Madereva wa magari ya Serekali wasumbufu

kosamfe

Member
Apr 14, 2009
71
2
Naomba tujadili kidogo pengine na kutoa ushauri kuhusiana na ukorofi wa madereva wa magari ya serikali barabarani. Utakuta dereva anakimbiza sana huku kawasha taa zote na hata wakati mwingine anatanua na kuvunja sheria za barabarani. Ukimnyima nafasi ya kupita anakutukana na kukutishia kuwa anaweza kukusababishia matatizo au kukufunga kwa kuwa eti anamuendesha mkubwa fulani. Je wao wanaruhusiwa kuvunja sheria?
 
wao hawaruhusiwi kuvunja sheria isipokuwa ni ushamba tu kutishia kumuendesha mkubwa, huyo mkubwa ni mkubwa kwake yeye dereva yawezekana hata wewe ni mkubwa kibaruani kwako. lakini pana ukweli kuwa madereva wa magari ya serikali wengi wao si wastaarabu, wanajua wazi kuwa hata wakivunja sheria ma-trafiki mara nyingi hawawashiki kwa kujua kuwa hawatawapa hongo bali wataishia kuambiana tu mie namuendesha fulani wa wizara fulani, ndio maana wanakuwa na jeuri ya kuendehs ovyo. niwapo barabarani watu wanaoendesha ovyo ni daladala, taxi na magari ya serikali hilo halina ubishi, tena kama ni usiku anatanua na kuwasha mitaa yao ya kichini inawaka utadhani karabai hata huwezi kuona unakoenda! i hate that:angry:
 
Magari yasiyokuwa na mwenyewe yanawazuzua.
Lakini hawajui kuwa yale magari yamenunuliwa kwa hela zetu na hela zetu ndizo zinazowaweka mjini.
 
Takwimu tulizo nazo. Kuna magari 40,000 ya serikali. lazima asilimia fulani ya Madereva wawe na kiburi.
 
Back
Top Bottom