uzeebusara
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 657
- 514
Habari wana Jf
Nimeonelea kuleta wazo hili linalowahusiana na biashara ya usafirishaji mizigo hasa ya nje za nchi 'Transit Goods' kwenda nchi mbali mbali tuweze kubadilishana mawazo, kusaidiana katika kutafuta na kupata mizigo.
Biashara hii ina umuhimu sana katika kukua kwa uchumi wa nchi yetu japo kwa sasa haijakaa vema kutokana na kupungua kwa mizigo katika bandari zetu lakini naamini muda si mrefu itarudi katika hali yake ya kawaida
Hivyo basi nimeonelea ni vema kwa makampuni ya kuclear mizigo bandarini wawe wanaleta taarifa mbali mbali za mizigo iliyopo katika mzunguko tayari kwa kusafirishwa pamoja na ofa za bei zao na wasafirishaji wawe wanapata ahueni ya kuwakwepa madalali kwani wanashusha sana bei na vile vile kumekuwa na tatizo la madalali kukimbia na balansi ya mwisho pindi ukiishafanya kazi
Vilevile kupeana ushauri na gharama za mipakani na hata ndani ya nchi nyingine. Hapa nikiwa na maana kwa mfano lori lako lipo Ndola, Zambia na mzigo wa kurudi upo Chingola je Road Toll pale ni dola ngapi nk. Masuala ya upatikanaji wa mizigo ya kurudi toka nje ya nchi kuleta Tanzania na bei zake kwa usahihi. Karibuni katika mjadala
Nawasilisha