UMUCHAMICHI
Member
- Oct 20, 2012
- 41
- 13
Kuna tetesi kwamba vigogo kadhaa serikalini wanataka wachukue eneo linalozunguka mgodi wa northmara vitongoji vya murwambe,nyamichele,gokona ili walinunue kwa bei chee toka kwa wananchi husika halafu wao waliuze kwa bei kubwa ya kutisha mgodini,hao vigogo wameomba huo udalali mgodini baada ya kuona kuna mvutano mkubwa kati ya mgodi na wananchi wanaogoma kuchukua malipo maana ni kidogo mno, wameelekeza timu ya watathmini toka wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makaazi wanaofanya tathmini huko northmara kwamba watu wanafanyiwa tathmini ya kupisha shughuli za mgodi wa northmara eneo la gokona,nyamichele,murwambe watachukua malipo yao huko halmashauri kwa mkurugenzi, pesa ya malipo imepelekwa huko,mtu yeyote atakaye jaribu kukataa kuchua malipo,wanakulwakatale , mali pamoja na mazao mengine yataharibiwa wewe ukiwa umepumzishwa .kuna tathmini inafanyika huko na mwenye eneo anatakiwa kusaini fomu ya kukubali hiyo tathmini kwa lazima apende asipende,maana ni dili ya wakubwa. Humu jf kuna wataalamu wa kila sector,tunaomba mtujuze sheria za ardhi na tathmini zinasemaje na viwango vya malipo.kama ni kweli hizi habari basi nchi inaekelea kubaya.