Madaktari wapige upya mahesabu yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari wapige upya mahesabu yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kiogopeni, Jul 2, 2012.

 1. k

  kiogopeni Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Madaktari wapige upya mahesabu yao
  Watu wamekuwa wakipaza sauti wakihimiza serikali imalizane na madaktari ili warudi kazini wagonjwa wasiendelee kuteseka.
  Kwa kiwango kikubwa mjadala wa mgomo huu wa madaktari umeelemea katika kuilaumu serikali.

  Picha inayojengwa ni kuwa madaktari wana madai halali na yanayotekelezeka kwa Bajeti iliyopo, ila serikali kwa kutokujali kwake, haitaki. "Rais kuendelea kukaa kimya kuhusu mgogoro huo ni ishara tosha kuwa hana uchungu na wananchi ambao kipato chetu hakituruhusu kwenda kutibiwa nje ya nchi." Liliandika gazeti la Majira katikati ya wiki hii likihoji watu mbalimbali.

  Nalo Nipashe likaripoti kuwa Askofu wa Jimbo la Katoliki la Singida, Desderius Rwoma, ameitaka serikali iwalipe madaktari madai yao kwani kipato wanachopata hakilingani na ugumu wakazi yao. Gazeti hilo hilo la Nipashe la Jumatano Februari likanukuu taarifa ya wanaharakati wamashirika yasiyokuwa ya kiserikali wakitoa madai hayo hayo kupitia kwa bi Hellen-Kijo Bisimba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki binadamu (LHRC).

  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake,Ananilea Nkya, yeye alikwenda mbali zaidi. Alinukuliwa na Nipashe akisema kuwa:"Serikali inafanya makusudi kutomaliza mgogoro wa madaktari kwa kuwa wao na familia zao hawatibiwi nchini."

  Ukitizama habari zote hizi na kwa hakika takribani zote, zinazoandikwa katika vyombo vya habari, mwelekeo ni huo huo. Sisi tunadhani kuwa mwelekeo huu hautasaidia kumaliza tatizo hili, wala kuwasaidia wagonjwa na wananchi kwa ujumla tunaodhani tunawatetea. Ukitizama mijadala na kelele zote hizi zinazopigwa, lile jambo la msingi halijadiliwi.

  Unapoichagiza serikali iwalipe madaktari, unaposema kuwa kwa makusudi serikali haitaki kumaliza mgogoro wa madaktari, kwa sababu haina huruma na wananchi wanyonge, ni lazima kwanza wewe uanze kumsaidia mwananchi huyu kwa kumweleza na kumfafanulia tatizo ni nini.

  Swali la msingi ni je, madaktari wanadai nini? Kwa mujibu wa taarifa ya serikali, mnamo tarehe 27 Januari 2012 madaktari kupitia chama chao yaani Medical Association of Tanzania (MAT) waliwasilisha serikalini barua yenye madai kumi. Moja ya madai hayo ni kuongezwa mshahara wa Daktari anayeanza kazi kutoka shilingi 700,000 hadi shilingi 3,500,000 kwa mwezi. Na kwamba mshahara huu uanze kulipwa mara moja. Na kwamba serikali itoe kauli ya kukubali kulipa mshahara huo kwa maandishi ndio madaktari watarudi kazini.

  Madai mengine ni pamoja na posho ambazo wameziorodhesha kama ifuatavyo:

  • Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (risk allowance) asilimia 30 ya mshahara.
  • Posho ya kulala kazini (On call allowance) asilimia 10.
  • Posho ya nyumba (house allowance) asilimia 30.
  • Posho ya kufanya kazikatika mazingira magumu (Hardship Allowance),asilimia 40.
  • Na posho ya usafiri (transport allowance), asilimia 10.

  Jumla ya posho hizi ni asilimia 120 ya mshahara. Mshahara ambao kwa sasa wanataka uwe milioni 3, 500,000. Na kwamba ni lazima serikali ikubali kuzilipa kwa maandishi niuanze kulipwa mara moja ndio madaktari watarejea kazini. Kama tulivyosema,madai yao ni kumi lakini tutosheke kwanza na haya kwa leo.

