Madaraja ya mishahara

watu wanaona shida kusema wahajui, wanaishia dhihaka
binafsi hata sijawahi kujua mshahara unapandaje serikalini
ila nasikiaga RAHISI(Tangu TEKWEKI,LIFUGUMA NA AMISA) mara nyingi ndo anasema ameamua kuongeza mhashara(sina uhakika kama kweli anaongeza yeye)
NB! kwa ushauri wangu ajichange apate usd 10000, ajikite kwenye biashara huko atateseka bure(au aingie kwenye siasa(ubunge,udiwani,uraisi,uwaziri nk) huku ndo kuna HERA)
KUONGEZEA! Sina uhakika kama kuna mtumishi wa serikali(ukitoa wa kisiasa kama wanaochaguliwa au kuteuliwa na RAISI ) AMBAYE ANALIPWA ZAIDI YA 1000USD kwa mwezi(ndio maana rushwa zimetawala pesa haiendani na gharama halisi za maisha)
NB! HUU NI MTAZAMO WANGU (HUENDA SIO UHALISIA)
 
Nimerudi tena.
Ipo hivi mkuu, suala la kupanda madaraja kwenye utumishi wa umma ni haki ya kila mtumishi baada ya kutimiza wajibu wake. Mfano ukiajiriwa na daraja TGS D.1 hapo unatakiwa usubiri baada ya miaka minne kwenda TGS E. Kwa maana ya mwaka mmoja wa matazamio (probation) kisha miaka mitatu ya utendaji kazi, ila katika kipindi hicho cha miaka mitatu unatakiwa kuhakikisha unafanyiwa tathimini na kupata alama nzuri na supervisor wako, kwa mfumo wa zamani ni OPRAS ila mfumo mpya wa kidijitali unaitwa PEPMIS.

Madaraja kama D.2, D.3, D.4 ..... D.12 hayo yanatokana na increments za kila mwaka kulingana na sera za utumishi, pia unatakiwa kuhakikisha unatekeleza majukumu yako vema kwenye tathmini za PEPMIS au OPRAS ili uweze kupata hizo increments kila mwaka. Hivyo utaenda D.2 kisha D.3. Ikifika mwaka wa kupanda daraja, ambapo ni kila baada ya miaka mitatu utaenda TGS E baada ya miaka mitatu mingine utaenda TGS F.

Kwa watumishi wenye elimu ndogo au vyeo ambavyo daraja la mwisho ni TGS D hao wamefika ukomo wa madaraja yao wataendelea na increments D.4, D.5, D.6 mpaka D.12 kisha watakomea hapo. Kuna madaraja ili kuyafikia unatakiwa kuwa na kiwango fulani cha elimu. Mfano kufika TGS H hadi TGS I unapaswa uwe na elimu fulani (maybe master).

Ndio maana kuna walimu wapo shule ya msingi wana mishahara hadi Tsh. milioni 3 (TGS I) kwa mwezi.
 
Hii ndio Afrika mkuu na watu wameridhika kabisa. Umasikini tumeufanya ni sifa. Ukiwa huna kazi hiyo pesa ni nyingi sana inakuwa ndogo ukiwa na kibarua kwa hapa bongo.
 
Ajira mpya atakaa mwaka 1 wa KUTHIBITISHWA. Kisha miaka 3 ya kutumikia cheo. JUMLA 4, atapanda kutoka TGS D1 kwenda TGS E1.
Hizo za D1, D2, D3 ....... Inategemea na hisani ya rais kila mwaka
 
Hii tabia ya kila mtu akileta uzi humu kusema rafiki yangu, mtu wangu wa karibu, jamaa yangu inatokana na nini, kwani ukisema niwewe kuna shida gani
 
Muulize ChartGPT au Copilot ana majibu
 
Hii tabia ya kila mtu akileta uzi humu kusema rafiki yangu, mtu wangu wa karibu, jamaa yangu inatokana na nini, kwani ukisema niwewe kuna shida gani
Tulishadanganya kwenye forum X kwamba tunauza magari, sasa huku tukija front ile CV fake inaweza ku shake.
 
Ajira mpya atakaa mwaka 1 wa KUTHIBITISHWA. Kisha miaka 3 ya kutumikia cheo. JUMLA 4, atapanda kutoka TGS D1 kwenda TGS E1.
Hizo za D1, D2, D3 ....... Inategemea na hisani ya rais kila mwaka
Degree anaweza pata TGS E?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…