Machozi! Kwanini mmemchinja mama yangu?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,814
34,198
Mtoto Allan akiwa amekumbatia picha ya marehemu mama yake, Anethe Msuya.

STORI: MWANDISHI WETU, WIKIENDA

DAR ES SALAAM: ‘Kwa nini mmemchinja mama yangu?’ Ndiyo maneno yaliyokuwa yakimtoka mara kwa mara mtoto, Allan Kimario (4) kila alipokumbuka tukio la mama’ke, Anethe Msuya (30) kuchinjwa shingoni hadi kufa na watu wasiojulikana, nyumbani kwake, Kigamboni, Dar.

KUMBUKUMBU FUPI
Anethe alichinjwa Mei 26, mwaka huu na watu watano waliovamia nyumbani kwake usiku wakiwa wamefunika nyuso kwa soksi nyeusi.

SIKU YA KUAGA MWILI

Mwili wa Anethe ulisafirishwa, Mei 30, mwaka huu kwenda Kijiji cha Kairo, Mererani wilayani Simanjiro, Manyara kwa mazishi baada ya kuagwa kwa machozi yasiyo na mfano huko Salasala jijini Dar. Kwa mujibu wa baadhi ya ndugu wa marehemu, mtoto wake huyo kila alipokuwa akirudiwa na uelewa wa kilichomkuta mzazi wake huyo, alikuwa akiuliza ni kwa nini watu hao walimchinja mama yake?!

“Ni swali gumu kulijibu lakini ukweli ni kuwa, huyu mtoto ameumizwa sana. Mara nyingi amekuwa akilia kwa uchungu na kulala akiwa amekumbatia picha ya mama yake ya enzi ya uhai, jambo lililowatoa watu machozi
msibani.
“Kuna wakati anakuwa kama amesahau na hajui nini kinaendelea, lakini akikumbuka tu, anapoteza amani na uso unakosa furaha. Hasa ndugu anaowafahamu walipokuwa wakilia.”

SWALI LA KILA MARA

“Hata siku ya kuuaga mwili, alikabidhiwa picha moja ya mama yake na akaonekana yupo sawasawa, lakini wakati anapita kuuona mwili huo, alilia na baadaye swali lake lilijirudia tena ni kwa nini walimchinja mama yake?”
kilisema chanzo kimoja juzi baada ya kurejea kutoka mazishini.

MAKUBWA KATIKA MAISHA YAKE
Habari zaidi zinasema kuwa, ukiacha tukio la mama yake kuchinjwa chumbani huku yeye akiwa amelala sebuleni baada ya watu hao kumpulizia dawa inayosadikiwa ni ya usingizi, aliwahi kukumbana na tukio lingine zito. Dada wa Anethe aliyetajwa kwa jina la Antuja inadaiwa kwamba, aliwahi kumwagiwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni sumu wakati akiwa amelala chumbani na mtoto huyo maeneo ya Mbezi-Beach, Dar.



Mtoto hakuathirika lakini mama mkubwa huyo aliathirika na ikawa ni moja kati ya matukio mengi yaliyoonekana kuiandama familia hiyo.
“Hebu piga picha Allan katika kukua kwake atakuwa na kumbukumbu ya mambo mangapi mazito?” kilihoji chanzo hicho.

KILICHOWAUMIZA WENGI

Wengi wa waombolezaji msibani walikuwa wakimhurumia mtoto huyo kwamba, katika umri mdogo wa miaka 4 amempoteza mama kwa njia ya ukatili huku yeye mwenyewe akili zake zikiwa zinachambua tukio na wakati mwingine kuacha.

“Kama utakumbuka, Allan ndiye aliyekwenda kwa jirani kueleza kwamba, mama yake amelala na kila akimwamsha
haamki wakati yeye anataka kwenda shule.
“Majirani walipokwenda kuchungulia walimkuta amelala chini kwenye dimbwi la damu. Ina maana Allan aliona lakini akili zake zilishindwa kujenga picha kamili kwamba, mama yake amechinjwa na hakuwa hai!
“Na kuna uwezekano mkubwa kwamba, amekuwa akisikia kwa watu wakisemasema kuhusu tukio lile ndiyo maana na yeye linamwingia na kutoka,” kilisema chanzo.

WAFANYAKAZI WENZAKE WAMWAGA MACHOZI

Mamia ya waliofika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mashariki, Salasala jijini Dar wakiwemo wafanyakazi wenzake wa Wizara ya Fedha alikokuwa akifanya kazi marehemu, walishindwa kujizuia na kuangua vilio walipokuwa wakipita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili huo kutoa heshima zao za mwisho.

