa napenda kusafiri sana usiku na mpaka sasa nina uzoefu wa kama miaka 4 hivi ktk safar zangu za usiku.

Sababu za kupenda kutembea usiku ni huwa sipendi karaha na bugudha za mchana hasa usumbufu wa askari, msongamano wa magari mchana, pia na hali ya hewa kidogo hasa kuanzia Dar mpaka unakaribia kuingia mkoa wa Iringa na njia yangu kuu ni Iringa road...

Hal ya hewa ikiwa jua na joto, safari kwangu inakuwa ngumu sana.

Sasa katika baadhi ya kero nilizokutana nazo au nakutana nazo bhn kwanza magar makubwa yanaudhi sana:

1. Kutembea katikati mwa barabara usiku
Hili huwa linanikwaza sana hasa kwa sababu ni hatar sana hasa ktk kona kali au sehemu hatari kama ukiwa ktk spidi kali unaweza ukalivaa na ikawa hatari zaidi.

2. Uwashaji wa full light ovyo ovyo
Utakuta mnapishana lkn mwenzako bado kawasha full light za chin za juu mpaka inabidi sometimes unalazimika kusimama pembeni ili apite. Sasa hili linaudhi kwa baadhi ya madereva wasiojua sheria za barabarani.

Na ziko nyingi.

Wakuu, ukiacha hizo nyingine ni za kishirikina! Naamini hivyo sababu unakutana na mbuzi au kondoo barabarani kwa mbali, ukiwakaribia huwaoni. So, changamoto za udereva wa usiku kama hizo..

Vipi kwako dereva mwenzangu wa safari za usiku unakutanana changamoto zipi au kero zipi?
 
Mkuu:
Mara nyingi madereva wanao safiri usiku huwa wanachoka sana, uzoefu unaonyesha kuwa mchana hawapati muda wa kupumzika.

Sheria tulizorithi ni kuwa dereva asiendeshe gari kwa zaidi ya saa 8 mfululizo. Hivyo anatakiwa kupumzika si chini ya masaa sita.
 
Binafsi nasafiri usiku ikibidi tu, maana inahitaji umakini sana hasa kunapokuwa na magari mabovu njiani yasiyokuwa na alama za tahadhari.
da kwel mkuu magara mabovu barabaran yanaboa sana afu ata alama awawek za triangle wao wanaweka majan sa kwa mbal inakuwa shida kugundua mara moja unakuta.hata gar liliobovu ht ule mkanda wa reflects hauna.ni hatari
 
Mkuu:
Mara nyingi madereva wanao safiri usiku huwa wanachoka sana, uzoefu unaonyesha kuwa mchana hawapati muda wa kupumzika.

Sheria tulizorithi ni kuwa dereva asiendeshe gari kwa zaidi ya saa 8 mfululizo. Hivyo anatakiwa kupumzika si chini ya masaa sita.
mkuu iyo labda kwa madereva wa malor lkn kwa sisi wa private huwa swafi kbsa..usik ni raha sana kusafir kwanza kuna utulivu sana so kuchoka ni kwa kawaida nahasa umefika safar yko.
 
safari ya usiku kwangu inakuwaga kama mchana, ukipata tatizo ndio issue otherwise hakuna usumbufu wa tochi, pia si rahisi kupata ajari zinazosababishwa na over taking maana taa zitakushtua.
sema kuna mapori yanatakaga moyo kuyachana usiku, pamoja na yote nishapita kondoa dodoma night kali, ifakara mlimba night kali, kigoma mwanza via tabora night kali, moro dar hazihesabiki, mtwara dar hazihesabiki, kiufupi napenda sana safiri usiku.
sekeseke lilinikuta siku moja engine ilinock vijiji vitatu baada ya mto wami...sitosahau.
 
Ni wapi hiyo mkuu? mi kuna siku naenda dodoma tokea dar sa nane usiku pale karibu na kibaigwa nikaona mbuzi katikati ya barabara nikawagonga na hakuna kilichotokea mpaka nafika
aah vp mkuu baada ya kuwagonga uligeuka kuangalia km wapo barabarani..km uliwaona bac ni mbuz kwel ila km hukuona kitu ndo majin yenyewe hayo mkuu..mi huwa napishana nayo sana lkn huww nayaona kwambal nikisogelea kwa karib huoni na hujigeuza maumbile ya wanyama mara nying.
 