  Katika kuchambua na kujibu madai haya ya madaktari serikali inasema kuwa "kwa mujibu wa mapendekezo ya Madaktari ya mshahara pamoja na posho mbalimbali, itamaanisha daktari anayeanza kazi atapata jumla ya Shilingi 7,700,000/= kwa mwezi ikijumlisha mshahara na posho.

  "Katika majibu yake serikali inaongeza ikisema kuwa "kwa mujibu wa mapendekezo hayo daktari mshauri Mwandamizi atapata Shilingi 17,231,020/= kwa mwezi."Kwa kuzingatia ukubwa wa gharama hizi ambazo madaktari wanataka zilipwe mara moja kama sharti la kurudi kazini, ndio waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda akasema kuwa "kwa kuzingatia hali halisi ya Bajeti ya Serikali" haiwezekani.

  Na katika mazungumzo yake pale Karimjee ambapo aliwasubiri madaktari ajadiliane nao ambapo hawakutokea, alisisitiza kuwa ilikuwa katika kukutana nao wajadili pamoja kifungu kwa kifungu ili kama ni ugumu wauone kwa pamoja na kama kuna lenye wepesi wa kutekeleza mara moja,lionekane pia.

  Lakini kwa bahati mbaya madaktari hawakutaka kukutana na Waziri Mkuu wakidai kuwa wasingekutana naye bila wenzao wa mikoani kuwepo. Serikali ikionyesha ugumu wa kutekeleza madai haya ya Madaktari mara moja ilisema kuwa, endapo itatekeleza madai hayo hivi sasa kama yalivyo, mishahara ya madaktari itapanda kutoka sh. 222,214,936,800/= za sasa hadi Juni 2012, na kufikia sh.799,692,615,592.98 kwa mwaka mmoja.


  Serikali inasema kuwa kwa vile katika madai ya Madaktari wametaka pia kuwa kada nyingine katika watumishi wa afya wajumuishwe katika nyongeza hizi, ina maana kuwa itabidi serikali itoe theluthi mbili (2/3) ya mishahara yote ya watumishi wa serikali kuwalipa madaktari na wenzao katika sekta hiyo.

  Kwamba katika Shilingi 3,450,000,000,000.00 ambazo ndio mishahara kwa watumishi wote wa serikali, itabidi madaktari pekee wachukue 2,039,290,867,710/= Na watumishi wengine wa serikali waliosalia wagawane theluthi moja iliyosalia."Hii maana yake ni kwamba wao walipwe theluthi mbili na kiasi kinachobaki cha theluthi moja ndicho kigawanywe kwa watumishi wengine.""Huu ndio ukubwa wa madai (demand) ya Madaktari ambayo yamewasilishwa kwangu na wanataka Serikali itekeleze mara moja."Anasema Waziri Mkuu. Haya ndiyo baadhi ya madai ya madaktari,kwamba mshahara wa daktari anayeanza kazi pamoja na posho uwe shilingi 7,700,000 kwa mwezi.

  Haya ndiyo madai ya Madaktari na watumishi wenzao wa sekta ya afya kwamba walipwe theluthi mbili ya Tirilioni 3.45/= ambazo ndio jumla kuu ya mishahara ya watumishi wote wa serikali kwa sasa. Sasa namna nzuri ya kusaidia jambo hili, sisi tunadhani kwamba, kwanza ni kwa waandishi wa habari, wanaharakati,taasisi za kidini, Wabunge na wengine wote ambao wamejitokeza kulisemea jambo hili; kuhakiki kwamba haya aliyosema waziri Mkuu, ndiyo kweli madai ya madaktari? Kama ni kweli, ndiyo madai ya madaktari,tujiulize, yanatekelezeka,tena mara moja kama madaktari wanavyotaka?