KIFO CHA KAKA YAKE
Agosti 8, 2013, kaka wa Anethe, ambaye alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa madini jijini Arusha, Erasto Msuya ‘Bilionea’, (43) aliuawa kwa kupigwa risasi 22 maeneo ya Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (Kia), Kilimanjaro huku kisasi kikitajwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wenzake. Hivyo, wengi wamekihusisha kifo cha Anethe na kumwagiwa sumu kwa dada yake kama sehemu ya mwendelezo wa kisasi katika familia hiyo.
 

Attachments

  • Mtoto Allan.jpg
    Mtoto Allan.jpg
    125.4 KB · Views: 105
  • Mtoto hakuathirika lakini mama mkubwa huyo.jpg
    Mtoto hakuathirika lakini mama mkubwa huyo.jpg
    133.7 KB · Views: 107
  • SIKU YA KUAGA MWILI.jpg
    SIKU YA KUAGA MWILI.jpg
    161.6 KB · Views: 128
  • Kama utakumbuka, Allan.jpg
    Kama utakumbuka, Allan.jpg
    140 KB · Views: 108
  • SWALI LA KILA MARA.jpg
    SWALI LA KILA MARA.jpg
    202.5 KB · Views: 119
Duh!Wallah ni maumivu yasiosahaulika..ama kweli dunia imebeba mengi tuyajuayo na tusiyoyajua..Swali hilo la mtoto nadhani limebaki kitendawili hata kwa wakubwa zake katika familia na jamii kwa ujumla..lakini Mungu anajua zaidi,acha tumkabizi yeye ikosiko ataliweka wazi.
 
Mpka leo police hawajapata mhusika.....ila maandamano ya upinzani intelijensia yao huonyesha haraka sana kua fujo zitatokea.....kazi zimewashinda siasa ndio wanaiweza



Usiongeee usivyovijua??? Hata habari hufuatilii unaongea ongea tuu.
 
Ndo ninapokuja kuwashangaa hawa jamaa. Eti oh! tunalinda raia na mali zao...ndo nini wanafanya sasa kama tangu tar 26 may mpaka leo hawajawapata wahusika? shame upon thee.........
Intelijensia ya mwendo kasi......kule mwz wameenda jeshi zima plus waandishi utafikiria walikua wanafanya mazoezi......
 
Huyu mtoto ananiuma kupitiliza kila nikijaribu kuvaa viatu vyake pamoja na sharubu zangu zilizojaa mvi nashindwa kuvumilia. Mungu ampe nguvu na kumsahaulisha.
Hilo tukio huwa halisahauliki litaendelea kukaa kichwani mwake daima kama lilivyo.
 
Pole Sana dogo hasa ktk kipind hiki kigum cha kupotelewa na mama yako kipenz najua unauchungu Sana kuhus hilo lkn hata sisi tunauchungu Sana lkn tunaamin kua maandiko yatafanya kaz kua atakae ua kwa upanga nae atauliwa kwa upanga mwenyez mungu ampunguzie adhab ya kabur mama yako kipenz Amina.
 
Duh!Wallah ni maumivu yasiosahaulika..ama kweli dunia imebeba mengi tuyajuayo na tusiyoyajua..Swali hilo la mtoto nadhani limebaki kitendawili hata kwa wakubwa zake katika familia na jamii kwa ujumla..lakini Mungu anajua zaidi,acha tumkabizi yeye ikosiko ataliweka wazi.
Ni maumivu makali mno... Nimeshindwa kuisoma yote maana duh watu ni wakatili sometimes.
 
Mpka leo police hawajapata mhusika.....ila maandamano ya upinzani intelijensia yao huonyesha haraka sana kua fujo zitatokea.....kazi zimewashinda siasa ndio wanaiweza
Waxha akili mbovu mbovu za ki Ukawa ! mkuda wewe !
 
Hili tukio limekua mwiba mkali kwangu wakati mwingine naogopa kufungua hata uzi unaohusu habari hii...nikimfikiria huyo mtoto machozi yananitiririka mno,, mbona tumekua wakatili kiasi hiki jamani
Mtoto amebebeshwa picha yenye uchungu mkubwa maisha yake yote..Mungu ninakulilia baba mfariji mtoto huyu mana kwa hakika umemuona ana uwezo wa kulishinda hili
 
Back
Top Bottom