Madeni ,Amtumbua Mkuu wa Soko kuu Arusha

Madeni ,Amtumbua Mkuu wa Soko kuu Arusha

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ,dkt Maulid Madeni amemtimua mkuu wa Soko kuu la Arusha,Yusuf Ngenya kwa kushindwa kufikia malengo ya makusanya ya ushuru na kodi katika Soko hilo.


Aidha Dkt Madeni amemteua Magige Makuli kuwa mkuu mpya wa Soko hilo ambaye ameonyesha mafanikio makubwa ya makusanyo yaliyofikia wastani wa sh,milioni 1.5 kwa siku.


Akizungumza na vyombo vya habari mapema.leo ofisini kwake,Dkta Madeni amesema kuwa,Ngenya ameshindwa kufikia malengo ya wastani wa sh, milioni 1 kwa siku badala yake amekuwa akikusanya kiasi cha sh,elfu 90 hadi 150,000 kwa siku huku fedha zingine zikipotkusikojulikana na kuisababishia hasara kubwa halmashauri hiyo.


Amesema chini ya uongozi wake hata mwonea haya mtumishi atakayeshindwa kutimiza malengo yake hususani suala la makusanyo ya mapato na kwamba atahakikisha hakuna udanganyifu unaofanywa na watendaji wake.


"Tangu nimefanya mabadiliko katika masoko yetu kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya makusanyo kwani mapato yameongezeka tofauti na hapo awali" Alisema


Aidha amesema Jiji hilo imejipanga kuvuka malengo ya makusanyo iliyojiwekea ya sh,bilioni 15 hadi kufikia sh,bilioni 17 kwa mwaka.


Amesema hadi sasa Jiji hilo limekusanya wastani wa asilimia 69 ambayo ni sawa na sh,bilioni 13 na kudai kuwa hadi kufikia Mei mwaka huu watakuwa wamevuka malengo ya makusanyo ya sh, billion 15.


Wakati huo huo Dkt Madeni amesema kuwa zoezi la operesheni ya kukusanya ushuru na Kodi walilolizindua January mwaka huu wamefanikiwa kukusanya kiasi cha sh, bilioni 1.9 .


Amesema Jiji hilo linamapato mengi ila baadhi ya watendaji wasiowaaminifu wamekuwa wakisababisha kupotea kwa mapato kutokana na usimamizi mbovu wanaoufanya na amejipanga kufanya mabadiliko makubwa katika kwa watendaji mbalimbali ili kubiresha upatikanaji wa mapato.


Ends......


IMG_20190228_141833.jpeg
IMG_20190228_130521.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom