Madai ya Mpendazoe yakutwa na dosari; Mahakama Kuu yatoa amri ya kuondolewa kwa kesi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madai ya Mpendazoe yakutwa na dosari; Mahakama Kuu yatoa amri ya kuondolewa kwa kesi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 6, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Monday, 06 June 2011

  NA NJUMAI NGOTA

  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imetoa amri ya kuondolewa kwa kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea, Fred Mpendazoe.

  Hatua hiyo ya Mahakama Kuu inatokana na sababu kwamba baadhi ya mambo katika hati ya madai ya Mpendazoe kuwa yamejificha.

  Mpendazoe alifungua kesi ya msingi mahakama hapo, akipinga ushindi wa Mbunge wa Jimbo hilo, Dk. Makongoro Mahanga. Walalamikiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo.

  Jaji wa Mahakama hiyo, Profesa Ibrahim Juma alitoa uamuzi huo jana baada ya kupitia hoja zilizowasilishwa
  mahakamani hapo na upande wa mlalamikaji na walalamikiwa. Alisema ametoa amri ya kuondolewa kwa kesi hiyo mahakamani kwa sababu baadhi ya aya katika hati ya madai ya Mpendazoe ina mambo yaliyojificha ambayo yangeweza kuwasaidia upande wa walalamikiwa kuandaa utetezi wao.

  Jaji alisema anaiondoa kesi hiyo na kutoa siku 14 kwa upande wa mlalamikaji kufanya marekebisho katika hati hiyo.

  Wakili wa Serikali, David Kakwaya katika hoja zake aliiomba mahakama iifute kesi hiyo na kwamba katika hati ya madai ya Mpendazoe kulikuwa na dosari, kwani kuna baadhi ya mambo yaliyojificha ambayo yangeweza kuwasaidia katika utetezi wao.
   
 2. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Ibrahim Juma alikua Dean Faculty of Law UDSM - alimbeba sana mtoto wa JK katika kipindi hicho, kwani alwahi kufeli si chini ya mara mbili..2005 aliteuliwa kuongoza Tume ya kuchunguza mauaji ya wafanyabiashara wa madini-kama mnakumbuka kesi ya Zombe..

  Pia kama sikosei alipewa shavu la uenyekiti wa Law Reform Commission..ni katika utaratibu wa nilishe nikulishe...kesi hii ni ngumu, itakula kwa Mahanga kama haki itafuatwa...

  Mpendazoe atafute sababu za 'kukosa imani' na jaji huyu...
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Duuh!
  I love JF. Kuna vichwa vya instant analysis.
   
 4. M

  Masauni JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mdau nakupa shavu.
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni kwa Mujibu wa Gazeti la Uhuru

  Gazeti la Nipashe limeandika Kinyume Kabisa

  Lenyewe Limeandika Mahakama imetupilia Mbali Maombi ya Upande wa Mlalamikiwa
   
 6. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sasa hapa ndipo tutakapojua Waandishi wa Magazeti gani ni Makanjanja na Magazeti gani yana Waandishi makini.

  Je ukisoma hiyo habari na kichwa chake Vinaendana!
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,813
  Likes Received: 420,401
  Trophy Points: 280
  Code:
  Mpendazoe atafute sababu za 'kukosa imani' na jaji huyu...
  Hakuna sababu ya kumkataa Jaji kwa sababu huu uamuzi haujaharibu kitu na vigumu kutumia yaliyo nje ya uamuzi huu katika kumkataa Jaji...amwache aiamue hii kesi halafu kama kuna dhuluma basi Mahakama ya Rufaa itafanya kazi yake.............
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,813
  Likes Received: 420,401
  Trophy Points: 280
  Kesi ya uchaguzi Segerea: Fred Mpendazoe aendelea kumng'ang'ania Dkt. Mahanga
  Na Rehema Mohamed

  MAHAKAMA Kuu imetupilia mbali ombi lililowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea Dkt.Makongoro Mahanga na wakili wa serikali, Bw.David Kawaya, la kutaka
  mahakama hiyo ifute kesi ya kupinga matokeo ya ubunge katika jimbo hilo.

  Mlalamikaji katika kesi hiyo ni aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Bw.Fred Mpendazoe.

  Uamuzi wa mahakama ulitolewa jana mahakamani hapo na Jaji Profesa Ibrahim Juma.

  Jaji Juma aliwapa muda wa siku 14 mawakili wa Bw.Mpendazoe kufanyia marekebisho hati ya madai ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.