  Kama hayatekelezeki kulingana na Bajeti iliyopo hivi sasa, tunachukua hatua gani kuwa rai Madaktari na serikali ili angalau wafikie muafaka? Kwa bahati mbaya kabisa, wengi wetu jambo hili tumelichukua kishabiki bila kuzingatia hoja za msingi na uhalisia wa madai ya Madaktari.

  Ni kweli yaweza kuwa kuna ufisadi mkubwa unaofanywa serikalini ikiwa ni pamoja na kuwalipa posho kubwa baadhi ya watumishi au wabunge kama inavyodaiwa. Ni kweli pia kuwa inawezekana serikali inapoteza fedha nyingi za umma kupitia mikataba ya kifisadi katika sekta mbalimbali za uwekezaji.

  Lakini tatizo hili huwezi kulichanganya na madai haya ya Madaktari. Kila moja litizamwe na litafutiwe ufumbuzi kwa namna yake na kwa ratiba yake. Watu waanzishe mjadala wa kitaifa kuangalia namna ya kunusuru rasilimali za nchi na namna ya kuzuiya matumizi mabaya ya fedha za serikali ili upatikane uwezo mkubwa zaidi wakutoa huduma nzuri kwa jamii na kuwalipa vizuri wafanyakazi wa umma.

  Lakini tukilitafakari hilo tujiulize tena na tena,kama madai ya madaktari ni kulipwa mshahara wa kiwango cha chini kabisa wa Shilingi 7,700,000 kwa mwezi, na ulipwe mara moja kwa kutumia Bajeti hii iliyopo mezani; serikali gani katika dunia hii inaweza kutekeleza madai haya?

  Kama madai ya Madaktari yanamaanisha kulipwa theluthi mbili ya tirilioni 3.45/= ambazo ndio jumla kuu ya mishahara ya watumishi wote wa serikali kwa sasa, kama waziri Mkuu anavyodai,tunawasaidiaje Madaktari ili waone mantiki yakutizama upya madai yao?


  Sera ya Afya Mbovu
  Serikali ijitosheleze kabla ya kutoa sadaka
  Awali tulimnukuu Askofu Desderius Rwoma akiichagiza serikali iwalipe mara moja Madaktari stahiki zao. Lakini pia baadhi ya vyombo vya habari vinatufahamisha kuwa hospitali za makanisa zimekuwa ndio kimbilio la wagonjwa. Kwamba wakati Muhimbili ikibaki tupu kwa kukimbiwa na wagonjwa, zile za taasisi za kidini zinafurika. Kwa hiyo kama alivyodai Ananelia Nkya kwamba muhimbili na hospitali nyingine za serikali zimekosa huduma kwa sababu viongozi wa serikali hawawajali wananchi, wale wenye taasisi zao za kidini ambazo zimekuwa kimbilio la wagonjwa,ndio wataonekana watu wema.

  Mwaka jana katika Bunge la Bajeti hii ambayo askofu Desderius Rwoma anataka madaktari watekelezewe madai yao ya kulipwa kiwango cha chini cha mshahara na posho ya shilingi 7,700,000 kutoka laki saba (700,000), serikali iliwasilisha pendekezo la kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini. Rekodi za serikali zinaonyesha kuwa kila mwaka serikali ‘hupoteza'mabilioni ya shilingi kupitia misamaha ya kodi. Na asilimia kubwa ya misamaha hii, zaidi ya asilimia 72, huenda katika taasisi za makanisa.

  Lakini kwa upande mwingine ni kuwa, kupitia makubaliano ya kiitifaki kati ya serikali na taasisi za makanisa (mou), serikali hutumia zaidi ya asilimia 54 ya Bajeti ya Wizara ya Afya kwa taasisi za afya za makanisa. Kiasi kilichobaki ndio huenda kwa hospitali za umma.

  Uchunguzi unaonyesha kuwa katika mwaka wa fedha wa 2009/2010 Serikali ilitumia jumla ya shilingi 85, 776, 373, 200 katika hospitali na taasisi nyingine za afya zinazomilikiwa na makanisa na zile zinazomilikiwa na serikali kwa ajili ya kulipa mishahara ya wafanyakazi na gharama za uendeshaji.

