Madaktari hivi ndivyo mtakavyo shindwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari hivi ndivyo mtakavyo shindwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KYALOSANGI, Jan 30, 2012.

 1. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,890
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Kuna wakati binadamu akiambiwa ukweli huwa hakubali kama unapingana na maslahi yake!

  Nina wasiwasi huenda moto walioanzisha madaktari ukaonekana kama ni madai yasiyozingatia hali halisi ya Watanzani
  Naamini hata haya ninayo andika yatawakera wengi ,lakini naamini huu ni ukweli!

  Binafsi naunga mkono madaktari kudai maslahi yao kutokana na mazingira wanayofanyia kazi .Na kwa misingi hii naungana na vuguvugu la kuishinikiza serikali iboreshe maslahi ya watumishi hawa.

  Hata hivyo napingana na naman wanavyojenga hoja zao! Tukumbuke kuwa civic competency ya Watanzania ilichakakachuliwa na mfumo wa ujamaa na chama kimoja ,hivyo bila madakatri kubainisha kwa undani ni kwanini wanadai kiasi hicho wangewaelimisha zaidi Watanzania kuwa nivipi Serikali inauwezo wa kutekeleza.

  Nianavyo mimi matatizo ya sekta ya afya nchini ni ya kimfumo zaidi, mamlaka ya Rais kikatiba ya uteuzi wa viongozi na mmundo wa serikali ni tatizo .kwa kuwa hatuna ajenda za kitaifa ndio maana leo hii kila waziri anayeteuliwa anaweka vipaumbele vyake.

  Leo hii wizara ya afya ni mojawapo ya wizara zinazopewa fedha pungufu kulingana na mahitaji yake.
  N hata hicho kidogo kinatumikaje ?

  Madaktari mnapaswa kuwaelimisha Watanzania kuwa ni kwa nini serikali inawaficha wezi wa mabilioni ambayo yangetumika kutoa huduma za afya ikiwemo maslahi ya watumishi!

  Kama mtu mmoja anaiba fedha serikalini anarudisha na serikali inakiri lakini matumizi ya fedha hizo ni siri ,hilo ni tatizo la kimfumo na mawazo mgando ya Watanzania ya kutohoji viongozi wao

  Leo hii madaktari mnahangaika na Mganga Mkuu wa seriklai kuwa ndio tatizo ! huyu ni mtazamo finyu
  Kwa wanaomfahamu Dr Mtasiwa wanasikitishwa na hilo!

  Mganga Mkuu wa SERIKALI hana nguvu ya uendeshaji wa wizara! Re
  jeeni malamalamiko ya Freeman Mbowe kuhusu mamalaka ya makatibu wakuu katika wizara wakati wa skendo ya Jairo!

  Labda kosa lake(MGAMGA MKUU WA SERIKALI) ni kwa nini anakubaliana na mfumo huu! lakini hii ni kosa letu wote kuwa ni kwa nini tunatatawaliwa kijinga na tunakubali tu!

  Kama mamalaka zinamuangalia katibu mkuu anayekwenda kununua suti za bilions Uingereza kwa ajili ya maonesho ya 77 na 88 tena bila kuzingatia utaratibu na kwa kutumia mabilioni hayo huku kunamama wakijifufungulia sakafuni
  WIZARA INAPEWA TUZO !

  NANI ALAUMIWE
  Niseme hivi bila ktafuna maneneo MATATIZO YENU NI MFUMO HUU MBOVU WA UTAWALA

  PILI, KWA SASA ANAYE TOA MWELEKEO SEKATA YA AFYA KWA SASA SI MWINGINE NI BLANDINA NYONI ...BILA KUHOJIWA NI MTU YEYOTE YEYE NDIYE DIRA YENU KWA SASA, MNAOTEGEMEO WAMSHAURI HAWANA UBAVU HUO ...(SIO WAJINGA) TATIZO NI MFUMO
  Kuna mambo mengi ya kuandika ...........

  Please the BRAINS jengeni hoja vizuri ushindi ni wenu hapa .
  iLA MTUKUMBUKE NA SISI BASI AH!
   