  Marekebisho hayo ni pamoja na kuondoa vituo vya kupigia kura ambavyo vilikuwa eneo la Buguruni, Tabata na Kipawa ambavyo katika hati hiyo, havikutajwa mahali halisi vilipokuwa, ambavyo kasoro yake ilikuwa ni kutohesabiwa kura zake.

  Ilielezwa kuwa katika hati ya madai kuna baadhi ya aya zimefumbwa hivyo itampa shida mlalamikaji katika kuandaa utetezi wake.

  Kesi hiyo itajwa Juni 22, mwaka huu tayari kupangiwa tarehe ya kusikilizwa.

  Mei 25, mwaka huu wakili wa Dkt.Mahanga ,Bw.Jerome Msemwa na Bw.Kawaya waliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kutaka kufuta kesi hiyo kwa madai kuwa hati ya kesi hiyo ina kasoro za kisheria.

  Bw.Mpendazoe katika madai yake anaitaka Mahakama Kuu itengue ushindi wa Dkt. Mahanga kwa kuwa taratibu za Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 hazikufuatwa.

  Kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, yalitokea mabishano makali ya kisheria, ambapo, wakili wa Bw. Mpendazoe, Peter Kibatala na wa mlalamikiwa (Dkt.Mahanga), Bw.Jerome Msemwa ambaye aliiomba mahakama kufute shauri hilo.

  Alidai kuwa Bw.Mpendazoe hakufuata taratibu wakati wa kufungua kesi hiyo, ambapo ilitakiwa ianze kusikilizwa kasoro zote za kisheria mbele ya Msajili wa Mahakama Kanda na baada ya hapo ifikishwe kwa jaji.

  Alidai kuwa kutokufanya hivyo, kunakiuka kifungu cha 8 kidogo cha (1) cha sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010, ambapo jalada linatakiwa kufikishwa kwa msajili ili kusikiliza kasoro za kisheria au makosa mbalimbali ili yafanyiwe marekebisho kabla ya kufikishwa kwa jaji kusikilizwa.

  Pia, wakili huyo alidai kuwa katika hati yake ya malalamiko Bw.Mpendazoe hakutaja majina ya vituo ambavyo anadai vilifanyiwa uchakachuaji wa kura na kwamba hakuna maelezo ya kutosha hivyo mahakama ifute kesi hiyo.
   
 9. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hebu tueleze chuo chenu kinavyofanya kazi, mtu anafeli halafu dean of faculty "anambeba," anambeba vipi, anabadilisha grade aliyopewa na mwalimu mwingine au anabadilisha policy ya mandatory retention GPA kwa mwanafunzi mmoja?

  Au kama alipasishwa juu kwa juu, wewe umejuaje alifeli?
   
 10. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,205
  Likes Received: 267
  Trophy Points: 180
  Hata mimi nilitaka kushangaa. Which is which?
   
 11. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ukisoma makala zote mbili ile ya Uhuru na ya Nipashe utaona ya kwamba Jaji Ibrahim kamsaidia Mpendazoe. Kimsingi kagundua mapungufu ya hati ya awali iliyowasilishwa na kawataka Mpendazoe na mawakili wake wairekebishe ile kesi ianze mara moja na sio kupoteza muda kujadili "technicalities". Mpira upo kwa Mpendazoe na mawakili wake, wairekebishe hati then waiwasilishe. Kesi hii ina ushahidi wa hata kumfunga Mh. Mahanga
   
 12. S

  Sio Mwanasiasa Senior Member

  #12
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kaka me nadhan ungejadili hoja ya msingi na c kumjadili mtu,tusifanye hii ndio hulka yetu hapa jamii forums.Samahan kama ntakua nimekukwaza
   
 13. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  ...narrow-minded...
   
 14. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  seems you want to "know" more, ni-pm..
   
 15. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wewe unachanganya issue. Yaani kuna watu hapa kwenye professionals wanaweka siasa. Yaani tumefika wakati kama unatengeneza barabara, ukasema ili barabara iwe imara basi inabidi uwekwe mkondo wa maji, watu watakuuliza wewe ni chama gani? Yaani hawataki kuangalia mantiki tena ya kitaalamu. Kama ni muhasibu, ukisema sipitishi malipo mpaka supporting documents ziwepo watakwambia wewe wakati unasoma ulilipiwa ada na chama fulani. Yaani utumbo mtupu.
   
 16. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2011
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Kiongozi wa tume ya wana madini wa mahenge alikuwa jaji kipenka na siyo prof. Juma
   
 17. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Time will tell. Kila kitu kitajulikana siku moja.
   
