Neno Machinga Lina uhusiano na wamakonde kutoka mkoa wa Mtwara kwani miaka ya 19 kwa wingi wao walihamia mkoa wa Dsm hasa mtaa wa kongo wakijihusiha na biashara ndogo ndogo kama vile kuuza mifuko ya plastiki aka Rambo , walikuwa na umoja na kubebana sana kuanzia kibaruani mpaka kwenye malazi.
Kwenye chumba kimoja walikuwa wanalala mpaka kumi na kwa mama LISHE walikuwa wakienda kikundi wakinunua ukoko na maharage na kudanganya tumbo. Walikuwa hawana mitaji zaidi ya uaminifu kwenye maduka ya jumla.
Baada ya muda wakaanza kuonekana mtaani wakitembea kama enka wakiwa na bidhaa ndogondogo kuanzia sufuria, nguo za Bei rahisi na viatu.
Asili ya wamachinga hawa hawana wajualo kuhusu mikopo, hawa huwa wanahitaji sehemu ya kufanyia biashara