 2. k

  kuzou JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hospitali kimfumo haziingizi pesa nyingi zinategemea serikali nchi nyingine kimfumo hospili zinaingiza pesa nyingi hivyo kuwa na uwezo wa kuwalipa madaktari uliza watu waendao india hulipa shs ngapi kwa kitu kile kile kinachofanywa dar,MADAKTARI PIGANIENI MFUMO UBADILISHENI KABLA YA KUDAI PESA,HUWEZI MLAZIMISHA NGOMBE ATOE MAZIWA MENGI WAKATI HANA
   
 3. W

  We know next JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watanzania bwana, hivi maneno tutaacha lini?? OK wewe ulikuwa wapi kuweza kujenga hiyo hoja ya kimfumo - kiutawala?? Na kama unafahamu kabisa kuwa tatizo kubwa ni Uongozi, sasa madaktari wana kosa gani?? Nadhani pesa mabazo zinafujwa Serikalini, kama kweli zingethibitiwa, si kwa madaktari tu, bari watumishi wengi wa serikalini wangekuwa na maslahi mazuri. Lakini tatizo ni Utawala. Mwaka jana Waziri Mkuu huyuhuyu, wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya utumishi wa umma pale Mnazi mmoja, alisema hivi, 3/4 ya wafanyakazi ktk serikali ni mbumbumbu, hawafanyi kazi kama inavyotakiwa, na alisema ni 1/4 tu ndio wanaofanya kazi vizuri. Sasa leo anapokuja na kuanza kutupa figure za mishahara za wafanyakazi wote serikalini kuwa serikali haiwezi kulipa, si awafukuze kwanza hao mbumbumbu then pesa za mishahara yao zilipwe kwa hao 1/4 waliobaki?? Yaani hii nchi kuna kijiwe cha watu ndio wanaokaa na kupanga kuwa nchi iiendaje sasa, tena kwa hila tupu. Madaktari wameonyesha njia, tuwauunge mkono, nasema na wengine ktk sector nyingine anzeni migomo ili nanyi mfukuzwe. tuone kama wataweza na hayo mabavu yao. Crazy hii Gvt.
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani wabunge walipoongezewa posho walipigania mfumo gani kubadilishwa? Embu funguka vizuri kwenye hii hoja yako
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu so drs. let you be the unit to accoplish what you aiming
   
 6. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,890
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  mkuu wabunge ndio wananufaika na mfumo huu watapigana nao vipi mkuu! Kwani madaktari nao wanataka kuwa kama wabunge ....mbona unanitsha aisee!
   
 7. ngamiamzee

  ngamiamzee JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pesa zipo mhe anakula nazo raha kuzunguka dunia mpaka jana ni safari 355xmilion 300
  unapata bilion 105 sasa mnataka je ni mtu mmoja na wapambe wake hivyo hali ndiyo
  ilivyo george bush utawala wake wa miaka nane kasafiri nje mara 69 tu sasa kitaifa
  kidogo masikini kama hiki pesa zote wanakula wakubwa wenye meno sasa akuna la kufanyia
  yetu macho kila mtu aangalie usalama wake ukifanikiwa kuiba iba lakini nenda kaibe nje ya tanzania
  leta nyumbani na siyo humu ndani wameshamaliza zote

  kikupacho raha na uchungu kitakupa
   
 8. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,890
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  ndugu haya si maneno ni ukwelimatatizo mengi ya nchi ni mfumo tulionao @
  kosa la madaktari ni kutopigamna na mfumo zaidi wanapigananamatokeo /athari za mfumo huo usipo badilika kesho pia litaibuka lingine!
   
 9. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,694
  Likes Received: 2,375
  Trophy Points: 280
  Thank matey ! exactly my thoughts,but where do we go from here? we all know not only health sector beepin red,all other key sectors-Agri,Ed,mining you name them.WHERE DO WE GO FROM HERE BAJAMENIIII??
   
 10. clet 8

  clet 8 JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,065
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Yote haya yanasababishwa na serkali y2 migomo, maandamano n.k kwa sababu imeshindwa kuwajibika katika misingi ya haki na usawa kwa watu/wananchi wake. Yanayotokea hayatokei kimiujiza, natokea kwa sababu ya makosa ya kiutendaji ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa ya kibinafsi.

  Naumia kuona wagonjwa wakikosa huduma za kiafya mahospitalini, lkn naunga mkono mgomo wa madaktari. Serikali isikilize hoja zao.
   
Loading...