Madereva kugoma tena Jumatatu tarehe 4/5/2015

Madereva kugoma tena Jumatatu tarehe 4/5/2015

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Ujumbe mfupi wa maandishi unasambaa kwa madereva kuwaasa madereva wote kutoendesha magari tarehe tajwa. Masharti ni kupatiwa mikataba maalum na vutizi ya kazi pamoja na kuondolewa kwa sharti la kwenda kusoma. Kusoma ni kila baada ya miaka mitatu.

Sioni dalili za kutekelezwa kwa masharti hayo. Masharti yameelekezwa kwa Serikali kupitia Wizara za Ajira na Mambo ya Ndani,pamoja na TABOA,TAKUBOA na washikadau wengine wa kada ya usafirishaji kwa mabasi.

Mgomo u dhahiri tarehe nne mwezi ujao,mwaka huu. Matembezi ya mshikamano pamoja na nauli za mashindano zitatamalaki!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Mzee mwenzangu utakuwa dereva wewe maana hizi habari mgomo uko flont kweli..
 
Aisee...basi jioni waziri ataenda...atatoa ahadi...utaisha kwa leo...afu utaanza tena baada ya kipindi fulani.....typical poverty viscious circle.
 
hii migomo inasababisha usumbufu sana kwa sie tunategemea public transport!! Serikali sikivu hebu malizeni hili gogoro!
 
Wakat ulipotokea mgomo awali nikajua tu kuwa kuna siku mgomo mwingine utatokea, hii ni kudhihilisha kuwa viongozi hawana habari na wananchi... mfn mdogo tu
Wazir mkuu anasema atakutana na hayo makundi yote saa 6 mchana, hv kwel tunawazili au shari tu??

Kwa nn asikutane nao asub?? Au kwa nn asubr mpaka mgomo?? Y asingechukulia kama dharura?? Hajui kuwa leo wanafunzi hawakufanya mitihani yao kwa sababu ya usafr?? Hajui hasara kiasi gani ameletea taifa kwa watu kutokwenda hospital?? Je hajui wagonjwa wangapi wamekufa leo kwa ajr ya hli??

Ifike mahari hata kama viongozi wamelewa madaraka wakumbuke watu wa hali ya chini....
Mwisho wa siku sisi sote ni wtz, tunaohitaji maendeleo. Ila kwa viongozi hawa wasioheshim wananchi wasio wazalendo, wenye kukumbatia matajr... tutasubiri boti airport... badala ya bandarini..
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
ni upuuzi wetu watanzania katika kujadili nani rais ajae badala ya kudeal na matatizo tulio nayo
 
ni upuuzi wetu watanzania katika kujadili nani rais ajae badala ya kudeal na matatizo tulio nayo


Saa sita mchana na nusu hajafika.nani anajali kiasi cha mapato Serikali WAMEKOSA $ inazidi kuimarika wakati Tsh inazidi kushuka thamani

nani anajali
 
Nimekaa Shekilango since saa moja asubuhi na hakuna basi lililondoka hadi sasa. Kwa kweli inaumiza sana na inakera sanaaa. Watunyonye ila basi vile vya muhimu watupe
 
Serikali sikivu ya CCM itatenda jambo punde

Mzee Tupatupa
 
form six nao si wameanza mitihani ya taifa leo!!??..
na hii adha ya usafiri mungu awaangazie...nchi ngumu hii
 
Kweli jamaa wamekaza mpaka jioni hamna usafiri.
 
Back
Top Bottom