KIFUPI KUHUSU NDEGE AINA YA BOEING 737 MAX
Ndege za Boeing aina ya 737 MAX ilitumbukia katika moja ya janga kubwa zaidi katika historia ya usafiri wa anga kufuatia ajali mbili mbaya zilizosababisha kusitishwa uendeshaji wake kwa muda.
Hali hiyo ilisababishwa na 'Software' (MCAS) yenye lengo la kudhibiti tabia mpya inayozalishwa na ndege katika upaaji kwasababu ya injini mpya kubwa, mara nyingine ilidhibiti tabia hiyo nje na maamuzi ya rubani.
Licha ya hiyo, 737 MAX ilirudi kuendelea kutoa huduma baada ya marekebisho na maboresho makubwa na kubaki kuwa moja ya ndege maarufu na salama zaidi duniani, kwa historia na mtandao mkubwa wa waendeshaji na wauzaji.
MAX inakuja moja kwa kushindana na mpinzani wake mkubwa 'Airbus' familia ya 320NEO' na pia Embraer toleo za EMR190s.
Boeing 737 MAX ni kizazi cha nne cha familia ya ndege zake za Boeing737 Bodi nyembamba (Narrow body)
MAX inajumuisha injini mpya na maboresho mengine ya teknolojia kulinganisha na vizazi vyake vingine vilivyopita kama:
Boeing 737-100/200 (kawaida)
Boeing 737-300/400/500 (Classic)
Boeing 737-600/700/800/900 (Next Generation "NG"
Boeing 737 MAX iliongeza ufanisi kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi, kuongezeka kwa idadi ya abiria, kupunguza matumizi ya mafuta na vichafuzi kwa asilimia 20 huku ikipunguza kelele kwa asilimia 50% na pungufu ya asilimia 14% gharama za matengenezo.
Boeing 737 MAX ni maarufu zaidi kwa muonekano wa ncha yenye V kwenye mabawa (winglets).
Toleo la Boeing 737 MAX ilianzishwa Desemba 2011 baada ya kupokea oda kutoka shirika la ndege Southwest.
Max ya kwanza yenye namba 42554 na usajili N8701Q ilifanya mruko wa uzinduzi mnamo Januari 29, 2016, kutoka Renton, Washington.
Matoleo ya MAX, upakiaji abiria viwango vya juu pasipo kuzingatia madaraja;
B737-7 hadi abiria 172
B737-8 hadi abiria 189
B737-9 hadi abiria 220
B737-10 hadi abiria 230
Mashirika yanaendesha ndege hii ni kama AerCap, Aviation Capital Group (ACG), Copa, Donghai, GE Capital Aviation Services, Lion Air, Malaysia, TUI Group, United Airlines, Xiamen Airlines, Ethiopian, Air Tanzania n.k
Shirika la ndege Air Tanzania linategemea kupokea ndege yake ya kwanza aina ya Boeing 737-9 MAX siku ya 03/Oktoba/2023 kwa mujibu wizara ya uchukuzi.
Makala fupi na:
#Airwaysmag
#Admin mkuu/Aviation Media Tanzania
[emoji328]
Kwa hisani ya mtandao
Sent using
Jamii Forums mobile app