Madawa ya Kulevya, Waraka MPYA watoka

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,371
2,000
Waraka mwingine ulioandikwa katika lugha ya Kiswahili umechapishwa kwenye tovuti v2catholic.com... unataja majina ya Watanzania wawili kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Waraka huo wenye ulio na saini ya aliyejiita Jumaa, akiwa jela Hon Kong, tarehe 12 Desemba 2013 ni wa kurasa mbili zilizojaa maneno ya kujuta kwa kufanya kazi hiyo haramu, unaeleza mbinu mpya inayotumiwa na wafanyabiashara hao haramu kwa kuwatoa kafara Watanzania wanaokubali kuwa punda wa kubeba dawa hizo.

Mwishowe unatoa onyo kwa kila Mtanzania anayejiingiza katika biashara hiyo na kutoa wito wa kusambaza taarifa hii ili kuwaonya watu wengine wasithubutu kujiingiza katika biashara hiyo haramu.

Unaweza kubofya linki iliyopachikwa hapo juu (v2catholic.com...) kufungua na kusoma waraka huo. 

Cyan6

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,534
0
Kama kamtaja Januu ni kweli! Januu ni mkongoman na siyo mtz ila kaoa kadada kashangingi ka Ilala! Wanashirikiana kufanya hiyo business kwa sana! Poleni sana ndugu zetu mliofungwa China! Tamaa mbele mauti nyuma
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,453
2,000
Guangzhou haswa maeneo ya Dong Feng Hotel na Tian Xiu Lou kuna Wabongo wengi sana wanajifanya wanapiga dili za biashara kumbe wapo kwa ajili ya kusukuma mzigo.

Ukiacha hizi mambo za upunda na uuzaji sembe pia kuna wadada wa Kibongo wengi wanajifanya wafanyabiashara kumbe ni wauza mbunye tu.
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,743
2,000
Ukiuliza ...maendeleo ya kufutilia suala hili..ili wahusika watiwe mbaroni.waweza kujibiwa kuwa wanasubiri uteuzi wa mawaziri wa mambo ya ndani na ulinzi kujaza nafasi za waliotenguliwa.
 

fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
6,594
2,000
Guangzhou haswa maeneo ya Dong Feng Hotel na Tian Xiu Lou kuna Wabongo wengi sana wanajifanya wanapiga dili za biashara kumbe wapo kwa ajili ya kusukuma mzigo.

Ukiacha hizi mambo za upunda na uuzaji sembe pia kuna wadada wa Kibongo wengi wanajifanya wafanyabiashara kumbe ni wauza mbunye tu.

Duh, ni hatari kweli kweli.
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
6,935
2,000
Wataje na mbinu wanazotumia ili kuweza kuwaokoa watu wanaoingia kwenye mitego ya wauzaunga.Vijana wengi wanaangamia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom