Joseph Tunu
Member
- Apr 8, 2016
- 55
- 14
Kama inavyofahamika, Wenyeviti wa Bodi za mashirika na Taasisi za Umma wanateuliwa na Rais. Lakini katika hali isiyo ya kawaida, Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha ilimteua Profesa Christian Nyahumwa wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam kuwa kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha
Kuteuliwa kwa Profesa Nyahumwa kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha ni kutaka kuweka muendelezo wa kufisidi mali ya umma kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari.
Haya yanafanyika Baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi hiyo Bwana Abrahamu Nyanda kumaliza muda wake kisheria. Hata hivyo Bwana Nyanda alimaliza muda wake baada ya kudumu kwenye Bodi hiyo kwa muda wa miaka tisa mfululizo.
Wakati Profesa Nyahumwa anateuliwa na Menejimenti ya chuo kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo, tayari alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Chuo hicho kwa mihula miwili.
Inaaminika kwamba kitendo cha Menejimenti ya Chuo kuteua Kaimu Mwenyekiti wa Bodi na Bodi chini ya uenyekiti wa Kaimu mwenyekiti kuendelea na vikao vyake kama kawaida ni kudharau Mamlaka ya Rais kama Mkuu wa Nchi na Serikali. Nia kubwa mpaka kupelekea kuingilia madaraka ya Rais ni ili tu kutaka kuendelea na biashara kama kawaida (Business as usual) ya kuliibia Taifa rasilimali chache zilizopo kwa faida ya watu wachache.
Ufisadi wa mali ya Umma umekuwa ukipingwa na kila mwananchi mwenye mapenzi mema na hata Rais wa Nchi
Jambo hili la Menejiment ya Chuo cha Ufundi Arusha kuingilia madaraka ya Rais ili kutaka kutimiza malengo yao binafsi, ni kuvunja sheria na kuenda kinyume cha Katiba ya Nchi. Rais amepewa Madaraka na Mamlaka aliyonayo kisheria na kikatiba.
Chanzo: MF