𝗡𝗗𝗘𝗚𝗘 𝗛𝗨𝗞𝗔𝗧𝗔𝗝𝗘 𝗞𝗢𝗡𝗔 𝗔𝗡𝗚𝗔𝗡𝗜?
{Ufafanuzi mwepesi}
Ndege inakata kona kutumia pedeli mbili {kushoto na kulia} anazokanyaga rubani.
Pedeli hizo {#foot_pedal} ndiyo zinakata kona tairi ya mbele na kielekezi cha mkia uliosimama {#rudder}.
Rubani akikanyaga pedeli ya kushoto tairi itakata kushoto na kinyume chake.
Lakini pedeli hizo zimegawanyika mara mbili, endapo zikikanyangwa kwa upande wa juu unapata #brake za tairi.
Kwahiyo rubani anatumia upande wa visigino vyake kusukuma 'pedal' ili kukata kona au kukanyaga pedal hizo kwa upande wa vidole vya miguu kukamata 'brake'
Inapokuwa chini ndege inakata kona kwa kutumia tairi ya mbele (ukiacha ndege za #trail_dragger} na ikiwa angani tairi haina kazi tena na inatumika 'rudder' pekee kukata kona kwa kukinzana na upepo upande wa kushoto au kulia mkiani.
Kwa upande wa mbawa kuna vielekezi vilivyo karibu na ncha kulia na kushoto viitwavyo "#ailerons" ambavyo vinafanya kazi kwa kutumia usukani wa ndege {#steering_yoke/#flight_yoke} kukata kulia au kushoto.
Pia usukani huu ukivuta au kusukuma ndiyo unainamisha au kuinua pua ya ndege kwa kutumia kielekezi cha mkia uliolala {#elevator}
Vielekezi vya mbawa 'Ailerons' hutumika zaidi angani wakati ndege inahitaji kukata kona kwa kulala {#bank} na mara nyingi vinafanya kazi kinyume.
Ndege ikitaka kukata kona ya kulia basi kielekezi cha mbawa ya kulia 'Aileron' kitainuka juu kikinzana na hewa ipitayo na kulazimisha mbawa kwenda chini wakati huo kielekezi cha kushoto kitainama chini kukinzana na hewa ipitayo chini na kusukuma mbawa juu.
Hapo utaona ndege inalala upande wa kulia na kinyume chake.
Ndege huwa haikamiliki kukata kona kwa kulala kulia au kushoto, hapo itakuwa inateleza tu angani kuelekea mbele {#slipping} kama vile gari iliyokata kona ghafla kwenye utelezi.
Kwasababu hiyo rubani anakata kona yake vizuri kwa kujumuisha pamoja vielekezi vyote "Ailerons" kulaza ndege upande aliokusudia, atasukuma pedeli ya upande aliolazia ndege ili rudder mkiani ipeleke pua ndege alipokusudia.
Hapo utaona ndege inakata kona nzuri kwa kulala upande.
Uchambuzi ujao utakuwa kuhusu vifaa vinavyosaidia ndege kupaa na kutua kwa mwendo mdogo "#lifting devices"
{#Flaps & Slats} na brake za kukinzana na upepo {#speedbrake au #Spoilers}
Tafsiri kutoka:
#boldmethod
#Aerodynamics_syllabus
Picha kw hisani ya mtandao.
View attachment 2665463View attachment 2665464View attachment 2665465
Sent using
Jamii Forums mobile app