  Kati ya fedha hizo; shilingi 46, 624, 820, 500 ambazo ni sawa na aslimia 54.4 ya fedha zote zilipelekwa katika hospitali na taasisi nyingine za huduma ya afya zinazomilikiwa na makanisa. Wakati hospitali na taasisi zote za Serikali zikipewa shilingi 39, 151,552, 700 sawa na asilimia 45.6.

  Lakini la kutaja hapa pia ni kuwa, wakati serikali inatoa ruzuku hii ya zaidi ya asilimia 54 ya bajeti ya Wizara ya Afya kwa hospitali za kanisa, haiwajibiki kukagua jinsi fedha hizo zinavyotumika kama inavyokagua Muhimbili. Na zaidi ni kuwa ada wanayotozwa wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu katika hospitali za kanisa hubaki kanisani. Haziingii katika mfuko wa serikali. Hii ni sera mbovu ya afya ambayo tunadhani kama tuna nia njema ya kuisaidia Serikali na nchi hii pamoja na wananchi wake, basi tuitake Serikali na Bunge libadili utaratibu huu.

  Kwa sasa kutokana na sera hii mbovu, badala ya serikali kujenga hospitali za Mkoa na wilaya au Rufaa katika baadhi ya mikoa, hutoa fedha na kuziimarisha na kuzipandisha daraja zahanati za kanisa na kufanywa ndio hospitali za Wilaya/Mkoa. Lakini pamoja na kupandishwa daraja na kuhudumiwa na Serikali, bado hospitali hizo zinabaki kuwa ni za kanisa.

  Hivi ikitokea siku moja kanisa likisema linasimamisha huduma za hospitali zake mpaka serikali itekeleze jambo fulani, hali itakuwaje? Serikali itafanya nini?

  Wewe ambaye una jukumu la kutoa huduma za afya kwa wananchi unapoacha kujenga na kuboresha hospitali zako, badala yake unatoa fedha za wananchi kujenga na kuboresha hospitali za kanisa lisilohojiwa na wananchi madaktari wakigoma au Muhimbili ikikosa dawa, ni jambo linalozua maswali mengi yanayohitaji majibu.

  Sisi tunadhani kuwa kuna haja, kwanza kwa serikali kutizama upya utaratibu huu wa kutoa zaidi ya asilimia 54 ya bajeti ya Wizara ya Afya kuzipa hospitali za kidini.

  Pili, kuna haja kwa serikali kutizama upya ule muswada wake wa kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini ambao ulipingwa na wabunge. Msingi wa hoja yenyewe ni kuwa serikali ndio ina jukumu la kutoa huduma za afya kwa wananchi.

  Sasa inapokuwa yenyewe haina uwezo wa kutoa dawa za kutosha katika hospitali zake hali kadhalika kuwalipa madaktari wake, inakuwaje ihamishe tena uwezo huo mdogo kwa kutoa ruzuku kwa taasisi ambazo kimsingi hazina wajibu ilionao serikali?

  Na ndio maana zinashukuriwa kwa kuisaidia serikali. Sasa katika utaratibu huu wa serikali kutumia asilimia kubwa ya Bajeti yake kuyapa makanisa kuliko inavyotumia katika hospitali zake, nani anamsaidia nani? Mantiki ya taasisi za kidini kuisaidia serikali katika kutoa huduma za afya ni kuwa viongozi wa kidini watakusanya Zakka, sadaka na michango kutoka kwa waumini wao na watu wengine wema kuanzisha na kuendesha shule na huduma za afya.

