Tatizo la watanzania hawaeleweki,Ni kama bendera fuata upepo.Maandamano ni haki ya msingi ya kikatiba.Labda niseme kuwa watu wengi wanadhani kuwa haki ya mtu inaombwa kama kipande cha mkate kwenye sahani.Haki siku zote inanyakuliwa na hasa kama imebakwa na wabaka haki za wananchi.Namuunga mkono mh.Kigwangala kwa madaktari wetu kugoma.Nchi isiyothamini wataalamu wake ni nchi dhalimu isiyoheshimu utu na thamani ya wanachi wake.Kwa kuwa nchi hii inaongozwa kidharura maandamano yatakuwa ni suluhisho la matatizo yao.Maandamano yakianza ndo serikali itakurupuka toka usingizini.Msirudi nyuma aluta continua,viva madaktari viva,viva Tanzania viva.