Madaktari wawili na Muuguzi wasimamishwa kazi kwa kumtolea mgonjwa lugha chafu

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Hospitali ya Rufaa ya Amana, Ilala imewasimamisha kazi madaktari wawili na muuguzi mmoja kwa madai kumtolea lugha isiyostahili Asha Said (17), aliyejifungulia chooni.

Tukio hilo lilitokea mwezi uliopita katika hospitali hiyo, baada ya Asha kujifungulia chooni na madaktari na wauguzi hao kumtolea lugha chafu.

Mganga Mkuu wa Amana, Dk Meshack Shimwela amesema leo baada ya kusimamishwa kazi watumishi hao(majina yanahifadhiwa) wamepelekwa katika Baraza la Watumishi na Madaktari wa hospitali hiyo kwa uchunguzi zaidi.

"Kilichotokea siku ile ni kauli zilitoka kwa watumishi hao kwenda kwa mama aliyejifungua ambaye pia alikuwa mdogo kiumri,”

"Sisi madaktari na waaguzi tuna taratibu za kinidhamu, huwa tunazifuata baada ya watumishi kubainika kufanya makosa hatua ya kwanza ndiyo kwa hiyo tusubiri nyingine wakati uchunguzi ukiendelea dhidi yao," amesema Dk Shimwela.

Dk Shimwela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), amesema kilichohitajika ni lugha nzuri kwa sababu kisheria ni lazima kwa mgonjwa yeyote kuoga akifika hospitali ili kumkinga na maradhi mbalimbali.


Chanzo:
Mwananchi
 
Mm mbona umri wa huyo mzazi una walakini. Binti wa miaka 17 kuwa na mtotol,si ajabu kujifungulia chooni
 
Back
Top Bottom