Madai ya kupoprwa haki ya Wazanzibari,2015, wahafidhina watambue Neno "Justification" na "Time cost"

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Bado kiwingu cha Uchaguzi wa 2015 na kilichotokea kinaendelea kuwatesa watawala wa Zanzibar. Kwa wanaofuatilia siasa za huko watakubaliana nami kwamba imekuwa vigumu kwa watawala kunyamazisha hali na kila baada ya muda mzuka unapanda jambo linalowafanya watawala kutaabika.

Si mara moja wala mbili Dr shein kama rais wa Zanzibar hulazimika kuhutubia na kurejea kutoa ufafanuzi kuwa yeye ndie rais na hawezi kungolewa. Wazanzibari wengi wanajiouliza kunani kiongozi wao kila wakati kulazimika kutamka hivyo? Bila shaka kuna kitu kinawanyima usingizi.

Takribani wiki tatu, dr shein alifanya ziara kisiwani Pemba na kuwataka wananchi kupuuza kauli za wapinzani kwamba karibuni watakabidhiwa nchi. Haikutosha juzi waklati anaadhimisha mwaka mmoja tangu aingie ikulu katika awamu ya pili alizungumzia hilo na kwamba hakuna wa kumngoa.

Nimetyanguliza hayo ili kuinesha hali halisi. Sasa turudi kwenye mada halisi.

Ukweli utabaki kama ulivyo kwamba siasa za kihafidhina ndio zimeifikisha Zanzibar hapo ilipo. Uchaguzi wa Marudio wa Machi, 20, 2016 ulikosa sababu za kuaminika na hivyo kukosa " Justification" neno hili Wahafidhina wanapaswa kulitambuwa. Dunia ya leo inahitaji ushawishi wa hoja. Uchaguzi wa 2015 kufutwa unawakosesha raha wahafidhina na kinachomtesa Dr Shein na wafuasi wake ni dhambi ya kukosa "Justification." Dunia haikutoshelezwa juu ya hoja za kufutwa uchaguzi ule ambao waangalizi wote wa ndani na nje walisifu kuwa ulikuwa huru na haki.

Wazanzibari wengi hawakumchagua Dr Shein kwa hali zote mbili. Uchaguzi wa Oktoba, 2015 ulionesha hivyo, na ule uliolalamikiwa wa Machi, 2016 haukuwa na uhalisi. Kilichofanyika ni mazingaombwe ya kihafidhina ambapo imearifiwa kuwa wananchi wengi hawakushiriki.

Mwangwi wa malalamiko ya kimya kimya na nguvu ya upinzani ilivyo kubwa inamnyima raha Dr Shein na watu wake ingawa anajificha kuonesha ukweli. Ndio maana nadhani kila baada ya muda hulazimika kutoa ufafanuzi wa uraisi wake.

SOMO KWA WAHAFIDHINA.

-Watu hawa watambuwe kwamba dunia inaendeshwa kwa principles maalum zilizowekwa na kwamba sio kila wakati utafanya yale yale kwa mbinu zile zile na ukaachwa.

-Watu hawa watambuwe kwamba subira ya wapinzani ina gharama kubwa kwa wapinzani wenyewe lakini ina madhara makubwa kwa wanyima haki . Maalim Seif na subira yake iliyotukuka kamwe haitapita bure na muda si mrefu mtalitambua hilo.

- Wahafidhina watambuwe kuwa mabadiliko ni lazima katika mifumo ya kilimwengu na huwezi kuzuwiya hilo. Watambuwe kwamba Zanzibar ilifanya mapinduzi, nchi ikaongozwa na decree za rais, ikaja Katiba, Kukaja chama kimoja, kukaja vyama vingi, ikaja awamu ya mshindi kuchukuwa na kuongoza yeye peke yake, kulifanywa mabadiliko ya katiba kuruhusu mashirikiano katika kuongoza nchi na kuja GNU.

- Wakumbuke mabadiliko hayo niliyotaja yaligharimu muda (Time Cost) na fedha za wahisani lakini yaliyotakiwa yakawa. Wakumbuke dunia inaweka matakwa yake mahala fulani na kwa Zanzibar pamechaguliwa GNU iwe ndio muundo wa uongozi. Mtambuwe kwamba kwenda kinyume na matakwa hayo hamtabaki salama kamwe na ni huo muda (time cost) ndio utawahukumu.

- Kukosa kwenu "justification" kwa kufuta uchaguzi wa 2015 na visingizio mlivyoleta havikuweza kubadilisha ukweli na msimamo wa ulimwengu juu ya haki ya maamuzi ya umma, Acheni muda upotee, endelezeni jeuri na kiburi, tisheni na kudinda lakini subira na gharama ya muda wa zaidi ya miaka 25 ya mabadiliko imewafichuwa na mmejulikana mlivyo. Nasema tena gharama hiyo itawaumbuwa muda si mrefu.

Jueni katika siasa kuna kitu " hope for the results" wenzenu walikubali kuwa wajinga wa kusubiri kuidhihirishia dunia vile mlivyo na kwa kukosa maono mliingia kichwa kichwa. Sitaki kutabiri juu ya kile kinachoendelea kwa sasa kuhusu mgogoro wa Zanzibar lakini najuwa jitihada zilizochukuliwa na dunia kabla ya 2015 zimetosha kuwaonesha mlivyo na sasa tunasubiri hiyo "Results"


Zanzibar njema ya ushirikiano ilipangwa, iliwezekana na itawezekana.


Kishada.
 
Back
Top Bottom