Kuna jamaa alimpenda mwanamke sana, kiasi kwamba chochote atakacho anampa. Siku moja jamaa alimuahidi demu kuwa atamfanyia suprise. Jamaa siku imefika akamtumia elfu mbili 2000/=, basi demu kafurahia kajua laki mbili.
Akaenda M-pesa akakuta elfu mbili. Akachukua simu akampigia jamaa ,ile anapokea simu tu, demu alikuwa kapaniki sana kwa kutumiwa buku mbili, basi demu kamtukana jamaa kinoma na akamwambia "kuanzia leo usinijue milele kwanza wangu amesharudi"
Kifuatacho: jamaa kaomba asikilizwe akamuambia "unajua kwanini nilituma pesa hiyo? Nipo hapa yard ya magari, nilikuwa nataka nijue jina lako kamili ili nisaini ndio nikatumia njia ya M-pesa kujua jina lako. Nashukuru, maisha mema."
Upande wa pili sauti mpya ya kinyooonge ikasikika "beb beb" simu ikawa imekata. Dah! kilichoendelea sikuwepo maana nilienda kufuturu.