  Sio serikali kuchota fedha katika kodi za wananchi unalipa Kanisa liendeshe hospitali halafu unalishukuru kwamba linaisaidia serikali
  . Matokeo yake ndio haya, serikali inaonekana haina huruma kwa wananchi, na taasisi za kidini zinaonekana ndio wakombozi.  Wagonjwa wasifanywe‘Collateral Damage'
  Katika mgogoro huu unaoendelea kati ya serikali na Madaktari, waathirika ni wagonjwa. Kwa bahati mbaya mjadala unaoendelea, umekwepa kabisa kuzungumzia haki ya mgonjwa. Ile haki yake ya uhai. Kwamba uhai wake kama binadamu usitolewe kwa kisingizio cha madai au mgomo wa Madaktari. Ipo tabia ya majambazi na maharamia kuteka ndege na kuwashikilia abiria-watu wasio na hatia na kutishia kuwauwa wasipotekelezewa madai yao.

  Ipo pia tabia ya Marekani na NATO ya kutojali maisha ya wasio na hatia pale inaposhambulia hasa nchi inazovamia. Wao wanaita ‘collateral damage'. Je, hatudhani kuwa kwa mtindo huu wanaotumia madaktari wetu ni sawa na kuwateka nyara wagonjwa na kuwauwa kwa kuwanyima matibabu ili serikali itekeleze madai yao?

  Je, madaktari wetu wameamua kutumia mtindo na hoja za marekani na NATO za kutojali kuwauwa watu wasio na hatia ilimuradi wapate wanachokitaka? Je, hatuoni kuwa kwa mtindo huu nikuwa wagonjwa ambaoni Watanzania wenzao madaktari hawa, wameshawekwa rehani (ransome) na vifo vyao vimekuwa ‘collateral damage'?Lakini Marekani na NATO hawafanyii hayo kwao. Wanawaheshimu na kuwajaili mama, baba,dada zao, ndugu, jamaa na raia wao.

  Madhalimu hao hufanya uharamia na mauwaji katika nchi za nje wanakovamia kuganga njaa na kupora mali kama walivyofanya Iraq na Libya. Pamoja na kudorora uchumi wao, wataalamu wao hawajachukua hatua za kuruhusu vifo vya ndugu zao ili wapate masilahi zaidi. Kwa upande mwingine, sio sahihi kuangalia kisingizio cha posho za wabunge kuwa kigezo cha kuwahurumia madaktari. Ziangaliwe sekta na pande zote, hasa wananchi masikini ambao hawana uwezo wa kwenda kupata matibabu katika hospitali za kulipia.

  Wenye shida ya kuidai serikali sio madaktari tu. Wapo wakulima wa mahindi, pamba na karafuu wanaopunjwa bei ya mazao. Je, nao wagome? Tatizo kubwa hapa ni moyo wa uzalendo kwa nchi na wananchi. Moyo huo unawataka watoa huduma wawe watu wa mwisho kuwasahau wananchi na maisha yao.

  Jaaliya makundi mengine yanayofanya kazi kwa uzalendo na kwa kujitolea kwa hali ya juu na zaidi kwa kuhatarisha maisha kama Polisi na wanajeshi nao waamue kudai kupata kiwango cha chini cha mshahara, japo wa milioni 2 kwa mwezi la sivyo wanagoma,hali ya nchi na hali ya usalama wa raia na mali zao ingekuaje?


  Source: AN-NUUR RABBIUL AWWAL 1433, IJUMAA
  FEBRUARI 10 - 16, 2012
   
 2. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  Mbona outdated report ,hii mbona ilitoka since February 2012
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Naona mwandikaji wa makala hii ana ajenda yake ya siri ambayo inajitegemea yenyewe na wala haiusiani kamwe na huu mgomo unaoendelea. hivyo ushauri wangu kwake, ni kwamba ili aweze kueleweka vizuri,ni vyema akaleta hoja yake hiyo jinsi ilivyo bila ya kuiunganisha na mada nyingine yenye mwelekeo tofauti

  Baada ya kusema hayo, napenda niungane na wale walio hisifia hotuba ya JK aliyo itoa jana. Pamoja na hotuba kuwa nzuri ikilinganishwa na zile za nyuma bado ilikuwa na mapungufu yake: Mojawapo ya mapungufu hayo, ni kutozungumzia chochote kuhusu fedha zilizoripotiwa kufichwa huko uswizi; mgogoro uliopo hivi sasa, chimbuko lake ni uhaba wa fedha, hivyo inapodhihirika ya kwamba uhaba huo wa fedha unachangiwa kwa kiwango kikubwa na utoroshaji wa rasilimali yetu nje ya nchi, rais ategemewi kukaa kimya kwa jambo hilo

