TAA ZA NDEGE
Mifumo yote ya taa za vyombo vya moto inakusudia kupunguza uwezekano wa kugongana/Usalama wa chombo na watu.
Taa za ndege pia ni hivyo, uifanya ionekane zaidi na ndege nyengine au vyombo vingine vya moto/watu, wakati ikiwa chini au kupaa angani.
TAA ZA URAMBAZAJI
(#Navigation_Lights)
Hizi zinajumuisha taa mbili hadi tatu, nyekundu kwenye ncha ya mbawa ya kushoto, taa ya kijani ncha ya mbawa ya kulia na nyengine taa nyeupe kwenye mkia wa ndege.
Hapa ngoja nishuke kidogo..
Taa hizi mara nyingi huwa zinatoa taarifa kwa rubani/ chombo kingine angani kuwa ndege ipo upande gani.
Mfano:
Hasa usiku,
Ukiona taa ya kijani ipo kushoto kwako na nyekundu kulia tambua inakuja ulipo.
Ukiona kinyume chake ujue inaelekea mbali na ulipo.
Ukiona taa nyekundu tupu(sio kimulimuli) ujue inapita kuelekea kushoto kwako na ukiona ya kijani tupu inaelekea kulia kwako.
KIMULIMULI
(#Beacon)
Hizi ni taa zenye rangi nyekundu na zinaweza kuwaka au kuzunguka ili kutoa mwangaza wa onyo na inaweza kuwa juu ya ndege, tumboni au juu ya mkia.
Kifupi taa nyekundu ya kimulimuli huwa inatuonya au kutupa tahadhari juu ya hatari au kutosogelea chombo/sehemu husika.
'FLASHI'
(#Strobe)
Au tunaitaga "mweku mweku" wakuu au sio?
Hizi taa ni nyeupe zenye mwangaza mkali wa kuwaka na kuzima au kupokezana (flash)
Taa hizi kawaida huwekwa karibu na ncha za mbawa pia inaweza kuwa na mkiani.
Hizi zinaongeza muonekano wa ndege hata ikiwa mbali na unaweza kutofautisha kati ya ndege na nyota.
Usiku usipokuwa makini unaweza kuona ndege ukajua nyota.
TAA ZA KUTEMBEA NDEGE
(#Taxi_Lights)
Hizi ni taa za kiwango cha kati ambazo zinaweza kuwekwa kwenye pua ya ndege au mwanzo wa mbawa karibu na inapokutana na kiwiliwili cha ndege.
Hizi kazi yake kumulika ndege inapotembea kwenye njia zake za mchepuko kutoka barabara kuu (taxiways)
TAA ZA KUFUATA KONA
(#Runway_Turnoff_Light)
Taa za Turnoff zinafanana na taa za kutembea ndege isipokuwa taa hizi huweza kupinda kuangaza/kumulika kule tairi la mbele linapokata kona.
TAA ZA KUTUA
(#landing_Light)
Hizi ni taa zenye mwangaza wa kiwango cha juu zinazotumika kuangazia barabara ya kuruka na kutua na pia kuwezesha ndege kuonekana na marubani wengine kirahisi inakuwa inapaa au na kutua.
Huwa zinamulika mbele kwa mwangaza mkali zaidi.
TAA KAGUZI MBAWA
(#Wing_Inspection_Light)
Taa hizi zenye mwangaza wa kutosha zimewekwa pembeni ya kiwiliwili (fuselage)na zinamulika nyuma kuangazia mbawa pamoja na injini.
TAA ZA NEMBO
(#Logo_Lights)
Hizi ni taa zinazomulika nembo ya ndege mkiani.
Mashirika na makampuni mengi ya usafiri wa anga hupenda kuweka nembo zao kwenye mkia uliosimama wima.
#Admin
Sent using
Jamii Forums mobile app