Taasisi ya Mifupa-MOI
Member
- Apr 15, 2025
- 91
- 174
Madaktari bingwa wa usingizi tiba nchini Tanzania wamepata mafunzo maalum kutoka kwa madaktari bingwa kutoka India, kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma za usingizi tiba katika taasisi mbalimbali za afya nchini Tanzania.
Mafunzo hayo ya siku 3 yaliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Madaktari Bingwa wa Usingizi Tiba na Ganzi Salama Tanzania (SATA) na wadau wengine wa sekta ya afya, yalihusisha mbinu za kisasa zinazolenga kuimarisha usalama wa mgonjwa wakati wa upasuaji na huduma za uangalizi maalum.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, jana Julai 24, 2025 Dkt. Angela Muhozya, Daktari Bingwa wa Usingizi wa Moyo na Rais ajaye wa SATA, alisema mafunzo hayo yamewapa madaktari wa Tanzania mbinu mpya muhimu ikiwemo mbinu za kupunguza maumivu bila kutumia dawa nyingi, matumizi ya mashine za kisasa za ufuatiliaji na matumizi ya dawa za kwenye mishipa pia utoaji wa ganzi salama.
"Kupitia mafunzo haya, madaktari kutoka India wamewajengea uwezo madaktari wetu wa ndani kwa kutumia mbinu za kisasa na salama zaidi, ambazo zinalenga kupunguza madhara kwa mgonjwa na kuongeza ufanisi wa huduma... Huu ni mwanzo mpya kwa taaluma ya usingizi tiba nchini,” alisema Dkt. Muhozya.
Naye, Katibu wa SATA, Dkt. John Kweyamba alisema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa chama hicho wa kuhakikisha kila mwanachama anapata elimu bobezi ya usingizi tiba.
Awali, mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea, ambaye alisisitiza umuhimu wa kutumia ujuzi huo kuimarisha huduma kwenye hospitali zote, akisema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi katika kuinua viwango vya huduma za tiba.