Pragmatist
Member
- Sep 21, 2012
- 18
- 1
Jana tarehe 12/11/2013 kipindi cha BBC saa 12 jioni iliarifiwa kuwa asilimia arobaini (40%) ya madaktari wanaomaliza Chuo Kikuu wanakimbilia nchi za nje.
Kiwango hiki kinashtusha kwa kuzingatia ukweli kuwa tofauti na wasomi wengine, madaktari wanasomeshwa BURE na hawarudishi gharama zilizotumika kuwasomesha.
Kabla ya miaka ya 1994 wanafunzi wa Vyuo Vikuu walitakiwa kusaini DHAMANA (Bond) ya kuifanyia kazi Serikali kwa miaka 5 kabla ya kuruhusiwa kufanya kazi mahali pengine.
KWA VILE MADAKTARI WANAAJIRIWA MOJA KWA MOJA NA SERIKALI PINDI WANAPOMALIZA CHUO, na Kwa vile kodi za Watanzania zinatumika kuwasomesha madaktari hawa ambao hatimaye wanawatelekeza Watanzania, ni lazima Serikali iweke utaratibu maalum wa kuwabana madaktari waliosomeshwa na pesa za walipa kodi.
Watakiwe kusaini dhamana (Bond) au watakiwe kurudisha gharama walizotumia kusomeshwa, vinginevyo wananchi wanaibiwa! Wabunge wetu walisimamie hili.