Nilikuwepo mahakamani. Bahati mbaya muda wa kusikiliza kesi ulihamishwa kutoka saa nne nusu ghafla hadi saa sita na nusu hivyo, nikashindwa kuisikiliza kesi live. Hata hivyo, baadaye niliongea na Mpendazoe. Ukweli ni kwamba Jaji alitupilia mbali mapingamizi ya wakili wa Mahanga. Huu ndo ukweli. Na kesi inaendelea tarehe 22 june 2011. Sasa kama kesi imtupiliwa mbali june 22 tutaenda kufanya nini mahakamani?
Jana nilimpigia mmoja wa waandishi wa gazeti la Tz daima kujua ukweli wa jambo hilo, nikaambiwa kuwa hata humo ndani kuna taarifa zisizothibitishwa kuwa mwandishi aliyeandika habari ile anachukua mulungula kutoka kwa …… wa chama cha magamba ili kupotosha ukweli.