 18. S

  Sio Mwanasiasa Senior Member

  #18
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  onyesha basi upeo wako kwa kujadili hoja,watu wenye akili ndogo daima hujadili watu, na wale wenye akili za kati....na wale wervu wanajadili.....tafuta nafasi yako
   
 19. N

  Nanu JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Source gazeti gani? magazeti mengi yameandika lakini vichwa tofauti na maana tofauti!
   
 20. N

  Nanu JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii hapo chini ndiyo story ya Nipashe. Nipashe si la Chama, hivyo nadhani ni more credible kwa hili kuliko Uhuru, hebu someni habari yenyewe. Inatakiwa pia mtu unapofany post ueleze chanzo kama gazeti taja gazeti lenyewe:

  Mapingamizi ya Mahanga kwa Mpendazoe yatupwa

  Na Hellen Mwango

  7th June 2011


  Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali mapingamizi yaliyotolewa na walalamikiwa, Mwanasheria Mkuu na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Makongoro Mahanga, wakitaka kesi ya kupinga ushindi wa mbunge huyo dhidi ya aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Fred Mpendazoe.
  Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Profesa Ibrahim Juma baada ya kupitia mapingamizi na majibu ya pande zote mbili, ambapo walalamikiwa waliomba mahakama kuifuta kesi hiyo kwa kuwa hati ya madai ina mapungufu ya kisheria.
  Hata hivyo, wakili wa mlalamikaji, Peter Kibatala alidai hati hiyo ilikuwa sahihi ambapo aliomba mahakama kutupilia mbali mapingamizi hayo.
  Akitoa uamuzi huo, Jaji Profesa Juma, alisema madai yaliyotolewa na walalamikiwa ya kutaka kesi hiyo ifutwe hayana msingi isipokuwa mlalamikaji arekenishe hati ya madai kwa kuondoa vituo 10, ikiwemo viwili vya Buguruni, vinne vya Tabata na vinne vya Kipawa.
  Jaji Profesa Juma alisema hati ya kiapo iko sawa na kwamba kati ya vituo 259 ambavyo vilivyokuwa katika hati hiyo, 10 havitaongelewa katika kesi hiyo ambapo vitakavyotolewa ushahidi ni vile vituo 120 vya Kiwalani na 129 vya Vingunguti.
  Kesi hiyo itatajwa Juni 22, mwaka huu saa 4:30 asubuhi.
  Mapema mahakamani hapo, mabishano makali ya kisheria yaliibuka mahakamani hapo ambapo, wakili wa mlalamikiwa, Jerome Msemwa, aliomba mahakama kufutilia mbali shauri hilo kwa kuwa hati ya kesi hiyo ina mapungufu ya kisheria.
  Alidai Mpendazoe hakufuata taratibu wakati wa kufungua kesi hiyo ambapo ilitakiwa ianze kusikilizwa kasoro zote za kisheria mbele ya Msajili wa mahakama hiyo wa kanda, na baada ya kukamilika ifikishwe mbele ya jaji.
  Alidai kuwa kutokufanya hivyo, kunakiuka kifungu cha 8 kidogo cha (1) cha sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010, ambapo jalada linatakiwa kufikishwa kwa msajili na usikilizwaji wa ama kasoro za kisheria au makosa mbalimbali yanafanyiwa marekebisho kabla ya kufikishwa mbele ya jaji anayepangiwa kusikiliza.
  Pia, wakili huyo alidai kuwa katika hati yake ya malalamiko Mpendazoe hakutaja majina ya vituo ambavyo anadai alifanyiwa uchakachuaji wa kura na kwamba hakuna maelezo ya kutosha mahakama ifutilie mbali kesi hiyo. Akijibu hoja za upande wa mlalamikiwa, wakili Peter Kibatala alidai kuwa mapingamizi yao hayana msingi na kwamba mahakama itupilie mbali madai ya kufuta kesi hiyo.
  Kibatala alidai kuwa kuhusu kutaja majina ya vituo katika hati ya kesi hiyo, sio sahihi kwa kuwa ni sehemu ya ushahidi wao wakati wa usikilizwaji kesi ya msingi itakapoanza na kwamba mapingamizi hayo hayana msingi yanapoteza muda.
  Katika kesi ya msingi Mpendazoe anapinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 jimbo la Segerea yaliyomtangaza Dk. Mahanga kuwa mbunge wa jimbo hilo.
  Hata hivyo, Jaji Profesa Ibrahimu Juma alikubali maombi ya Mpendazoe yaliyowasilishwa kupitia wakili Kibatala akitaka mahakama hiyo iwaruhusu kuweka kiasi hicho cha fedha kwa sababu ombi hilo limekidhi matakwa ya kifungu cha 111(2) cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...