  Mbali na hayo, kuna haja kubwa ya rais wetu kuanzisha mjadala wa kitaifa kuhusu namna nzuri ya kuendesha uchumi wetu. Sera za uchumi zilizoanzishwa wakati wa Mkapa ni dhahiri zimeshindwa kutatua tatizo la mzingi la uchumi wetu ambalo ni ukosefu wa ajira na uwekezaji endelevu, Kama itakavyokumbukwa, mbinu iliyobuniwa kwaajili ya kupambana na tatizo hilo wakati wa enzi ya Mkapa ni kujenga tabaka la watu wenye kipato cha kati, kwa imani kwamba tabaka hilo lingelitumia utajiri wake katika kuwekeza hapa nchini, na hivyo ajira na ukuaji wa kasi wa uchumi. Mbinu nyingi baadhi zikiwa ni halali na nyingine zikiwa ni haramu, zimekuwa zikitumika katika kujenga tabaka hilo la kipato cha kati; hata hivyo jambo moja linalojitokeza ni kwamba wengi wa watu hao waliofanikiwa kuingia kwenye tabaka hilo,hawapendi hata kidogo kuwekeza hapa nchini, badala yake wamekuwa wakihamisha utajiri wao kwenda nchi za nje. Hali hiyo, imesababisha hizo juhudi za kujenga tabaka la kipato cha kati, badala ya kuinua uchumi wa taifa zichangie katika kuudidimiza. Ni kutokana na sababu hiyo natoa rai kwamba kuna haja ya kutazama upya sera hiyo.
   
 4. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,640
  Likes Received: 16,593
  Trophy Points: 280
  Nadhani mtoa mada hajui MOU kati ya hizo hospitali za kidini na serikali.
  Pili hiyo asilimia wanayopeleka kwenye hizo hospitali sidhani kama ni ruzuku ila ni malipo ya madakatri,wauguzi na wataalamu mbalimbali walioajiriwa kwenye hospitali hizo.
  Tatu asilimia nyingine ni kwa ajili ya manunuzi ya dawa na vifaa vingine ili kuchangia gharama za uendeshaji za hospitali hizo.
  Gharama wanayotozwa wagonjwa inatumika kwa ajili ya kuhudumia hospitali hizo na wala haziendi makanisani.
  Na sadaka na zakha zinazolipwa na wakristu makanisani asilimia fulani inaenda kuendeleza hospitali hizo na asilimia nyingine inatoka kwa wafadhili ambao kwa sasa mchango wao ni mdogo.
  Nafikiri waandishi wa habari wawe chachu ya kuelimisha watanzania na siyo kuwagawa kwa matabaka ya kidini,vyama.Kama Mwandishi anaaona haeleiw jambo ni bora kuuliza kulipatia maelezo na siyo kukurupuka na kuandika siyo tu ujinga bali upumbavu na mwisho wa siku unaonekana kilaza wa habari kwani wanasema usilolijua ni kama usiku wa kiza....
   
 5. mpiganaji jm

  mpiganaji jm Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi siungi mkono kabsaaaa mawazo ya mtoa mada, kwani ni uwongo usio kubalika kwamba serekali haina pesa, wabunge wanalipwa 10m kwa mwezi, mawaziri nao zaidi ya hapo, vikao kila kukicha, safari za nje ya nchi zisizo na msingi thn mnatuambia hakuna pesa,,,,,, no way huu ni uongo tuuuuuuuuuu
   
 6. n

  ndagabwene Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shwari mtu mzima?mie wala siitaji kuandika vitu vingi hapa kwani huyu mtu hajui hawa jamaa wanagoma kwa nini.so ajipange mtu mzima na sio kukurupuka.
   
Loading...