Mamba 2 ni tatizo sana kwa barabara ya tdm -dar
Usiku hakuna usumbufu wa trafiki kwa barabara ulioitaja ispokuwa pale chek point ya iringa na mikumi kidogo,pia jama una private car/ gari ndoho taixo hakuna idpokuwa madere wa malori wanawasha taaf full ambayo uleta usumbufu,
Hatari kwa wenye magari ya mizigo ,mafuta na transt goods kwani kunakuwaga na wizi unapopanda milima mikali kama kitonga, mlima nyoka, inyara, senjele na vaadhi ya maeneo kwa road ya tdm-Dar
Kwa private car chukua taadhali dhid ya utekaji na kusinzia.
 
safari ya usiku kwangu inakuwaga kama mchana, ukipata tatizo ndio issue otherwise hakuna usumbufu wa tochi, pia si rahisi kupata ajari zinazosababishwa na over taking maana taa zitakushtua.
sema kuna mapori yanatakaga moyo kuyachana usiku, pamoja na yote nishapita kondoa dodoma night kali, ifakara mlimba night kali, kigoma mwanza via tabora night kali, moro dar hazihesabiki, mtwara dar hazihesabiki, kiufupi napenda sana safiri usiku.
sekeseke lilinikuta siku moja engine ilinock vijiji vitatu baada ya mto wami...sitosahau.
du pole sana mkuu ..ilikuwaje iyo kasheshe..pia ni kwel mkuu usumbufu night hmna..na unahitaji.gar nzur pia..ila iyo roada ya mikumi tu ifakara (ifoza wanaita wenyewe) ni hatar sabb roadni rough tu hmna lami..lami kuanza mikumi mpk ruaha na seheme inaitwa kiberegemkuu ndo kirami kidogo ..ila kwingne ni hatari road lake..pia bhn ushaenda njia ya irinda roada km unaenda mbeya au songea.ebhh ulee msitu wa sao hill ni hataari km huna moyo uwez tembea kabsa bhn..
 
aah vp mkuu baada ya kuwagonga uligeuka kuangalia km wapo barabarani..km uliwaona bac ni mbuz kwel ila km hukuona kitu ndo majin yenyewe hayo mkuu..mi huwa napishana nayo sana lkn huww nayaona kwambal nikisogelea kwa karib huoni na hujigeuza maumbile ya wanyama mara nying.
Sikugeuka nyuma baada ya hapo ila cha ajabu ni kwamba sikuskia kama nimewagonga mana niliwaona kwa mbali mpaka nawakaribia na nikawagonga lakin sikuskia mshindo, ila mkuu mi haikuwa mara yangu ya kwanza kusafiri usiku na hizi stori nimekua nikiziskia kitambo tu
 
safari ya usiku kwangu inakuwaga kama mchana, ukipata tatizo ndio issue otherwise hakuna usumbufu wa tochi, pia si rahisi kupata ajari zinazosababishwa na over taking maana taa zitakushtua.
sema kuna mapori yanatakaga moyo kuyachana usiku, pamoja na yote nishapita kondoa dodoma night kali, ifakara mlimba night kali, kigoma mwanza via tabora night kali, moro dar hazihesabiki, mtwara dar hazihesabiki, kiufupi napenda sana safiri usiku.
sekeseke lilinikuta siku moja engine ilinock vijiji vitatu baada ya mto wami...sitosahau.
pia njia ya dom mkuu nishaenda mpwapwa kupitia kongwa unaingilia mbande..dah kule hatare mkuu kuna mibuyu mwanzo mwisho kelele za ajabu hatari yaan bila kufunga vioo huendeshi gar yan..
 
Sikugeuka nyuma baada ya hapo ila cha ajabu ni kwamba sikuskia kama nimewagonga mana niliwaona kwa mbali mpaka nawakaribia na nikawagonga lakin sikuskia mshindo, ila mkuu mi haikuwa mara yangu ya kwanza kusafiri usiku na hizi stori nimekua nikiziskia kitambo tu
duh..mkuu hyo bhn ni majin km hukusikia mshindo wwte.sabb majin yanasifa ya kujibadilisha maumbile..mi huwa hawanitishi kbsa hao..ukiwaona tu we chapa hmna kugeuka nyuma yan.
 
mkuu iyo labda kwa madereva wa malor lkn kwa sisi wa private huwa swafi kbsa..usik ni raha sana kusafir kwanza kuna utulivu sana so kuchoka ni kwa kawaida nahasa umefika safar yko.

Mkuu:
Kwa kawaida haya magari madogo (Cars) yana starehe sana na kufanya dereva asijisikie kuchoka haraka.
Mwili wa binadamu ni lazima upumzishwe pamoja na starehe zote. Takwimu zinaonyesha uwezekano wa kupata ajali usiku ni mkubwa sana kuliko mchana.sababu kubwa ni kwamba viashiria vya ajali usiku ni vingi kuliko mchana. Ni vyema ungepata muda mrefu wa kupumzika mchana kabla ya kuanza safari za usiku.
 
nakubaliana na ww mkuu..ila kwa upande wang mim huwa napumzika vyakutoshs mchana bfore ya safar.yng usiku.na safar zang n za private zaid
 
Back
Top Bottom